Tanzania ya mitandaoni

Tanzania ya mitandaoni

Mshana Jr

Platinum Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
301,577
Reaction score
754,412
*1.Tanzania; Una mgonjwa mahututi ndani lakini unamuacha ili uwahi mazishi ya mtu aliekufa ambae hata sio ndugu yako!*

*2. Tanzania; Mgeni akija nyumbani anakula vyakula vizuri kuliko familia yako na anatumia vyombo vizuri kuliko familia yako.*

*3. Tanzania; Ukiugua Ukaomba michango utibiwe hakuna anaejitokeza, ila ukifa wanatoa mpaka offer za maji, chakula, usafiri na jeneza!*

4.Tanzania; Unamuomba mtu msaada wa sh 10,000 anakwambia sina ila anakwambia twende tukanywe bia anakununulia bia za 30,000.

*5. Tanzania; Watu wote mtaani wanajua mke wako au mme wako anachepuka lakini hakuna wa kukwambia, wanaogopa kusutwa!*

*6. Tanzania;Unavunjiwa nyumba usiku wezi wanaiba, hakuna jirani anaemuona mwizi, lakini usiku ingiza mchepuko, asubuhi wote wanajua!*

*7. Tanzania; Ukienda bar na mwanamke, wahudumu hawakuchangamkii na wanaweza hata kumpiga kikumbo usipokuwa makini.*

*8. Tanzania; Wenye vitambi wanaheshimiwa kuliko wasionavyo, ukienda kwenye harusi na kitambi hata kadi huulizwii, ngoja uende kibaumbau uone sura ya mtu wa getini!*

*9.Tanzania; Ukimkopesha mtu hela mnakuwa maadui, usipomkopesha mnaendelea kuwa marafiki.*

*10.Tanzania; watu wanafuatilia mambo ya wasanii na kujua mpaka siri za ndani, lakini muulize mtu, asili ya ukoo wao, akutajie babu wa babu yake anaitwa nani hajui!*

*11. Ukiwa na hela unaishi vizuri mtu anakuchukia tu bila sababu, na utaambiwa unaringa, unajisikia kumbe tu umepambana umetusua!*

*12. Tanzania; Mtu yuko kwenye magroup sita, la primary, secondary, chuo, kazini, manchester fans etc, kote huko kila siku mtu kafiwa uchangie, anaoa uchangie, anaolewa uchangie, anaumwa* *uchangie, ...wewe nani uwe na hela zote hizo?? Maisha yataacha kuwa Magumu?? Punguza* *network isiyo ya lazima!*
*Watanzania tubadilike.*[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
C&P
 
No. 02 hiyo inaitwa mgeni njoo mwenyeji apone bi mdashi alikuwa anavitenga kabisa vyombo vya wageni sasa ole wake mtu avitumie.

No. 12 yaani katika vitu ambavyo sijawahi kuviwaza wala kuvitamani kwa sasa ni kuwa kwenye hizo groups labda huko mbeleni sijui.
 
1) Ukiwa na vipesa kidogo automatically wanandugu wana haki ya kusaidiwa kila tatizo lao na pia kusifiwa roho mbaya.

2) Ukienda sehemu yoyote na gari kupewa heshima au hata kuzidishiwa bei katika huduma bila kujali kama gari umeazima au ya mkopo.

3) Ukimuita msichana hata kama unataka umuulize kitu, mawazo yanayomjia ni unataka kumtongoza.
 
Back
Top Bottom