Tanzania Yaingiza Tani 52,000 ya Nyama ya Nguruwe (Kitimoto) Kutoka Nje

Kitimoto

JF-Expert Member
Joined
Aug 25, 2012
Posts
6,941
Reaction score
7,808
images - 2023-05-06T154405.078.jpeg

Chama cha Wafugaji Nguruwe Tanzania (TAFIPA) kimesema wastani wa tani 52,000 za nyama ya nguruwe huingizwa nchini kila mwaka kutoka nje ya nchi, huku Tanzania ikizalisha tani 27,000 pekee.

Katibu wa chama hicho, Collins Ritenga amesema leo Jumamosi Mei 6, 2023 kwenye mkutano ulioratibiwa na Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO) ukihusisha wafugaji na wafanyabishara wanyama hao kutoka Mikoa ya Mbeya, Iringa, Katavi na Rukwa.

Kikao hicho kimelenga kujadili na kuweka mikakati ya pamoja ya kuthibiti na kukabiliana na ugonjwa wa homa kali ya mafuta ya nguruwe ambao umekuwa ni changamoto katika mikoa ya Nyanda za Juu Kusini.

“Licha ya jitihada kubwa za wananchi kujihusisha na ufugaji wa nguruwe, bado kuna changamoto ya kutofikia malengo ya uzalishaji wa kibiashara kama mataifa mengine, ikiwepo ufugaji wa mazoea unaochangia kupata changamoto za ugonjwa wa homa ya mafuta ya nguruwe,” amesema.

Ameongeza kuwa ujio wa FAO huenda ukawa mwarobaini kwa wafugaji kuondokana na ufugaji wa mazoea ikiwepo changamoto za kukabiliana na ugonjwa hho ambao umekuwa ukiathiri sana sekta ndogo ya ufugaji nguruwe nchini.

Mwananchi
 
Kumbe kuna chama cha wafuga mbuzi katoliki hapa Nchini hahaha
 
View attachment 2612126

Waroho wa kitimoto wanali cost taifa
 
Wamefanya jambo jema kabisa. Kuliko wangeingiza mifugo ambayo ni red meat ambayo inasababishia watu matatizo ya miguu na viungo wameingiza nchini nyama Bora kabisa. Wote mnaalikwa kula
 
Hahaha sawa Mkuu walau bei ishuke kidogo Tuendelee kufaidi rost
Iringa tumefanikiwa kushusha Bei. Tatizo huko Darisalamu hii biashara imeshikwa na wachaga ndio maana Bei haishuki.
Ngoja tufanye mchakato wanyalukolo waianzishe huko Darisalamu utaona Bei ikifika angalau sh 7000 kwa kilo iliyo rostiwa na 6000 kavu.
 
Fanya importation kwa vitu vya maana hizo nguruwe tungeweza kufuga coz tuna maeneo mengi. Tunatengeneza unfavorable balance of Payment bila sababu.
Kwani mnazuiwa kufuga? Watu classic wanataka nyama ya maana ya nguruwe sio hizo za kienyeji mnazochoma hovyo na bila kufanyiwa parkaging nzuri..
Hakuna bidhaa ambayo tunajitosheleza kama Taifa na hii ni kutokana na vikwazo vingi vinazuia uwekezaji

View attachment 2612126

Chama cha Wafugaji Nguruwe Tanzania (TAFIPA) kimesema wastani wa tani 52,000 za nyama ya nguruwe huingizwa nchini kila mwaka kutoka nje ya nchi, huku Tanzania ikizalisha tani 27,000 pekee.

Katibu wa chama hicho, Collins Ritenga amesema leo Jumamosi Mei 6, 2023 kwenye mkutano ulioratibiwa na Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO) ukihusisha wafugaji na wafanyabishara wanyama hao kutoka Mikoa ya Mbeya, Iringa, Katavi na Rukwa.

Kikao hicho kimelenga kujadili na kuweka mikakati ya pamoja ya kuthibiti na kukabiliana na ugonjwa wa homa kali ya mafuta ya nguruwe ambao umekuwa ni changamoto katika mikoa ya Nyanda za Juu Kusini.

“Licha ya jitihada kubwa za wananchi kujihusisha na ufugaji wa nguruwe, bado kuna changamoto ya kutofikia malengo ya uzalishaji wa kibiashara kama mataifa mengine, ikiwepo ufugaji wa mazoea unaochangia kupata changamoto za ugonjwa wa homa ya mafuta ya nguruwe,” amesema.

Ameongeza kuwa ujio wa FAO huenda ukawa mwarobaini kwa wafugaji kuondokana na ufugaji wa mazoea ikiwepo changamoto za kukabiliana na ugonjwa hho ambao umekuwa ukiathiri sana sekta ndogo ya ufugaji nguruwe nchini.

Mwananchi
Huu ni upuuzi kama ule wa maziwa Lita bil.10
 
Back
Top Bottom