Uchaguzi 2020 Tanzania ya baada ya Uchaguzi: Taifa lililogawanyika

Uchaguzi 2020 Tanzania ya baada ya Uchaguzi: Taifa lililogawanyika

WHY SHOULD YOU HELP ONE MAN IN HIS EVIL ENDEAVOR, AT THE EXPENSE OF THE WHOLE NATION, ARE YOU THAT SHORT SIGHTED AND CHEAP?


Ni njaa na ubinafsi wa watu waliopo madarakani, isitoshe wanapalikia vibarua vyao kwa kutii maagizo haramu kutoka "JUU".

Hakuna uzalendo.

ONES HEART LIES ON WHERE HIS TREASURE IS.
 
Wasaliti na beti zao, hatuna nafasi ya mabeberu. Nchi imenyonywa sana. Tuna hitaji mbegu mpya ya upinzani
 
Ule mpango wa kubadili katiba ili apate muda kuendelea kuongoza unaelekea kwenda kutekelezwa. Japo alionyesha kutokuupenda
 
Teh teh teh teh. Mnatia huruma Sana, naona mnaanza kujipa maneno ya matumaini, teh teh teh!
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]Nikikumbuka ushabiki wa mleta mada kwa Membe napata tabu kweli..
 
Umegawanyika mwenyewe sisi Watanzania tumeungana na tuna ari ya MAENDELEO lakini pia tunavipongeza vyombo vya ulinzi na usalama kwa kazi nzuri na waendelee na kazi hiyo kuanzia kesho mpaka siku isiyo na kikomo.

Hongera Magufuli,Hongera Mwinyi,Hongera CCM
CCM KWA MAENDELEO YA TANZANIA
 
Umegawanyika mwenyewe sisi Watanzania tumeungana na tuna ari ya MAENDELEO lakini pia tunavipongeza vyombo vya ulinzi na usalama kwa kazi nzuri na waendelee na kazi hiyo kuanzia kesho mpaka siku isiyo na kikomo.

Hongera Magufuli,Hongera Mwinyi,Hongera CCM
CCM KWA MAENDELEO YA TANZANIA
Subiri hii kitu, utaleta mrejesho hapa tukiwa hai
 
Si unaelewa lakini hizi tabiri hazina maana yoyote!? Unatabiri tu halafu tunacomment ila ukienda ofisi za uma mzee yupo pale ukutani.
 
Ule mpango wa kubadili katiba ili apate muda kuendelea kuongoza unaelekea kwenda kutekelezwa. Japo alionyesha kutokuupenda
Alionyesha kutopenda kwa sababu ya afya yake siyo nzuri hata huu mhula wa pili kuumaliza lazima ana wasiwasi huenda akaishia njiani. Katika hali hiyo asingefanya aliyofanya katika Uchaguzi huu kulazimisha ushindi kwa mbinu chafu angeacha taratibu zichukue mkondo wake akishindwa arudi kijijini kwa heshima akangoje siku yake badala ya kuingoja imkute Ikulu. Akiweza kumaliza miaka 5 ya mhula huu kuna uwezekano mkubwa atabadili Katiba agombee mhula mwingine afie madarakani akitumia mbinu zilezile potelea mbali. Anapenda kuongoza angawa hana uwezo!
 
Hahaha limegawanyikia wapi?!

Mbona mnazusha, nchi hii igawanyike kumetokea nini kipya, tetemeko?!

Huyo alikuwepo, na atakuwepo milele, na nchi hii itaendelea kuwepo vile vile na haitagawanyika.
 
Alionyesha kutopenda kwa sababu ya afya yake siyo nzuri hata huu mhula wa pili kuumaliza lazima ana wasiwasi huenda akaishia njiani. Katika hali hiyo asingefanya aliyofanya katika Uchaguzi huu kulazimisha ushindi kwa mbinu chafu angeacha taratibu zichukue mkondo wake akishindwa arudi kijijini kwa heshima akangoje siku yake badala ya kuingoja imkute Ikulu. Akiweza kumaliza miaka 5 ya mhula huu kuna uwezekano mkubwa atabadili Katiba agombee mhula mwingine afie madarakani akitumia mbinu zilezile potelea mbali. Anapenda kuongoza angawa hana uwezo!

Jiwe mpango wa kusalia madarakani ni dhahiri alikuwa nao ila ni kweli hajiamini afya yake kama itamruhusu ndiyo maana anatone down hilo suala, lakini machinery nzima ya kumtengenezea njia ili atawale zaidi ya miaka kumi ameifungulia njia full force
 
Mnapiga ramli lkn hamna baya litakalo tokea.Ila kama unakumbukumbu nzuri mgawanyiko ulinzia hapa 2015👇👇👇
images (22).jpeg

2020 upinzani ukakosa maana.
 
Ukiwasoma humu waweza kufikiri Watanzania wote wanaipinga serikali iliyopo, mitaani ni tofauti kubwa mno na kizungumzwacho humu,

Watu wanaendelea na maisha kama kawaida, ukisema haya unaambiwa unaishi kwa shemeji yako!

Sijajua haya yanatoka wapi, sasa hivi kila mtu ni mtaalamu wa siasa, mtu wa takwimu, uchumi, sayansi ya jamii nk.
 
Hahahahahahah

Safari hii hamuendi Ccj kudai ushindi wenu kama 2015?
Foolish clever at your best! Unapewa uchambuzi ya yanayotarajiwa kutokea baadaye nchini kwako unaingiza uzwazwa! Uzuri ni kuwa mabaya yanayotarajiwa yatamgusa kila mmoja aliyemo ndani ya mipaka ya nchi na Hali hiyo haitambagua yeyote!
Na tangu lini ccj ikahusika na Mambo ya kisiasa? Au hujui ulisemalo? Ccj no mahakama ya kibiashara ya kimataifa!
 
Ukiwasoma humu waweza kufikiri Watanzania wote wanaipinga serikali iliyopo, mitaani ni tofauti kubwa mno na kizungumzwacho humu,

Watu wanaendelea na maisha kama kawaida, ukisema haya unaambiwa unaishi kwa shemeji yako!

Sijajua haya yanatoka wapi, sasa hivi kila mtu ni mtaalamu wa siasa, mtu wa takwimu, uchumi, sayansi ya jamii nk.
Huenda mtaa uliofanyia utafiti ni masaki peninsula na Ile ya Chamwino Ikulu! Ila ukiingia huku uswahilini watu wamenuna na Wana hasira Sana! Leo tu shabiki wa CCM kawaletea za kuleta wanazengo kijiwe Fulani kaambulia manundu ya kutosha! Amshukuru kijana wa bodaboda kamuokoa kwani wanazengo walitaka kumtia moto!
 
Uchaguzi umekwisha,na kwa nguvu za kidola tumerudishwa katika mfumo wa chama kimoja huku kukiwa na vyama vingi vya kuzugia na kudanganyia dunia.

Haya mambo si kwa faida ya Taifa zima, bali ni ego tu ya mtu mmoja na genge lake dogo la watu wanafiki wanaowaza matumbo yao badala ya Taifa zima na hivyo kujitoa ufahamu kwa kuangalia shibe yao ya leo badala ya mustakbali mpana wa Taifa la kesho!

Kutokana na yaliyotokea nchini, kuna mambo nayaona yanaweza kutokea nchini katika awamu hii ya pili ya utawala wa awamu ya tano

1. Kutakuwa na nguvu kubwa ya kuzima moto unaofukuta
Kama ulidhani biashara ya kununua watu waunge mkono juhudi imekwisha, tegemea hii inayokuja kuwa fungakazi, watu wenye ushawishi mkubwa watapewa option chukua mpunga ukae kimya au leta kidomodomo tukikate!. tegemea blackmails za kiwango cha Kimafia!. Sasa watu wana familia zao, wanaogopa hatma ya maisha yao, wapo ambao kwa hofu kubwa watanyamaza, wapo wachache ambao sauti zao zitaendelea kulia kutokea nyikani

2. Kutatokea kibinyo cha wahisani, na hivyo ili tuwe na unafuu tutajikuta tunajikurubisha zaidi kwa wachina
Wahisani wetu kwa miaka mingi ni nchi za Ulaya na Marekani, nchi za Nordic na Scandinavia wamekuwa ni wahisani wetu kwa miaka mingi tangu enzi za mwalimu, hawa wanaguswa na values za demokrasia na haki za binadamu huko wapelekapo misaada. Tegemea kuanza kuona wakipunguza misaada kwa sababu ya kilichotokea katika uchaguzi huu.

Marekani yenyewe inaona uchaguzi huu ulivyoendeshwa kama mpango mkakati wa Tanzania kufuata mfumo wa China wa chama kimoja huku kukiwepo vyama vya kuzugia (kwa wasiofahamu hata China vipo vyama vya kuzugia ila haviruhisiwi kushika dola!!), Kwa hiyo Marekani itatumia ushawishi wake ikiwemo Kupunguza misaada mbalimbali kama vile ya barabara, madawa na pia kuweka kibinyo kupitia mashirika ambayo ina ushawishi mkubwa kama World bank na IMF kuiweka Tanzania katika msitari inaotaka!. Tegemea kuanza kuona Tanzania ikisnza kulazimishwa kwa nguvu kubadili sheria ilizozitunga hivi karibuni ikiwa ni kstika mkakati wa kuminya upinzani wowote wa maana!

3. Kurudishwa kwa mchakato wa katiba mpya, lakini ile ya Chenge siyo ya Warioba
Kutatokea jitihada za serikali kutafuta legitimacy kwa umma, na kwa jumuia ya kimataifa. Wanajua, umma unataka katiba mpya, kwa hiyo kupoza hasira za umma baada ya uwendawazimu uliofanyika katika uchaguzi mkuu huu, wataurudisha mchakato wa katiba mpya pale ulipokuwa umefikia, yaani wataitisha kura ya maoni kupitisha rasimu ya Chenge. Na kwa kuwa katiba ya sasa ya mwaka 1977 inamzuia Magufuli kuendelea na uraisi baada ya mwaka 2025, hata hivyo katiba mpya ikipitishwa haimfungi mtu yeyote kuanza upya!. Kwa hiyo natabiri kuona Wapambe wa Jiwe wakipiga kampeni kali aendelee kwa hoja kuwa katiba hiyo mpya haimfungi mikono kuanza upya baada ya 2025

4. Kutakuwa na umasikini zaidi, hali ngumu ya maisha zaidi Ila kutakuwepo propaganda kali zaidi kuonyesha mambo yako shwari
Katika mazingira ya kisiasa ambayo bunge ni la chama kimoja na wabunge wana utiifu kwa Mwenyeiti tu mtu aliyewapa tonge kwa sababu kimsingi wao kama wao hawana uhalali mbele ya umma ambao haukuwachagua, Katika nchi ambayo wahisani wataacha kumwaga hela, nchi ambayo mifumo ya kisheria ipo compromised ili kuwa in favor ya regime(hata mahakimu na majaji nao wanaangalia bwana mkubwa angependa nini kwenye kuamua mashauri ya aina hii), usitegemee kuona wawekezaji wakileta mitaji kwa wingi, usitegemee kuona wafanyabiashara wakirisk kufungua biashara katika mazingira haya. Hali ya kiuchumi itakuwa ngumu na wimbi la ukosefu wa ajira litakuwa kubwa, na uchungu (bitterness) ya wananchi itakuwa kubwa zaidi na watajaribu kufanya reforms kadha wa kadha kutuliza hasira hiyo (angalia namba 5)

5. Kunaweza kutokea baadhi ya reforms za kutuliza hasira ya umma
Ili kutuliza watumishi wa umma wanaweza kuongezewa vijisenti viwili vitatu kwenye mishahara, Vitambulisho vya wamachinga vitarasimishwa, sasa vitakuwa na jina, picha, jinsia, anuani etc. Wakulima wanaweza kupewa uhuru kidogo wa kuuza mazao yao wanapotaka. Wanaweza kurejesha bunge live.

6. Umma kupoteza imani na dola na mifumo yake na kudharau chaguzi
Kutokana na jinsi uchaguzi huu ulivyofanywa, jinsi bunge lilivyobehave katika muhula wa kwanza wa awamu hii, na mahakama ilivyokuwa ikisimama na utawala katika mashauri yanayohusu demokrasia. Umma utapoteza imani na mambo ya chaguzi, umma kupoteza imani katika njia za kidemokrasia za kubadili serikali, hii ni hatari, kunaweza kutokea watu wakajaribu kuexploit dharau hii, Mwalimu alikutana na kadhia hii miaka ya 1980, na kwa experience ya tukio hilo na mengine yaliyotokea Afrika ni sababu mojawapo iliyomfanya baadae kutaka vyama vingi ili kuwepo na channel tofauti ya mawazo katika nchi (rejea aliposhauri kuwa tusingoje wanaotaka vyama vingi wawe wengi ndo tushtuke kuvileta, alisema hayo akitolea mfano wa rais wa Romania aliyeangushwa na wananchi kwa maandamano)

Kwa hiyo all in all, kuna njia ngumu iliyoko mbele yetu, siyo Wapinzani au CCM wote muda si mrefu tutaanza kuona consequences za uchaguzi huu. Yeyote anayeshangilia uwezo wa mtu kuwa mbunge, au diwani au cheo chochote bila ridhaa ya wananchi basi anashangilia yeye mwenyewe kupokwa nguvu na mamlaka ya kuweka madarakani serikali yake mwenyewe itakayomtumikia, Kiufupi anashangilia yeye kuwa mtumwa wa watawala badala ya yeye kuwa ndiye bosi wa watawala!. Mtawala hatokuogopa kwa sababu anajua kuwa wewe umeplay role ndogo sana ya yeye kuwa pale, mchango uliotuoa kwake ni Ujinga wako tu wa kuunga mkono magumashi yake

Na wale waliowezesha, kama ni wajumbe wa NEC, wakurugenzi, watu wa TISS, wa vyombo vya usalama laiti wangalijua ubaya wa waliyoyatenda kwa mama Tanzania kwa hakika wasingaliyafanya!. Wamelitendea Taifa kosa kubwa na dhulma kubwa ajabu ambalo naamini mpaka siku wanaingia katika makaburi yao kamwe Taifa halitowasamehe!. Wameangalia pafupi sana, badala ya mbele sana kwa mustakbali wa Taifa hili

WHY SHOULD YOU HELP ONE MAN IN HIS EVIL ENDEAVOR, AT THE EXPENSE OF THE WHOLE NATION, ARE YOU THAT SHORT SIGHTED AND CHEAP?

Naona hoja namba 5 wameanza nayo tayari kwa kurekebisha vitambulisho vya wamachinga kwa kupanga kuviewekea picha, na ahadi ya kuboresha maslahi ya watumishi
 
Back
Top Bottom