Tanzania vs Guinea: Tanzania yaaga mashindani baada ya kutoka sare ya mabao 2 kwa 2 dhidi ya Guinea

Na nahisi vingi vya vile vitoto vya Guinea vimetokea academy maana timu yao kubwa huko ni Horoya tuu ambayo imeanza kuwiki miaka ya karibuni but vina akili ya mpira seems wamewekeza.kwa.ajili ya kuuza wachezaji nje ya nchi ,huku Bongo hatuelewekagi kipi ni kipaombele si kwenye maendeleo ya kawaida,siasa au michezo
 
Giroud kombe la dunia alifunga magoli mangapi? Kwaajili taarifa yako bila Nchimbi na ule usumbifu wake pale mbele inawezekana tungekufa mapema tu,yes hey ndiye forward inatakiwa afunge,Ila huwezi kubeza kazi yake pale mbele
Nchimbi ndio fowadi pekee aliyesumbua Jana,zaidi ya mara 4 kacollide na kipa na kipindi cha pili alichoka sema Lyanga alikuwa mzigo tuu na Mhilu bora angeingia toka kipindi cha kwanza asaidiane na Nchimbi maana ana Kasi
 
Hata ukiwaona vitoto vidogo hivi kitu nilichopenda walivyobadilika kutoka draw walivyofungwa 2 unaona team wanatafuta nini pressure unajuwa tu hapa goal lipo
 
Nchimbi ndio fowadi pekee aliyesumbua Jana,zaidi ya mara 4 kacollide na kipa na kipindi cha pili alichoka sema Lyanga alikuwa mzigo tuu na Mhilu bora angeingia toka kipindi cha kwanza asaidiane na Nchimbi maana ana Kasi
Lyanga jana tangu 1st half hakuonekana,kwa nature ya gamejana nadhani,Sub ya Lyanga angeingia Kaseke japo hana accuracy pass sana ila anakaba
 
Tangu mwanzo wa michuano tatizo ni kocha
Mimi kwa maoni yangu..... ninawapongeza wachezaji walicheza vizuri...na kocha naona tumpe muda yupo vizuri...tulikosa technics za kilinda goli...mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni.
 
Kocha wa sasa hana viwango kabisa,atafutwe Kocha mpya mwenye viwango anaezungumza na wachezaji muda wote wa mchezo Na kuwakumbusha majukumu yao staili ya Marcia Maximo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…