watu kibao
JF-Expert Member
- Mar 25, 2025
- 466
- 1,663
Wanawake wengi sasa wana nafasi sawa kwenye elimu, ajira, siasa na fursa mbalimbali kama ilivyo kwa wanaume, Hakuna haja ya kuendeleza kampeni zilezile kwa wanawake.
Tunashangaa hadi leo kuona empowerment inaendelea kwa wanawake ambao tayari wameshajiweza.
Kwenye matangazo ya kazi imekuwa kawaida kuhamasiha wanawake kuomba kazi ila ni nadra sana kukuta wanahamasisha walemavu, na hata kwenye interview wakienda wanawekewa ugumu wa kupita kwa marks zile zile kama wanaojiweza bila kujali mazingira waliyopitia kwenye safari yao ya elimu, hakuna sheria inayoweka asilimia flani ya nafasi ziende kwao, hali hii imefanya iwe nadra sana kukuta walemavu maofisini.
Kwenye zawadi za matukio mbalimbali kuna kipengere maalum cha wanawake lakini walemavu wanapuuzwa,
Kwenye mabenki kuna account maalum za wanawake zenye riba ndogo lakini vipi kuhusu walemavu ?
Ni mambo mengi sana yanayotakiwa kufanywa kuwainua ndugu zetu hawa wanaopitia shida nyingi kuliko wanawake waliosaidiwa kujipata na sasa wana haki zao,