N'yadikwa
JF-Expert Member
- Aug 10, 2014
- 8,308
- 12,812
Tanzania tunaelekea kufanya jambo kubwa kupitia mradi wa reli ya kisasa ya SGR. Lakini baada ya kukamilisha SGR, nina pendekezo Serikali iandae project nyingine kubwa ya kimkakati ya kujenga barabara kuu za njia nne (dual carriageways) kwenye route muhimu zote za nchi yetu zinazobeba uchumi wa taifa.
Hii inaweza kuwa agenda ya taifa ya mwaka 2030–2035.
Barabara ninazopendekeza zipewe kipaumbele ni:
• Dar es Salaam – Namanga
• Dar es Salaam – Tunduma
• Dar es Salaam – Rusumo
• Dar es Salaam – Mwanza
• Tunduma – Mpanda
• Mwanza – Rorya
• Dar es Salaam – Tanga Port
• Dar es Salaam – Mtwara Port
Kwa mtazamo wangu, moja ya changamoto kubwa inayochelewesha movement ya uchumi wetu ni miundombinu ya barabara kuwa nyembamba kwenye njia kuu za biashara na usafirishaji.
Leo hii malori, mabasi, magari binafsi na mizigo kutoka bandarini vyote vinatumia njia zilezile ambazo ni njia mbili za mpishano zenye msongamano mkubwa.
Hali hii:
• Inachelewesha usafirishaji wa bidhaa
• Inaongeza gharama za biashara
• Inasababisha ajali nyingi
• Inapunguza ufanisi wa bandari zetu
• Inachelewesha uwekezaji na ukuaji wa viwanda
Tukijenga mtandao mkubwa wa barabara za njia nne, Tanzania inaweza kupiga hatua kubwa sana kiuchumi ndani ya muda mfupi.
Faida zake zinaweza kuwa:
• Kuongeza kasi ya biashara ndani na nje ya nchi
• Kuunganisha kwa ufanisi bandari na masoko ya kikanda
• Kuvutia uwekezaji mkubwa wa viwanda
• Kupunguza gharama za usafirishaji
• Kuchochea utalii na biashara za mipakani
• Kufungua fursa mpya za ajira na uchumi wa mikoa
Pia, napendekeza miradi hiyo ijengwe kwa viwango vya juu sana vya ubora vinavyoendana na uzito wa mizigo tunayobeba kutoka bandarini.
Kwa sasa baadhi ya barabara zinaathirika haraka kutokana na uzito mkubwa wa malori na mvua ikinyesha kidogo tu.
Lami nyingi zinaharibika mapema na kuongeza gharama za matengenezo kila mara.
Suluhisho ni kuanza kujenga kwa standard za muda mrefu zaidi.
Maeneo korofi, yenye mizigo mikubwa au yanayopata mvua nyingi yajengwe kwa barabara za zege (concrete roads) ili kuongeza uimara na kupunguza gharama za matengenezo ya mara kwa mara.
Tanzania ina nafasi ya kuwa kitovu kikubwa cha biashara na usafirishaji Afrika Mashariki na Kati na ukanda wote wa SADC, sasa ili tuwe vema zaidi barabara za haraka pia ni muhimu sana.
SGR ni mwanzo mzuri, lakini mtandao mkubwa wa barabara za kisasa unaweza kuwa game changer nyingine kubwa zaidi kwa uchumi wetu.
Tukiwa na reli ya kisasa + barabara za kisasa + bandari zenye nguvu, uchumi wetu unaweza kukua kwa kasi ambayo hatujawahi kuiona hapo kabla.
Napendekeza wataalamu mtakaosoma maoni haya pia msiache kutazama makala hii fupi ya namna Afrika Kusini ilivyopiga hatua za kimaendeleo kupitia uwekezaji mkubwa wa mabarabara hata kuzizidi baadhi ya nchi za Magharibi: Why South Africa's Highways Are So Good pia tazama: Top 10 Longest Roads in South Africa | The N2 Dominates
"Maoni hayapigwi rungu" - J.M. Kikwete