Tanzania yageuka kuwa kitovu cha kusambaza maambukizi ya COVID-19 ukanda wa maziwa makuu?

Tanzania yageuka kuwa kitovu cha kusambaza maambukizi ya COVID-19 ukanda wa maziwa makuu?

Sio siri tena kwa sasa Tanzania inatajwa vibaya sana duniani kuhusu mapambano dhidi ya COVID-19. Bahati mbaya hali hiyo imepelekea kuitaja Tanzania kama kitovu kipya cha kusambaza maambukizi ya COVID-19 (Covid-19 Epicentre) kwa ukanda wa maziwa makuu.

Hali hii inatokana na hatua ya nchi kadhaa zinazoizunguka Tanzania kueleza kupokea visa vipya vingi kutokea Tanzania na na wakati huo huo zikionyesha kutokukubaliana na namna taifa la Tanzania linavyokabiliana na hatari za kusambaa kwa Corona.

Mpaka sasa nchi za Kenya, Uganda, Rwanda na Zambia zimeweka takwimu rasmi zinazoonyesha visa vipya vilivyotokea huku vikiihusisha Tanzania moja kwa moja na zimeanza kuweka sheria ngumu zaidi kuzuia watu wanaotokea Tanzania kuingia nchini mwao.

Hatua hiyo pia imepelekea kwa Ubalozi wa Marekani nchini Tanzania siku ya jana kutoa tahadhari kuu kwa raia wa marekani waliopo Tanzania kubakia majumbani tu, kwa sababu hali ya maambukizi nchini Tanzania ni ya juu sana huku hospitali za jiji la Dar-es-salaam zikizidiwa na wagonjwa.

Wakati karibu kila nchi ikijaribu kutoa taarifa za mwenendo wa maambukizi ya COVID-19 wa kila siku hali ni tofauti kwa Tanzania ambapo kwa karibu wiki mbili sasa mamlaka za Tanzania zimekuwa kimya kabisa huku Rais wa Tanzania akitilia mashaka mwenendo mzima wa matokeo ya vipimo vya Corona nchini mwake na akihusisha jambo hilo huenda likawa ni njama za makusudi za mataifa ya makubwa kutaka kuichafua Tanzania kwa njia ya kukuza takwimu za maambukizi ya COVID-19. Mara baada ya kuzuka kwa shutuma hizo WHO ilikanusha vikali madai hayo na kusema vipimo vinavyotumiwa Tanzania kupima maambukizi ya COVID-19 ni vipimo sahihi, vinatumika dunia nzima na havina utata wowote katika kutoa majibu stahiki.
Wapiga dili wanahaha kuuza wananchi wao , mbona kenya huko tunaona joho anavyo haha kuwalazimisha wana mombasa kupima covid 19.
 
Huu ni uwongo wa mtandaoni

Tanzania ingekuwa imeathirika na corona tungeona misiba kili kona

Ila mtaani kwetu hakuna taarfa ya msiba wa corona toka hili gonjwa liingie Tanzania
Nusu mtu nusu Mbwa
 
Huu ni uwongo wa mtandaoni

Tanzania ingekuwa imeathirika na corona tungeona misiba kili kona

Ila mtaani kwetu hakuna taarfa ya msiba wa corona toka hili gonjwa liingie Tanzania
Misiba utaiona kwa kutumia chombo gani cha habari, hapa kijijini ulipo mnaangalia TBC peke yake.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mpuuzi kabisa wewe.Tanzania Ina maambukizi makubwa kuliko Marekani?
Marekani ipo eneo la maziwa makuu? au unaumwa Corona? hauna utofauti na Ng'ombe unakoswagwa ndipo unapoelekea.
 
Huu ni uwongo wa mtandaoni

Tanzania ingekuwa imeathirika na corona tungeona misiba kili kona

Ila mtaani kwetu hakuna taarfa ya msiba wa corona toka hili gonjwa liingie Tanzania
Mkuu kwa Mara ya kwanza katika umri wangu wa miaka 45 nilikuta maiti kando ya barabara pale kwenye U-turn ya baada ya korongwe ukitokea Kimara mtu alikuwa ameanguka na kufa pale siku ya jumatatu asubuhi wiki hii
 
Marekani ipo eneo la maziwa makuu? au unaumwa Corona? hauna utofauti na Ng'ombe unakoswagwa ndipo unapoelekea.
Umewahi kuona wapi ng'ombe anaefahamu kuandika mkuu, Okey sawa, mnajuana bhana, samahani
 
Huu ni uwongo wa mtandaoni

Tanzania ingekuwa imeathirika na corona tungeona misiba kili kona

Ila mtaani kwetu hakuna taarfa ya msiba wa corona toka hili gonjwa liingie Tanzania
Kama huamini kuwa kuna corona basi tena. Fungua ukurasa wa face book tafuta jina la mtu aitwae LOMNYAKI LETARA jana jioni alishuhudia ndugu yake akizikwa na watu.wa Halmashauri. Ni vidio mwanzo mwisho utaona kila kitu. Halafu urudi hapa kukanusha.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Umeanza leo kuona watu wameanguka barabarani ?
Hujui walevi kupindukia hufia barabarani pia ? Jiongeze acha kuishi kwa km Mtoto anayejufunza
Mkuu kwa Mara ya kwanza katika umri wangu wa miaka 45 nilikuta maiti kando ya barabara pale kwenye U-turn ya baada ya korongwe ukitokea Kimara mtu alikuwa ameanguka na kufa pale siku ya jumatatu asubuhi wiki hii
 
Kwa population yetu? Probably yes
Mkuu, sio kweli, ni siasa zetu tu za Kiafrica ili Baadhi ya Viongozi wa nchi zetu wajipendekeze Kwa mabwana wakubwa mkuu, China ndio kitovu cha kusambaza Corona duniani kote bhana
 
Umeanza leo kuona watu wameanguka barabarani ?
Hujui walevi kupindukia hufia barabarani pia ? Jiongeze acha kuishi kwa km Mtoto anayejufunza
Mkuu nimeshema kwa Mara ya kwanza katika umri wangu wa miaka 45 nimeliona maiti barabarani bila msaada wowote si wa police Wala raia.
 
Mkuu, sio kweli, ni siasa zetu tu za Kiafrica ili Baadhi ya Viongozi wa nchi zetu wajipendekeze Kwa mabwana wakubwa mkuu, China ndio kitovu cha kusambaza Corona duniani kote bhana
Mkuu kwa misongamano anayohimiza Magu,mpaka sasa tunaweza tukawa na maambukizi makubwa kuliko US .
 
Back
Top Bottom