esther mashiker
JF-Expert Member
- May 29, 2018
- 616
- 552
THAMANI ya mauzo ya Tanzania katika Soko la Jumuiya ya Afrika Mashariki imeendelea kuongezeka mwaka hadi mwaka. Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Profesa Palamagamba Kabudi (pichani) alisema hayo jana wakati wa hotuba yake ya Mpango wa Makadirio ya Bajeti ya Wizara kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020.
Alisema katika kipindi cha mwaka 2018 mauzo yaliongezeka kukia Dola za Marekani milioni 448.5 kutoka Dola za Marekani milioni 312.5 mwaka 2017 sawa na ongezeko la asilimia 43.6 Waziri Kabudi alisema mauzo kwenda Kenya yalikuwa ni asilimia 47.7 wakati mauzo kwenda Uganda yalikuwa ni asilimia 23.4 ikifuatiwa na Rwanda asilimia 17.8 na kuwa bidhaa zilizouzwa kwa wingi ni pamoja na mahindi, karatasi, viuatilifu, saruji, marumaru, konyagi, ngano na mafuta ya kupaka.
Alisema thamani ya ununuzi wa bidhaa kutoka nchi wanachama wa jumuiya ilipanda kwa asilimia 27.7 kutoka Dola za Marekani milioni 237.0 mwaka 2017 hadi kukia Dola milioni 302.7 mwaka 2018 na kuongeza kuwa bidhaa zilizonunuliwa kutoka Kenya zilikuwa ni asilimia 81.75 wakati asilimia 17.40 zilinunuliwa kutoka Uganda.
Kwa mujibu wa Waziri Kabudi, soko kubwa la biashara za Tanzania katika Jumuiya ya Afrika Mashariki ni Kenya ikifuatiwa na Uganda na kuwa wizara imeratibu utekelezaji wa Himaya Moja ya Forodha ya Afrika Mashariki ambayo ni sehemu ya Umoja wa Forodha.
Alibainisha kuwa katika kipindi hiki, bidhaa zote zinazoagizwa kutoka nje ya nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki zimeingizwa katika mfumo wa Himaya ya Forodha na kuwa nchi wanachama zinaendelea kuingiza bidhaa zinazozalishwa ndani ya jumuiya katika mfumo huo ili kurahisisha uuzaji wa bidhaa hizo nje na ndani ya jumuiya.
Katika hatua nyingine, Waziri Kabudi alisema katika kipindi cha Julai hadi Desemba 2018 Tanzania imefanikiwa kutoa vyeti 5,953 vya uasili wa bidhaa za wafanyabiashara wa Tanzania wanaofanya biashara katika nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki. Alisema vyeti hivyo vimewasaidia wafanyabiashara hao kutotozwa ushuru wa forodha kama wanavyotozwa wafanyabiashara wengine ambao nchi zao si wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Alisema pia katika kipindi hicho, Tanzania imefanikiwa kutoa vibali vya kuingia nchini 167,469 kwa raia wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki na wanachama wa Tanzania 133,543 wamepata vibali vya kuingia katika nchi nyingine za jumuiya. Aliongeza kuwa wanafunzi 325 kutoka Tanzania wamepata vibali vya kuingia na kusoma katika nchi wanachama wa jumuiya na Tanzania imetoa vibali 142 kwa nchi nyingine wanachama wa jumuiya.
Waziri Kabudi aliongeza kuwa ndani ya muda huo watanzania 766 wamepata vibali vya kufanya kazi katika nchi nyingine wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki na kampuni mbili kutoka katika nchi za jumuiya zimefanikiwa kusajiliwa hapa nchini kwa lengo la kufanya biashara.
Alisema pia Tanzania imetoa vibali vya ukaazi 619 kwa raia wengine wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki na watanzania 120 wamepata vibali vya ukaazi katika nchi wanachama wa jumuiya.
Alitoa mwito kwa Watanzania kutumia na kuchangamkia fursa zitokanazo na Soko la Pamoja la Jumuiya ya Afrika Mashariki katika maeneo ambayo milango imefunguliwa kwani kwa kufanya hivyo kutaifanya nchi ya Tanzania kuendelea kunufaika ipasavyo na Mtangamano wa Afrika Mashariki. Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki imeomba iidhinishiwe Sh 166,926,820,000.00 kati ya fedha hizo Sh 162,926,820,195.00 ni kwa ajili ya matumizi ya kawaida na Sh 4,000,000,000.00 ni kwa ajili ya bajeti ya maendeleo.