Nani huyuuu, Mandela labda, sina uhakika aliwahi sema " Success is going from one failure to another without loosing hope" yaani kwa kiswahili " Mafanikio ni kupitia kufeli sehemu moja na kufeli sehemu nyingine bila kukata tamaaa" Kama hivyo ndivyo basi naamini tusiikatie tamaa stars tupe muda tu, mbona imechukua ubingwa wa Afrika Mashariki na Kati? Tusidharau mafanikio madogo kwani ni hayo hayo ndio yanaashiria yale makubwa. Naamini miaka ijayo Stars inaweza kuwa timu tishio sio afrika Mashariki na Kati tu bali afrika nzima na dunia. Tusiikatie tamaa!