Naona mji wa Morogoro ktk kipindi cha miaka kumi kubadilika kwa kasi na kuwa jiji.Ukiangalia kwa haraka haraka tayari Moro ni kiunganishi kwa DSM, DOM, MBY na ikiwezakana barabara ya enzi hizo za ukoloni ikifufuliwa Korogwe,Handeni,Turiani....naona Moro haitashikika kwa maendeleo.Barabara na reli za uhakika ndio infastructure muhimu ktk kuleta maendeleo.Kwa wale waliowahi kuishi au kutembelea South Africa basi ni ushahidi tosha kwa nini tunahitaji infastructure za aina hii.kwa hili nampongenza JPM na team yake.