Data za Unemplymenet rate kwa nchi za kwetu siyo za uhakika kwa vile tafsiri halisi ya emplyoment haijulikani. Kwa mfano, hapa Tanzania umachinga nao ni employment; na kwa data za namna hiyoinaonekana kuwa hadi December mwaka 2018, unemployment ya Tanzania ilikuwa ni kati ya 9.9% na 12.9%. Rwanda uneployement rate ilikuwa mi kati ya 1.0% na 17.8%, wakati Burundi ilikuwa ni kati ya 1.5% na 2.1%. Data za namna hiyo zina uncertainity kubwa sana hasa kwa vile nchi zetu hazina uhakiki wa kutosha kuhusu maisha ya raia wake. Tunaweza kuwa na data za mauzo na mapato kwa vile namba zake zinapatikana kirahisi, lakini data za kuhusu maisha ya raia hatuna kabisa kwa vile hatuna mfumo wa kodi unaouhisha mapato ya raia wote, kiasi kuwa mwisho wa mwaka kila raia anawakilisha tax return zake.
Kupima kiwango cha uneplyment harakaharaka, hebu angalia kunapotokea jambo lolote hata dogo sana uone jinsi watu watakavyojaa pale mpaka askari waingilie kusimamia. Wote hao ni kwa sababu hawana jambo la maana la kufanya. Angalia watu wanaojaa airport eti kuipokea ndege mpya; majuzi niliangalia video kuwa Harmonize anamwendesha mpenzi wake kwa baiskeli huko kijijini kwao umma mzima wa watu walikuwa wanamkimbilia kumwona kwa vile hawakuwa na kazi ya kufanya.