Tanzania ya pili duniani kwa vivutio asilia vya utalii, tulikwama wapi?

Daaah
 
Umesema meeeengi lakini umeyasema kiushabiki zaidi. Hata Raisi angekaa huko ulaya mwaka mzima akitangaza utalii pasipo kurekebisha haya haitasaidia kitu.

1. Salama wa watalii. Unakumbuka watalii wamekuwa wakivamiwa na kunyang'anywa mali zao na hata kuuawa.

2. Huduma bora kwa watalii hili nao ni tatizo

Hizo ndiyo sababu za kwa nini watalii wanakuwa wachache kuzuru Tanzania. Kwani kwa usasa tuliyonao kila tulichonacho kinaonekana Katka mitandao ya kijamii.
 
Niwapi watalii wameuawa mkuu wangu,
 
Niwapi watalii wameuawa mkuu wangu,
Hifadhi ya SERENGETI watalii walishauawa mkuu. Katika hifadhi ya SERENGETI eneo la meatu mwaka 2018 ilitunguliwa helicopter na akauawa matlin. Pia miaka ya 2000 mwaka halisi siukumbuki hifadhi hiyo hiyo waliuawa wtalii na kunyang'anwa mali zao wakati wakienda hotel moja inaitwa SOPA lodge. Vile vile kumbuka watalii wengi wamevamiwa na kunyang'anwa mali zao katika fukwe za dsm na znz
 
Mtalii gani anatumia helkopta,

Ile kesi ya akina Njile na Dotto Mimi naijua vizuri wewe unapotosha sana,
 
Mwaka wa Mama,
 
Yule hakuwa mtalii mkuu, Nenda gereza la Bariadi kawaulize Wale vijana watakwambia kila kitu
 
Andiko hili
Asante kwa andiko hili, mwandishi
 
CM 1774858 hii ni akili kubwa mno,
 
Ni jambo jema kutangaza vivutio vyetu, ila tukumbuke umaskini ni kikwazo kwa vivutio vyetu. Ukaskini ni fedheha kwa ubinadamu. Watalii/wazungu wanakwreka na hali duni za maisha zinazowakumba wanaozunguka vivutio vyetu. Inakuwa kama wazungu wanakuja kuwakebehi maskini (kimsingi hwavutiwi na umaskini)

Pamoja na kutangaza vivutio, tuweke mikakati madhubuti ya kuondoa umaskini katika maeneo yetu ya vivutio vya utalii.
 
Haya ndiyo matatizo ya nchi yetu, kwa sasa tumegeukia Utalii kama njia ya kunyenyua uchumi wetu baada ya viwanda kushindikana.

Kila awamu na priority yake, hapa ndipo tunapokwamia - hatuna mwendelezo wa hizi awamu unaosimamiwa na sheria.
 
Tatizo Tanzania inakosa Demokrasia hivyo lazima Ufaransa watalii wawe wengi hata bila ya kuwa na twiga au simba kwa sababu kwao kila mtu ni muhimu tofauti na sisi matabaka matabaka,viongozi wengi kuwa wezi na kukanyagia haki za raia.
 
Je mna demokrasia au mna uccm ccm tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…