Tanzania yaipa Malawi Helkopta 2 na Dola milioni moja

Tanzania yaipa Malawi Helkopta 2 na Dola milioni moja

Hismastersvoice

JF-Expert Member
Joined
Jan 26, 2013
Posts
21,741
Reaction score
26,735
Balozi Polepole anazipokea helikopta mbili toka Tanzania kwenye uwanja wa ndege Chileka Blantyre Malawi, ndege hizi ni kwa ajili ya kutoa msaada wa uokoaji wananchi waliokumbwa na kimbunga Freddy, hizi zitafuatiwa na misaada ya chakula, madawa na mahema ambavyo vinaelekea huko kwa njia ya barabara.

Screenshot 2023-03-20 074224.png

Tani 60 za Chakula kuondoka Kila Siku Kuelekea Nchini Malawi. Serikali kupitia Jeshi la Wananchi wa Tanzania-JWTZ Limetoa Helikopta Mbili Kusaidia Shughuli za uokoaji.

Serikali ya Tanzania kwa kutambua ujirani mwema kati yake na Malawi, imetoa misaada mbalimbali ya kibinadamu kusaidia Nchi hiyo baada ya kukumbwa na Kimbunga Fredy ambapo Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) limepewa jukumu la kupeleka misaada hiyo.


====

Serikali ya Tanzania imetuma helikopta mbili nchini Malawi sambamba na kutoa dola milioni moja taslimu kwa ajili ya kusaidia walioathiriwa wa kimbunga Freddy.

Pia imetoa chakula tani 1,000, mablanketi 6,000 na mahema 50 kwaajili ya kusaidia wahanga nchini humo.


Msemaji wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Gaudentius Ilonda amesema, "Helikopta mbili zimeruka kutoka Dar es salaam kwenda Malawi kwaajili ya kusaidia katika shughuli mbalimbali za uokoaji katika maafa yanayoendelea.

"Pia serikali imetoa vifaa mbalimbali kama blanketi na mahema... sambamba na shehena za chakula zitapelekwa kila siku nchini Tanzania mpaka kufukia tani 1000," amesema.

Naye Balozi wa Tanzania nchini Malawi, Humphrey Polepole amethibitisha msaada huo kwa Malawi na kuongeza kuwa Serikali ya Tanzania itaendelea kusaidia nchi hiyo katika kipindi hichi kigumu.

"Katika kuhakikisha ndugu zetu wa Malawi wako salama na kuvuka kipindi hiki vizuri. Serikali ya Tanzania imetoa msaada ukiwemo wa fedha taslimu dola milioni moja, chakula, helikopta na vifaa vingine, " alisema Polepole.

Tanzania inapakana na Malawi na imekuwa na mwingiliano mkubwa wa watu kutoka kwenye mataifa yote mawili.

BBC Swahili
 
Mjamaa mhe. amenenepa ile sura kavu sasa imekua kama embe dodo ya Tabora, sikumtambua maana hata sauti sasa imejaajaa.
 
Duh ili nalo swali kweli?
Siyo swali gumu hata kidogo! Balozi Polepole ndiye mwakilishi wa nchi ya Tanzania nchini Malawi.

Hivyo, shehena ya msaada utakapo wasili Malawi inabidi Polepole atoe neno la kukabidhi hiyo shehena.

Baada ya hapo ataendelea na shughuli zake nyingine na zoezi hilo litaendelea kwa wakati wake.

Lakini Bwana Mnyika, Lema, Tundu Lissu, au Mbowe, hawatakabidhiwa shehena hiyo kusudi waiwakilishe Malawi.

Ila hilo linaweza kutokea baadae kama maridhiano yatazaa kitu kingine tusicho kijua kwa sasa.
 
Back
Top Bottom