Tanzania vs Yemen

Tanzania vs Yemen

Kilakshari

JF-Expert Member
Joined
Dec 13, 2008
Posts
350
Reaction score
20
hii mechi inaonyweshwa live online? naomba mnijuze wadau! Asanteni sana!
 
hii mechi inaonyweshwa live online? naomba mnijuze wadau! Asanteni sana!

Kwa mimi unisamehe...nachukia mpira sana, maana sitaki ugonjwa wa moyo! Kuna raia mmoja huku Mwanza amemwumiza fuvu la kichwa mwanae kwaajili ya Mpira wa ,,,sijui Arsenal na nini sijui...!Ukitaka kunikamata ongelea mambo ya pool bana...lol!
 
Ndo hivyo tena,

Tulitunguliwa 2 - 1 na Yemen.

Bao la kwanza la Yemen lilifungwa dakika ya 13 kipindi cha kwanza na mchezaji Tamer Hanash kwa mkwaju wa penati. Baadae Taifa Stars wakasawazisha dakika ya 34. Haikuchukua hata muda Yemen wakaongeza la pili dakika ya 37.

Lakini kipindi cha pili stars walionekana kusimama kidete na wangetumia vema nafasi walizozipata basi wangeweza kusawazisha na kulazimisha sare ya 2 kwa 2, mambo hayakuwa hivyo na wakalala 2 - 1 mbele ya Yemen.
 
Duh yale yale 2-1 tatizo ni wachezaji au tatizo ni kocha kuwaacha wachezaji wenye vipaji na kusingizia nidhamu?
 
Duh yale yale 2-1 tatizo ni wachezaji au tatizo ni kocha kuwaacha wachezaji wenye vipaji na kusingizia nidhamu?

Laana za Kaseja na Athumani Iddi zinafanya kazi yake vema.
 
Ndo hivyo tena,

Tulitunguliwa 2 - 1 na Yemen.

Bao la kwanza la Yemen lilifungwa dakika ya 13 kipindi cha kwanza na mchezaji Tamer Hanash kwa mkwaju wa penati. Baadae Taifa Stars wakasawazisha dakika ya 34. Haikuchukua hata muda Yemen wakaongeza la pili dakika ya 37.

Lakini kipindi cha pili stars walionekana kusimama kidete na wangetumia vema nafasi walizozipata basi wangeweza kusawazisha na kulazimisha sare ya 2 kwa 2, mambo hayakuwa hivyo na wakalala 2 - 1 mbele ya Yemen.

Haya warudi nyumbani sasa naona wameshatalii vya kutosha! Sijui huwa kuna report yeyote inatolewa baada ya wao kurudi ili tujue mafanikio yao katika utalii wao
 
Ha ha ha nilikuwa nachek position ya YEMEN ktk rank za FIFA nikakuta ni 139 na TZ ni ya 99.
 
Huyo Maximo ndio anadai timu inajiandaa na kombe la chalenji kwa staili hii, kweli hamna kitu coz yemen haistahili kutubania kiasi hicho tena michezo yote miwili halafu tuwe na fikra kuwa tunataka kuishinda timu ngumu kama misri, nigeria nk. Timu ingesukwa upya, wanaofaa waitwe bila kujali mambo yasio na msingi kwenye soka
 
Ha ha ha nilikuwa nachek position ya YEMEN ktk rank za FIFA nikakuta ni 139 na TZ ni ya 99.
Yaani inaboa mkuu na kutia aibu vibaya mno coz kuna rafiki zangu raia wa Yemen tupo nao hapa hata kuongelea juu ya hilo nashindwa coz timu yao ipo chini kisoka ila wanatubuluza tu, na wao sasa wameshajua mahali gani pa kupandia kwenye viwango vya FIFA, wakitaka kupanda tena au kujiweka pazuri watamuita tena kibonde wao wamchambue, duh kweli hii timu bado ni kichwa cha mwendawazimu!!
 
Mshaambiwa tatizo si Maximo, tatizo ni vyombo vya habari... Sijui vinacheza au kufundisha soka?

Aaah, heri niendelee kushabikia Chelsea mie, uzalendo mbaya... Timu ikifungwa kama umemwagiwa maji ya betri 🙁
 
Naona similarities nyingi kati ya Taifa Stars na serikali ya Tanzania. Ufujaji tu wa fedha, wachezaji vihiyo na (ma)bosi asiyetaka kuwajibika
 
Mshaambiwa tatizo si Maximo, tatizo ni vyombo vya habari... Sijui vinacheza au kufundisha soka?
si aliletwa na JK labda wanaogopa kumtimua teh teh..Timu tumeipa support ya khari na mali lakini bado inacheza utumbo...kocha hana first eleven kwa miaka mitatu...ngoja chaleji inakuja sijui watatoa sababu gani tukishindwa kulichukua kombe...
 
hivi washabiki tukiamua kugomea kwenda kutizama mechi za taifa stars zote mpaka hapo Kaseja ataporudishwa inama hatutosikilizwa na TFF?
 
Back
Top Bottom