Tanzania ya mifupa mikavu inawadia

Tanzania ya mifupa mikavu inawadia

Ryan Holiday

JF-Expert Member
Joined
Jul 25, 2018
Posts
2,026
Reaction score
4,450
Peace be upon you

Ni miaka 61 imepita sasa, tangu Tanganyika kujipatia uhuru wake kutoka kwa mkoloni.

Nchi iliyobarikiwa bahari, madini, mito, maziwa, ardhi nzuri ya kilimo, maliasili, hali ya hewa safi na uoto mzuri wa kiasili wa kitropiko (Tropical type of vegetation).

Lakini bado mali tumeikalia tunaendelea kumsujudia mkoloni na kutembeza bakuli mithili ya omba omba asiyekuwa na baba wala mama.

Nchi nchi ipo ipo, Wananchi wapo wapo hatueleweki tunataka nini? Bidhaa bei juu, vyakula bei juu, umeme wa mgao, maji ya mgao, maliasili kiulizo? Migodini viulizo?

Hakika Tanzania ya mifupa inawadia, hatutakuwa na cha kujivunia bali mifupa tu, na mashimo ya migodi mithili ya maandaki.

20210422_130802.png


👉 Mifupa ya Dinosaur - iliyopatikana Tanzania eneo la Tendaguru kati ya mwaka 1909 na 1913.
👉 Which made it the most successful dinosaur excavation of all time.
👉 Mifupa hiyo ipo katika makumbusho ya "Berlin" nchini Ujerumani mpaka hivi sasa.

🤔 NOTE: Tanzania yangu ukiwanacho watakuja usipo kuwanacho huta waona tena. Wanakupenda kwa sababu wanajua una cha kuwapa.
 
Tanzania Ya mifupa minono ni ya mafisiem tu........mabaki wana waachia chadema na raia maskini.

Nchi ya ovyo sana hii.
 
Back
Top Bottom