Geza Ulole
JF-Expert Member
- Oct 31, 2009
- 65,136
- 91,917
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
UselessShida hamjielewi intelligence yenu hovyoo tu, huwa anasema amezaliwa nzega,lakini birth certificate serial number yake na hospitali alipozaliwa birth record number hazifanani!, yaani ata mimi naweza kuja kugombea kiti cha ubunge hapo bongo maana nakifaham kiswahili! Tukipiga stori na wasomali huwa wanacheka sana, wanakwambia shamba la bibi afrika yetu linajulikana tu. Anyway nisiseme mengi tukamletea shida mbunge 'wenu' mpendwa bashe, alipozaliwa tutawaambieni siku nyingine tu.
http://trade.ec.europa.eu/doclib/docs/2009/january/tradoc_142194.pdfEPA,MKATABA HUU UNASEMA NINI ?/
Wewe babu unazeeka vibaya, ikiwa wewe ni mchumi huko tanzania duu hata bibi yangu ni profesa sasa, mbona unatoa analysis ya uharo mtupu...ohh bomba, ooh uk, ooh eac ivunjike¿!!@suelsmail mimi kama mchumi ngoja nikueleze kwa lugha nyepesi, priorities zinabadilika esp. baada ya mwekezaji mkuu Tanzania the UK kujitoa ndani ya EU. Tukiruhusu huu mkataba uendelee ina maana tunawaminya wale waliowekeza kwa kuwaanika kwa unfair competition toka kwa wale ambao hawajawekeza. Pili sera ya awamu ya tano ni tofauti na zote zilizopita. It is that simple. Kenya wamesaini kwavile wanataka kuvunja jumuiya na kumbuka kukosa pipeline deal kumewaumiza sana. Na pia project ya bandari ya Bagamoyo inawanyima usingizi ila amini hawatafanikiwa.
Haswa kama Uganda watabaki na Tanzania hizi nchi mbili ndo zina strong say kwenye block kwa sasa. The EU can't afford to ignore them.
Nashukuru kwa ufafanuzi.@suelsmail mimi kama mchumi ngoja nikueleze kwa lugha nyepesi, priorities zinabadilika esp. baada ya mwekezaji mkuu Tanzania the UK kujitoa ndani ya EU. Tukiruhusu huu mkataba uendelee ina maana tunawaminya wale waliowekeza kwa kuwaanika kwa unfair competition toka kwa wale ambao hawajawekeza. Pili sera ya awamu ya tano ni tofauti na zote zilizopita. It is that simple. Kenya wamesaini kwavile wanataka kuvunja jumuiya na kumbuka kukosa pipeline deal kumewaumiza sana. Na pia project ya bandari ya Bagamoyo inawanyima usingizi ila amini hawatafanikiwa.
Haswa kama Uganda watabaki na Tanzania hizi nchi mbili ndo zina strong say kwenye block kwa sasa. The EU can't afford to ignore them.
Haibu ya ndugu ako akitetea interest za nchi nyingine wakati nyie rushwa inawamaliza. Njoo umchukuee awasaidiee tuna kina bashe wengi wengine wapo mansese.Duuuh watz bwana!, sasa mnanuabudu huyu msomali na baadhi familia ake ipo nairobi, kaka yake anamiliki petrol stations kadhaa in the city. Wengine ndugu zake kama zulekha bashe wapo hargeisa in somaliland!. Huwa mnachefua eti...
OyoooooOk boss, sasa iyo hospital yenye the birth record number ambayo haifananii na ya cheti, inaitwaje hiyo hospital au ipo nchi gani
Umesema kweli kwamba tumeongea nao kwa muda mrefu hadi kufika tulipo sasa, lakini sio kwamba wakati tunayaongea timu yetu haikuwa makini, walikuwa makini na walikuwa wanazuwa hoja za kupinga vipengele vya mkata ambavyo vilikuwa kandamizi. Kila tusema tuaambiwa usijali tutayatatua. Kuna wakati timu yetu ilikuwa nchi uholanzi, watu wetu kila wakiwafata timu ya Kenya kujadili vipengele kabla ya kukutana na wazungu, wakenya na wanajizungusha na kujifanya wako busy. Wenzetu wanaukabila lakini ikija swala la utaifa na kupiga dili, wanashikamana na ukabila unapotea. Mkapa alikuwa ana sema sana kuhusu huu mkataba, sehemu nyingi akipiga safari za ulaya anajaribu kuchomekea na kupinga. Ila kwasababu wenzetu wameweka maslai ya kupinga dili mbele, wanapata kigugumizi ikifika kupinga ukizingatia ni wazungu walio wekeza kwao ndio wanawasukuma kukubali mkataba huu.
Swala lingine ni vipengele vilivyo kwenye mkataba huu, vingi ni kandamizi, vitatuweka kifungoni kiuchumi mpaka hapo na sisi tutakapo fikia viwango kama vyao vya uzalishaji. Lakini wakati huo huo, mkataba huu aujaandikwa kutupa sisi wazawa uwezo wa kufikia vigenzo vyao, upo hapa kuwaruhusu wawekezaji (amabo ni wazungu wenzao) ili watumie ardhi yetu, rasilimali zetu, na masoko yetu kwa manufaa yakwao wenyewe. Kumbuka haya matatizo hapo hata kwenye utalii, watalii wanalipa holiday package huko huko ulaya, wakija hapa wanapokelewa na kampuni ya kigeni inayo tumia hela kiduchu kuwaweka hapa mpaka wanaondoka, walicho tumia hapa hao watalii ni kidogo sana ukilinganisha na walicho lipia kwao. Ndio maana JPM kaweka VAT ili tuwalime na huku pia, hiyo VAT imawauma kwasababu tunagema kile walicho kificha kwao ulaya.
Kuna kipengele kwenye mkataba kinacho tunyima sisi fursa kuuza bidha iliyowekwa thamani kwenye soko lao kwa kisingizio cha viwango vyetu ni duni. Lakini wao wanaruhusiwa kuleta bidha zilizo ongezewa thamani na kuuza kwetu. Tunalima zabibu hapa, tunachuma tunapeleka kwao wao wanturudishia ikiwa kwenye chupa kama wine. Kuna vipengele vya bei, wanataka tukiuza bidha zetu kwa nchi kama india, kwa dola moja, basi na wao tuwauzie kwa dola moja hata kama tunajuwa wanauwezo wa kunua kwa dola tano. Kwa wakenya hawana shida sana, maua hayana haja ya kuongezewa thamani, wanakata shambani, pakia kwenye mfuko, safirisha hadi ulaya, kahawa hivyo hivyo, chai hivyo hivyo. Lakini jiulize, mchina atakubali dili kama hiyo, au mmarekani? Umasikini wetu usiwe kigezo cha kujingiza kwenye mikataba iso na tija, rasilimali tunazo nyingi na hatujaanza kuzitumia, ukanda wote wa bahari ni rasilimali yenye mapana na marefu, kuanzia uvuvi, utalii, mafuta na gesi, usafirishaji, ujenzi wa meli za aina zote, ufugaji wa samaki uzalishaji wa magugu ya baharini mpaka usalishaji wa umeme unawezekana. Kilimo ndio kwanza tuajenga kiwanda cha matreka, huko nako fursa hazina mwisho. Maziwa makuu ni fursa, utali ni fursa kubwa na pana. Usafiri wa aina zote. Viwanda ndio usiseme, kwa kifupi mkataba huu kwa sasa utatunyima uwezo wa kujihinili kiuchumi na utatufanya tuendele kuwa tegemezi, Kenya hawana rasilimali nyingi na tukikubali huu mkataba wawekezaji wazungu na wazawa wa kenya watakimbikia huku kwetu kwa mwamvuli wa EAC na kusafirisha kila kitu ulaya. Unaweza kuuliza kwani kuna ubaya gani hapo kama tuna pata pesa. Ujuwe hali hiyo haita tusaidia katika kuinua vipaji na kumiliki uchumi wetu, kila siku tutakuwa tunanyeyekea watu wa nje wakati wa kwetu wanadumaa. Numba ya watanzania kinaongezeka kwa haraka sana tusipo watengenezea mazingira ya kumiliki uchumi wao na wao watazaliwa wakiwa watumwa kama sisi.