Tanzania yafunga vituo maalum vya Corona kwa kukosa wagonjwa wapya

Tanzania yafunga vituo maalum vya Corona kwa kukosa wagonjwa wapya

Mbolabilika

JF-Expert Member
Joined
Jul 30, 2019
Posts
2,128
Reaction score
2,867
Wizara ya Afya ya Tanzania imetangaza habari ya kufunga vituo 74 kati ya 85 vilivyokuwa vimetengwa makhsusi kwa ajili ya wagonjwa wa COVID-19 baada ya kukosa kupokea wagonjwa wapya, huku ikisisitiza kuwa janga la corona limepungua kwa kiasi kikubwa nchini humo.

Waziri wa Afya wa Tanzania, Ummy Mwalimu amesema hayo katika taarifa ya jana Ijumaa, baada ya kufunga kambi ya wagonjwa wa COVID-19 ya Lulanzi katika wilaya ya Kibaha mkoa wa Pwani.

Amesema, "mgonjwa wa mwisho wa corona katika kituo hiki cha Lulanzi aliruhusiwa kwenda nyumbani mnamo Mei 26 na tokeo wakati huo, kambi hii haijapokea mgonjwa mwingine."

Amesema nchi hiyo ya Afrika Mashariki imebaki na kambi 11 za wagonjwa wa COVID-19 ambazo pia zipo katika mchakato wa kufungwa kutokana na kupungua kwa kiasi kikubwa kesi za maambukizi ya ugonjwa huo hatari nchini humo. Amesema vituo hivyo kwa sasa vinatoa huduma nyinginezo za afya.

Hata hivyo Waziri wa Afya wa Tanzania amewaonya wananchi dhidi ya kupuuza kanuni na protokali za afya ili kuzuia kutokea wimbi jipya la maambukizi kama inavyoshuhudiwa katika nchi nyingine duniani.

Wizara ya Afya ya Tanzania ilitoa takwimu za corona mara ya mwisho mnamo Aprili 29 ambapo ilitangaza kuwa imethibitisha kesi 509 na vifo 21 vya corona.

Serikali ya Dar es Salaam ilitangaza kufunguliwa shule zote nchini humo mwishoni mwa mwezi uliopita wa Juni, mbali na kuruhusu nchini humo ndege za kimataifa na kufungua shughuli za kiuchumi na kijamii.
 
Walikuwa busy kueneza uwongo kuhusu Tz wakasahau kwao kuwa ni kubaya.
Halafu cha ajabu mpaka vyombo vyao nya habari vilikua vinaomba mabaya Kwa TZ lakin hamna hata chombo kimoja cha Tanzania kilichotangaza ubaya Kwa Kenya ,eti Watanzania wamekufa hamsini ndani ya wiki moja sasa imewageukia wao wenyewe hawatangazi mbona.
 
Halafu cha ajabu mpaka vyombo vyao nya habari vilikua vinaomba mabaya Kwa TZ lakin hamna hata chombo kimoja cha Tanzania kilichotangaza ubaya Kwa Kenya ,eti Watanzania wamekufa hamsini ndani ya wiki moja sasa imewageukia wao wenyewe hawatangazi mbona
Vyombo vyao vya habari wanapunguza wafanyakazi biashara imekuwa ngumu hawana habari za maana zaidi ya kuwasema watanzania
 
Mbolabilika,

Watu waliambiwa wakiugua wasiende hospitali bali wapige nyungu (wajifukize), sasa unategemea watu waendelee kwenda kwenye hivyo vituo wakati walisha katazwa?

Madaktari na wauguzi pia wanawakimbia wagonjwa, sasa unategemea mtu aende sehemu ambayo anakimbiwa?
 
Tz haina uwezo wa kupima chochoteee!! labda uja uzitoo tuuu😂😂
 
Lini wamepima watu tena?siasa za kipumbavu sana
Ngoja ukishapata dalili za Corona au ndugu yako wa karibu utajua wanapimaje na akilizako hizo za kubangaiza . Unataka wapime Kwa kupita mitaani utazani wanahesabu Sensa ndio ujue kama watu wanapimwa au ndio akili za kikenya kila cku Pima pima pima pima pima pima pima pima pima pima pima pima pima pima pima pima pima pima pima pima pimaaaaa bila ya faida yeyote
 
Ngoja ukishapata dalili za Corona au ndugu yako wa karibu utajua wanapimaje na akilizako hizo za kubangaiza . Unataka wapime Kwa kupita mitaani utazani wanahesabu Sensa ndio ujue kama watu wanapimwa au ndio akili za kikenya kila cku Pima pima pima pima pima pima pima pima pima pima pima pima pima pima pima pima pima pima pima pima pimaaaaa bila ya faida yeyote
Nitoleee upumbavu wako hapa
 
Watu waliambiwa wakiugua wasiende hospitali bali wapige nyungu (wajifukize), sasa unategemea watu waendelee kwenda kwenye hivyo vituo wakati walisha katazwa?

Madaktari na wauguzi pia wanawakimbia wagonjwa, sasa unategemea mtu aende sehemu ambayo anakimbiwa?
Mtaani kwenu yupo mtu anaeugua Corona au ndani kwenu?
 
Wewe ni nani nikupe hizo taarifa?
Au labda hauna kazi ya kufanya kama chadema mpaka leo wanadai lockdown wakati mabwana zao wanaachana nayo huku wakiwa na maambukizi laki 3 na uchafu.
 
Au kama upo Kenya sawa ila Kwa Tanzania nayoijua Mimi kuhusu kitu kinachoitwa korona sahau ila Kwa chadema korona ipo

Wakati mwingine ni vizuri tu kukaa kimya kuliko kuleta ushabiki wa kivyama kwenye mambo yanayogharimu maisha ya watu.

HIYO CORONA INA MAHUSIANO GANI NA VYAMA VYA SIASA? Je huo ugonjwa unachagua itikadi za ki vyama?
 
Au labda hauna kazi ya kufanya kama chadema mpaka leo wanadai lockdown wakati mabwana zao wanaachana nayo huku wakiwa na maambukizi laki 3 na uchafu

Hatuombi huu ugonjwa umpate mtu, hivyo kama haujampata ndugu yako, basi jua kuna wengine wamepoteza ndugu zao kwa ajili ya corona.
 
Back
Top Bottom