Wassalam wana-JF,
Mwezi Machi mwaka 2019, waziri Mkuu wa JMT Mh. Majaliwa Kassim Majaliwa alizindua kikubwa na inawezekana cha pekee Mkoani Lindi maeneo ya Mbalala jimboni Mtama kinachojulikana kwa jina la CASSAVA STARCH OF TANZANIA CORPORATION. Kiwanda ambacho kinajishughulisha na uzalishaji na uchakataji wa Mihogo.
Tangu huu mwaka umeanza mwekezaji huyo raia wa Ufaransa amekuwa na malalamiko mengi kuhusu kupanda kwa gharama za uendeshaji, huku akidai amewekeza Zaidi ya Bilioni 4 lakini hakuna hata shilingi mia mbovu ameipata kutokana na uwekezaji.
Kutokana na hali hiyo Zaidi ya wafanyakazi na vibarua MIA MBILI (200) wamefutwa kazi ndani ya wiki mbili hizi, na ametishia kufunga kiwanda na kuondoka zake kurudi UFARANSA au kwenda kuwekeza kwenye nchi nyingine.
Baadhi ya vitu ambavyo amefanya tofauti na kujenga kiwanda hicho ni pamoja na, kuajiri Zaidi ya wafanyakazi na vibarua 250 ambao walikuwa na uhakika wa kila wiki kupata posho kwa ajili ya familia zao (kimahesabu ni kuwa kama kila mfanyakazi mmoja ana wategemezi watatu hivyo Zaidi ya watu 750 walinufaika na shughuli za mwekezaji huyo), aliweza kuwekeza kulima Zaidi ya ekari 1000 za mihogo maeneo ya kijiji cha LIPOME, NAHUKAHUKA, NYANGAMARA na MBALALA yenyewe.
Pia aliwekeza kwenye mitambo kwa ajili ya shambani na pia watoa huduma mbalimbali walimtegemea kwa ajili ya kuendesha biashara zao mf Kampuni ya Usafiri kwa ajili ya wafanyakazi wake kuwapeleka na kuwarudisha shambani na wakati.
WITO WANGU KWA SERIKALI; Kupitia waziri wa Viwanda na Biashara kijana Innocent Bashungwa na Waziri mwenye dhamana ya KILIMO Japhet Hasunga ni wakati sasa kukaa pamoja na mwekezaji huyu na kuweka mambo sawa, licha tu ya kuwa wananchi wakazi wa maeneo ya Halmashauri walikuwa na matumaini kwa ajili ya kupata ajira lakini pia wakulima wadogo wadogo (out growers) walikuwa na matumaini makubwa ya kunufaika na Kiwanda hiki. Au mnaweza kumtumia Matthew De Klerk ambaye ndie General Manager wa CSTC Ltd.