Tanzania ya viwanda

Tanzania ya viwanda

SautiYaMnyonge

JF-Expert Member
Joined
May 13, 2018
Posts
439
Reaction score
742
Wazawa wameamua kurudi kuwekeza nyumbani!

Kiwanda cha Shafa Tanzania Investment ni kiwanda cha aina yake Afrika Mashariki na kipo Wilayani Mkuranga, Pwani. Katika ziara ya Waziri @AngellahKairuki imeelezwa kuwa kiwanda kinamilikiwa na wazawa.

Wazawa hawa ambao kwa muda mrefu wamekuwa wakiwekeza nje ya nchi, lakini kwa kutambua umuhimu wa kuendeleza nyumbani, wawekezaji hawa wameamua kuja nyumbani ili kuunga mkono matamanio ya Mhe. Rais @MagufuliJP yanayohimiza ujenzi wa viwanda ili kufikia uchumi wa kati.

Mradi umeanza mwaka 2018 na tayari asilimia 90 ya ujenzi imekamilika ikijumuisha kiwanda na ghala.

Kiwanda kitawekeza takribani shilingi bilioni 18 mpaka kukamilika na utazalisha vifaa vya ujenzi ikiwamo tofali 'concrete blocks', 'perving blocks' na 'carb stones'.

Vifaa vya ujenzi viavyozalishwa katika kiwanda hiki vitakuwa na ubora wa hali ya juu kutokana na matumizi ya tekinolojia hii kutoka Ujerumani ijulikanayo kama 'Massa'. Kwa kuzingatia hilo kiwanda cha Shafa kimejipanga kuzalisha kiasi kikubwa cha vifaa, kwa bei nafuu,kwa muda mfupi.

Vifaa vitakavyozalishwa vitafaa kutumika kwenye ujenzi wa barabara, viwanja vya ndege, bandari, majengo makubwa na majengo madogo. Hivyo wateja wakubwa na wadogo watanufaika na uwekezaji huu.

#T2020JPM
IMG_20200120_144822.jpeg
IMG_20200120_144838.jpeg
IMG_20200120_144909.jpeg
IMG_20200120_144804.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Let's be serious hapa mtaani kwetu kuna machaliii wanatengeneza hivyo vitofali hao jamaa wakasome kwanza kuufikia mziki wa hawa madogojanja
Sasa ulivyoremba etiiii oooh wazawa kutoka wapi sijui wamewekaza dolali zao na maneno kibao. Unless wawe na business nyingine Ila kama ni hiyo ni Bora wacheleweshwe kidogo kupewa usajili waje na mawazo concrete kama wale wanaotaka kutengeneza daraja linaloelea dar to zanzibar
Waje na mawazo mbadala
 
Back
Top Bottom