Mkalukungone Mwamba
JF-Expert Member
- Aug 29, 2022
- 3,141
- 7,205
Kodi za wananchi zimefanya kazi, sasa tuone mabadiliko ya kweli kwenye hili.
================
Tanzania imekuwa taifa la kwanza barani Afrika kutumia Kombe la Dunia 2026 nchini Canada, katika jiji la Toronto, kama jukwaa kubwa la kutangaza sekta yake ya utalii.
Malori yenye mabango ya kampeni ya “Destination Tanzania” yameonekana yakizunguka maeneo mbalimbali ya jiji hilo, yakionesha vivutio vya utalii kama Serengeti, Mlima Kilimanjaro, Zanzibar na Bonde la Ngorongoro, huku yakivutia hisia za mashabiki wa soka na wageni kutoka mataifa mbalimbali.
Kampeni hiyo inakuja wakati Tanzania ikijiandaa kuwa mwenyeji wa AFCON 2027, kwa kutumia hadhira kubwa ya kimataifa ya Kombe la Dunia kutangaza nchi kama moja ya vivutio bora vya utalii duniani.