n-propanol
JF-Expert Member
- Apr 7, 2019
- 5,349
- 7,000
Mpaka sasa vilimi vyao vimeshavimba midomoni hata sauti hawatoi tuwasubirie ndundu zikipungua watatema nyongo zao!Mama ameamua kulea inji zote za maziwa makuu na kati, chadema watachukia na hili huwezi amini
Ukitulia ukaamua kushirikisha akili vizuri utaelewa mantiki ya swali langu.Duh ili nalo swali kweli?
Ataweza vipi kukabidhi bila kupokea?si anaupokea Kisha anakabidhi,asipokee kwani alikua tanzania,si yupo kuleU
Ukitulia ukaamua kushirikisha akili vizuri utaelewa mantiki ya swali langu.
Yaani Tanzania itoe msaada kwenda Malawi alafu nchini Malawi msaada huo upokelewe na Balozi wa Tanzania nchini Malawi. Wewe unaona inaleta maana hiyo?
Huyu Balozi alitakiwa kupokea huu msaada au kuukabidhi?
Tangu mababu na mababu vinyamkera na vimbunga vinahusishwa na jini lenye mguu mmoja likifanana na binaadamu kwa maana mguu na juu kifua kipana na linatembea, kutembea huko ndiko kumefanya yapewe majina ya binaadamu.Mungu ibariki Tanzania.
Hivi vimbunga mara Fredy, mara Katarina nani huwa anavipa haya majina halafu almost vyote vina majina ya kibinadamu wakati vyenyewe sio binadamu 🤔
🤣Sijui bei yake ila najua hauzwi.
Hii sio hongo ili wasahau juu ya ziwa Nyasa? Maana ccm ni waabudu hongo tu!Serikali ya Tanzania imetuma helikopta mbili nchini Malawi sambamba na kutoa dola milioni moja taslimu kwa ajili ya kusaidia walioathiriwa wa kimbunga Freddy.
Pia imetoa chakula tani 1,000, mablanketi 6,000 na mahema 50 kwaajili ya kusaidia wahanga nchini humo.
Msemaji wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Gaudentius Ilonda amesema, "Helikopta mbili zimeruka kutoka Dar es salaam kwenda Malawi kwaajili ya kusaidia katika shughuli mbalimbali za uokoaji katika maafa yanayoendelea.
"Pia serikali imetoa vifaa mbalimbali kama blanketi na mahema... sambamba na shehena za chakula zitapelekwa kila siku nchini Tanzania mpaka kufukia tani 1000," amesema.
Naye Balozi wa Tanzania nchini Malawi, Humphrey Polepole amethibitisha msaada huo kwa Malawi na kuongeza kuwa Serikali ya Tanzania itaendelea kusaidia nchi hiyo katika kipindi hichi kigumu.
"Katika kuhakikisha ndugu zetu wa Malawi wako salama na kuvuka kipindi hiki vizuri. Serikali ya Tanzania imetoa msaada ukiwemo wa fedha taslimu dola milioni moja, chakula, helikopta na vifaa vingine, " alisema Polepole.
Tanzania inapakana na Malawi na imekuwa na mwingiliano mkubwa wa watu kutoka kwenye mataifa yote mawili.
Vipi opinion ya Sukuma gang? Kwamba pesa za tozo wanapewa Wamalawi wakati wanyonge wanateketea?Mama ameamua kulea inji zote za maziwa makuu na kati, chadema watachukia na hili huwezi amini
Hayo majina hata mbwa hupewa, they don't mean shit. Jina lolote kinaweza kupewa kitu chochote.Mungu ibariki Tanzania.
Hivi vimbunga mara Fredy, mara Katarina nani huwa anavipa haya majina halafu almost vyote vina majina ya kibinadamu wakati vyenyewe sio binadamu [emoji848]
Ulielewa lakini ndo mana ulijua namanisha nini?,Ila khasante mana umejitofautisha na mizoga mingine ya chadema hapa ingeanza na matusi.
Siyo swali gumu hata kidogo! Balozi Polepole ndiye mwakilishi wa nchi ya Tanzania nchini Malawi. Hivyo, shehena ya msaada utakapo wasili Malawi inabidi Polepole atoe neno la kukabidhi hiyo shehena. Baada ya hapo ataendelea na shughuli zake nyingine na zoezi hilo litaendelea kwa wakati wake.
Lakini Bwana Mnyika, Lema, Tundu Lissu, au Mbowe, hawatakabidhiwa shehena hiyo kusudi waiwakilishe Malawi. Ila hilo linaweza kutokea baadae kama maridhiano yatazaa kitu kingine tusicho kijua kwa sasa.
Mama ameamua kulea inji zote za maziwa makuu na kati, chadema watachukia na hili huwezi amini