Tanzania yageuka kuwa kitovu cha kusambaza maambukizi ya COVID-19 ukanda wa maziwa makuu?

Tanzania yageuka kuwa kitovu cha kusambaza maambukizi ya COVID-19 ukanda wa maziwa makuu?

Mkuu kwa misongamano anayohimiza Magu,mpaka sasa tunaweza tukawa na maambukizi makubwa kuliko US .
Duh! Ni hataree mkuu kuamini hiki! Kwa sababu gani! Mimi kama Mimi ndugu yangu, sijui labda Niko bize mno, mpaka leo hii huku kwetu sjawahi kusikia au kuona mtu mwenye Corona ingawa Naamini ipo, Na sjui Kwa sababu ya Imani yangu, Imani yangu huniambia, Hakuna tatizo kubwa linalomzidi Mungu, basi natembea nikiwa sina habari ya Corona ingawa tahadhari zote nachukua!!

Mimi kama mimi nimefikia mahali kuamini kwamba, Corona Tanzania ipo, Ila Mungu kaifubaza kulikoni kwenye mataifa mengine
 
Huu ni uwongo wa mtandaoni

Tanzania ingekuwa imeathirika na corona tungeona misiba kili kona

Ila mtaani kwetu hakuna taarfa ya msiba wa corona toka hili gonjwa liingie Tanzania
Haya kaka ... Nakupa wiki Mona nyingine hapa naongea nawewe tayari nimezika ndugu watatu ndani ya wikimoja ... Wakati huohuo naandika mssage hii naelekea mazishini nikiwa natokea mazikoni sjui umenielewa?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huu ni uwongo wa mtandaoni

Tanzania ingekuwa imeathirika na corona tungeona misiba kili kona

Ila mtaani kwetu hakuna taarfa ya msiba wa corona toka hili gonjwa liingie Tanzania
Sahihi halafu anayendika hivyo ni Mtanzania. Kweli kuna watu hawajitambui kabisa, hata kama ni kweli ni mpumbavu tu mwenye kuona fahari kutangaza habari hizo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huu ni uwongo wa mtandaoni

Tanzania ingekuwa imeathirika na corona tungeona misiba kili kona

Ila mtaani kwetu hakuna taarfa ya msiba wa corona toka hili gonjwa liingie Tanzania

Unaishi mitaa mingapi? Jumatatu asubuhi naenda kazini mtaa wa pili kutoka kwangu kulikuwa na msiba, mazingira yalikuwa na watu kama kumi wenye barakoa, polisi wanne na watu waliovalia suit za plastic wawili.

Kama huamini ninachokwambia naweza kutuma screenshot za meseji nilizowatumia nyumbani kuwatahadharisha juu ya msiba mtaa wa pili. Screenshot ikionesha muda na conversation, dare me!
 
Sio siri tena kwa sasa Tanzania inatajwa vibaya sana duniani kuhusu mapambano dhidi ya COVID-19. Bahati mbaya hali hiyo imepelekea kuitaja Tanzania kama kitovu kipya cha kusambaza maambukizi ya COVID-19 (Covid-19 Epicentre) kwa ukanda wa maziwa makuu.

Hali hii inatokana na hatua ya nchi kadhaa zinazoizunguka Tanzania kueleza kupokea visa vipya vingi kutokea Tanzania na na wakati huo huo zikionyesha kutokukubaliana na namna taifa la Tanzania linavyokabiliana na hatari za kusambaa kwa Corona.

Mpaka sasa nchi za Kenya, Uganda, Rwanda na Zambia zimeweka takwimu rasmi zinazoonyesha visa vipya vilivyotokea huku vikiihusisha Tanzania moja kwa moja na zimeanza kuweka sheria ngumu zaidi kuzuia watu wanaotokea Tanzania kuingia nchini mwao.

Hatua hiyo pia imepelekea kwa Ubalozi wa Marekani nchini Tanzania siku ya jana kutoa tahadhari kuu kwa raia wa marekani waliopo Tanzania kubakia majumbani tu, kwa sababu hali ya maambukizi nchini Tanzania ni ya juu sana huku hospitali za jiji la Dar-es-salaam zikizidiwa na wagonjwa.

Wakati karibu kila nchi ikijaribu kutoa taarifa za mwenendo wa maambukizi ya COVID-19 wa kila siku hali ni tofauti kwa Tanzania ambapo kwa karibu wiki mbili sasa mamlaka za Tanzania zimekuwa kimya kabisa huku Rais wa Tanzania akitilia mashaka mwenendo mzima wa matokeo ya vipimo vya Corona nchini mwake na akihusisha jambo hilo huenda likawa ni njama za makusudi za mataifa ya makubwa kutaka kuichafua Tanzania kwa njia ya kukuza takwimu za maambukizi ya COVID-19. Mara baada ya kuzuka kwa shutuma hizo WHO ilikanusha vikali madai hayo na kusema vipimo vinavyotumiwa Tanzania kupima maambukizi ya COVID-19 ni vipimo sahihi, vinatumika dunia nzima na havina utata wowote katika kutoa majibu stahiki.
Tuombe Mungu sana watz na tuchukue hatua madhubuti kwani hali sio nzuri na bado mambo yanaendelea kuwa mabaya. Pia tuendelee kufikiri vizuri kuhusu mustakabali wa uongozi wa nchi hii. Je tunataka ccm iendelee na mambo yake haya au tunataka mabadiliko?
 
Huu ni uwongo wa mtandaoni

Tanzania ingekuwa imeathirika na corona tungeona misiba kili kona

Ila mtaani kwetu hakuna taarfa ya msiba wa corona toka hili gonjwa liingie Tanzania
kwa maoni yangu, tz ni ya pili barani afrika nyuma tu ya afrika kusini kwa kuwa na idadi kubwa ya maambukizi & vifo vya korona

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wanao sema mambukizi ya corona Tanzania nimengi hawapo Tanzania wamejichimbia kwamabeberu sasa utawaaminije je kama niwazalendo kwanini wasirudi Tanzania kuna mpuuzi mmoja anajiita Mange kimambi huyumtu niwakupuuziwa anatupotosha kwanza kasaliti nchiyake

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huu ni uwongo wa mtandaoni

Tanzania ingekuwa imeathirika na corona tungeona misiba kili kona

Ila mtaani kwetu hakuna taarfa ya msiba wa corona toka hili gonjwa liingie Tanzania
Camarade: imethitika sasa kuwa watanzania wengi wakipimwa wataonekana kuwa wanamaambukizi because of vaccines they took in the past
 
Sawa mzee, ngoja tuone week ijayo kama kauli yako ni kweli au uongo wa mitandaoni
 
Back
Top Bottom