Tanzania: Wagonjwa wapya 53 wa COVID-19 wathibitika, idadi yafikia 147 (Aprili 17, 2020)

Tanzania: Wagonjwa wapya 53 wa COVID-19 wathibitika, idadi yafikia 147 (Aprili 17, 2020)

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760
Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu amesema idadi hiyo imefikiwa baada ya Wagonjwa wapya 53 kukutwa na #COVID19

Wagonjwa wote ni Watanzania ambapo 38 wanatoka Dar; 10 wanatoka Zanzibar; Kilimanjaro 1; Mwanza 1; Pwani 1; Lindi 1 na Kagera 1

Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu ametoa idadi hiyo huku akisema Wagonjwa 4 wanapatiwa matibabu ya Wagonjwa mahututi kutokana na kusumbuliwa na matatizo mengine ya kiafya

Aidha, wagonjwa 131 wanaendelea vizuri na tayari Wagonjwa 11 wamepona maambukizi ya #CoronaVirus

Wananchi wenye dalili za ugonjwa huo wametakiwa kuacha kwenda Hospitali ya Taifa Muhimbili na badala yake Serikali imeamua kutumia Hospitali ya Rufaa ya Mkoa, Amana kama Kituo maalum cha matibabu ya Ugonjwa wa #COVID19

Serikali imesema hospitali hiyo ndiyo hospitali kuu ya rufaa ya Kitaifa, ina wagonjwa wengine na pia ndio inatoa matibabu mengine ikiwemo upasuaji wa figo, moyo, mifupa na mishipa ya fahamu

1.jpg


2.jpg


 
Wametoka sehemu mbali mbali za Tanzania hi ni hatari sanaa manaake ugonjwa umesha enea nchi nzima........naomba Raisi achukue hatua zingine zaidi ya maombi, ili hu ungojwa usiingie ndani sana vijijini ambao wana matatizo ya afya mengi
 
Hali itakuwa mbaya jamani kwa sababu ya tamaa, JP ni dhahiri hawezi kupambana na majanga kabisa alishaambiwa mapema kuwa mipaka ifungwe haraka watu wazuiwe kuingia nchini Magari ya mizigo Meli za mizigo na Ndege za Mizigo ndio ziendelee tu kuingia na kutoka ili uchumi usidorore na watu wa ndani kazi ziendelee. yeye akaweka tamaa ya pesa mbele , Wageni kutoka China na ulaya wakawa wanaingia kiholela tu na kuachwa kwenye mahoteli

Walivyoambiwa wakasema kuwa wachina ni ndugu zetu hatuwezi kuwazuia, wakasema tena utalii ukifa tutakosa mapato,Watu wakawa wanaingia nchini kiholela wanaenda kulazwa kwenye mahoteli wakitoka ulaya alafu wanajichanganya na watu hovyo hovyo mwishowe Gonjwa Likapata nafasi ya Kupenya mitaani kirahisi na limeanza kututafuna.

Mambo yamekuwa mabaya Ajira zimeanza kupukutika vifo vimeanza na Jp kaenda kujificha chattto alafu anawaambia watu wasali wakati aligoma kuchukua Tahadhari za mapema, Mungu mwenyewe anasema jisaidie kwanza nami nikusaidie, Huko Israel ,Italy , Saudi Arabia ndio kusali kulipoanzia lakini wana hali mbaya sisi tunaleta masihara.

Jp alitakiwa atoke Hadharani mapema kuweka mikamati kama Museven na Kenyata walivyofanya, Hili gonjwa kama limewapata watu wazito Duniani basi tujue hamna aliye salama na ndio maana Kenyata na Museven walikuwa kama machizi kufanya maamuzi magumu ya mapema huku Raisi wetu karelax tu jamani

Hili gonjwa litatuletea janga ambalo hatujawahi kushuhudia,Tumeshaingia kwenye ulimwengu mwingine utakaosomwa kwenye historia mbaya na kizazi kijacho ni swala la muda tu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Waziri alitahadharisha hili jambo. Hatujafikia peak bado.

Wiki hii na wiki ijayo ndio itatupatia picha halisi ya tatizo.

Hadi kufikia May tutakua tumefikia peak na maambukizi yataanza kupungua iwapo tu tutacbukua tahadhari kama za Uganda.

Maombi hayana nafasi sasa.

Huu ndio wakati serikali inatakiwa kuonyesha kwa vitendo kua kweli ina akiba ya kuemdesha nchi kwa miezi 5 wakati wa dharula maana kila siku hua wanasema hivyo, bahati mbaya dharula imeingia ila inaonekana hakuna hela ya kuemdesha serikali.

Serikali kukataa kuzuia na kufunga biashara wakati huu ni ushahidi kua haiwezi kuendesha nchi kwa miezi 5 kwa sababu hawana hela.
 
Back
Top Bottom