Tanzania yafuzu hatua ya Robo fainali, Kombe la dunia la Wanawake Chini ya Miaka 17

Bila bila

JF-Expert Member
Joined
Dec 20, 2016
Posts
22,168
Reaction score
39,118
Timu ya Taifa ya wanawake U17 Serengeti Girls imefanikiwa kufika hatua hiyo baada ya kutoka sare ya goli 1-1 dhidi ya Canada katika michuano inayoendelea Nchini India.

Matokeo hayo ya Kundi D yameiwezesha Tanzania kuwa na pointi 4 na kushika nafasi ya pili nyuma ya Japan iliyoongoza kundi kwa kuwa na pointi 9, huku Ufaransa na Canada zikiaga mashindano.

===========

Leo afe kipa afe beki ushindi au Sare inatupeleka Robo fainali.



=======
15’ Canada wanapata bao kupitia kwa Amanda Allen

36’ Tanzania wanasawazisha kupitia kwa Veronica Mapunda

70’ Tanzania 1 - Canada 1

85’ Tanzania 1 - Canada 1

88’ Tanzania 1 - Canada 1

Dakika 6 zimeongezwa

Mpira umekwisha, Tanzania (Serengeti Girls) imefuzu kucheza hatua ya Robo fainali dhidi ya Colombia.
 
Tunaupiga mwingi, tuko 1-1, hawa Canada walipata penati dakika ya 14 ila dakika ya 35 tukasawazisha.

Matokeo yakibaki hivi tunafuzu
 
Jinsi tunavyoshambuliwa wanaeza kupata bao Canada
 
Mabinti zetu U 17 wametoka draw 1-1 na Canada. Hivyo wametinga robo fainal. Kongole nyingi kwao[emoji120][emoji122][emoji122][emoji123][emoji91]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…