Tanzania ya sasa imekosa uzalendo! Mungu tusaidie

Joined
Sep 15, 2015
Posts
57
Reaction score
31
Nawasalimu kwa jina la muungano!
Katika vipindi vitatu vya uongozi ambao umekaribiana sana yaani kipindi cha JK,JPM na hiki cha mama yetu nimejifunza mengi kuhusu siasa na uzalendo. Nazungumzia hivi vipindi vitatu kwasababu enzi za kina nyerere na mwinyi huko nyuma uzalendo ulikuwepo na uchungu wa tanzania ulikuwa mioyoni. Hakika Tanzania ya sasa hatuna viongozi wa kisiasa wenye uzalendo na Taifa hili. Eeeh mungu tunusuru hili taifa ambalo uzalendo umepotea kabisa. Nasikitika kusema hata majeshi yetu hivi sasa yamekosa uzalendo japo weledi umeongezeka sana na ukiviangazia vitengo nyeti kabisa vya serikali vimekosa uzalendo. Viongozi, wanasiasa, Askari na usalama asilimia kubwa sasa hivi wapo katika vitengo hivyo kwasababu ya masilahi yao binafsi na familia zao.Inauma sana hata kuona watu wanakimbilia uaskari ili tu wapate ajira na ndani yao hakuna wito kabisa wa kazi hiyo na mwisho wa siku wanaharibu kabisa huko, wanasiasa ndiyo kabisaa wapo kimaslahi wazi wazi kabisa. Hakuna wa kuijali tena tanzania? Inauma sana unapoona viongozi walio juu yako hawana uzalendo na wao ndiyo wenye nafasi.Hakika inasikitisha hasa unamuona kabisa huyu analikosea taifa lakini yupo juu yako huna cha kufanya. Mwendazake alikuwa na uthubutu hakika japo alikuwa na mapungufu yake katika uongozi lakini alikuwa na uzalendo na uchungu na Tanzania yetu(alifanya kwa nafasi yake). Pia kizazi cha sasa hivi ukifanya mambo ya hovyo ndiyo kinashangilia yan kizazi cha oya oya nyingi(kisela) na kutaka mteremko kwa kila jambo japo wapo wazalendo ambao wapo tayari kufa kwaajili ya Tanzania na kutetea bendera yetu.

Tanzania yangu, nchi yangu sasa hivi watu hawajivunii tena kuwa watanzania, Hivi hii nchi inaelekea wapi? Ukienda maofisini hasa halmashauri yaani watu wapo kipesa zaidi na siyo kulitumikia taifa.
Sometimes huwa nawaza " ipo siku mtanikumbuka, nimeji-sacrifice maisha yangu kwaajili ya tanzania na watanzania". Hii kauli itakuja kuwa hukumu siku moja katika hiki kizazi. Haihukumu wenye madaraka/ viongozi lakini itawahukumu watu wa kawaida kabisa.uzalendo umepotea kabisa sasa hivi hasa kwa wanasiasa unafiki umekithiri kati yao wapo tayari kufanya chochote ili tu kupata maslahi yao binafsi. Naumia sana kuona kuna mambo ya kipuuzi yameanza kurudi kwa viongozi wetu yani naumia sana. Kwanini haya?
Ya mungu mengi! Eeeh mungu tunaomba Taifa lirudi kwenye mstari. Mama nakupongeza kutatua baadhi ya changamoto za mtangulizi wako lakini usikimbilie sana nje ukatusahau watanzania na Walio wengi anaofanya nao kazi siyo wazalendo watatuangusha.

Taifa langu,Tanzania yangu, nchi yangu Nakupenda.
Mungu ibariki Tanzania
 
Uzalendo utakusaidia nini mkuu, zaidi ya kukufukarisha tu. Kabla haujaamua kuwa Mzalendo kaiangalie familia ya Nyerere na wenzake wa aina yake.
Wanaokudanganya uwe mzalendo ni vile wanataka uendelee kuishi usingizini ili wao waendelee kuneemeka.
Uzalendo haukulipii kodi, wala haulipii mahitaji yako mengine. Wenzenu uzalendo walishaupiga teke kitambo, ila,ili msiwastukie wanashonesha tai na mashati yenye bendera za taifa ili waonekane Wazalendo, wengine wakachongesha vifimbo kama Nyerere, kumbe ni mambweha wakubwa wanapiga hela ya nchi kuliko Mkoloni.
Achana na habari hizo za uzalendo, wenzako wanauvaa kama nguo tu wewe unataka kuuweka akilini kama itikadi...utapotea.
 
Huyo Magu ndiyo hakuna kitu ni bora Kikwete 100%
1. Ameingia tu akafuta ajira za walimu na madaktari
2. Akahujumu uchaguzi. Sasa hivi uchaguzi umekuwa wa ovyo sana hakuna usawa. Wapinzani wamekuwa km maadui
3. Watu wasiojulikana walikuwa kila mahali. Watu wanatekwa, wanauwawa na kupigwa risasi mchana kweupe
4. Kesi za kubambikiana zilikuwa nyingi. Mfano Rugamalila
5. Alitengeneza viongozi wasiojua mipaka yao
Mfano Sambaya
Mkuu wa wilaya anafanya kazi za polisi, anaenda kukamata wezi n.k
Mkuu wa mkoa anaenda shuleni kuchapa viboko wanafunzi.
Kuna mgawanyo wa majukumu na mipaka. Kila idara ifanye kazi yake inavyopaswa. Makonda anaanza kufanya kazi za ustawi wa jamii, kupima tezi dume.
Angekuwepo jamaa, watu km Sambaya wangetengezwa wengi.
Bora jamaa, alijua mapema akaamua avute kamba fasta
 
Wazalendo wapo, usikose kupata darasa la uongozi pale unapopata nafasi🐒
20210925_212012.jpg
 
Uandishi Gani Huo Mkuu Hauna Mvuto Umekosa Hata Parandesi

Zamani Shule Mwalimu Angekuandikia Hivi "Andika Vizuri "
 
Kuishi maisha magumu na yasiyo na furaha sio uzalendo Bali Ni upunguani
 
Back
Top Bottom