Tanzania yaishukuru Benki ya EXIM ya korea kwa mchango wake katika maendeleo nchini

Tanzania yaishukuru Benki ya EXIM ya korea kwa mchango wake katika maendeleo nchini

Habari za Zanzibar

JF-Expert Member
Joined
Dec 18, 2024
Posts
651
Reaction score
433
TANZANIA YAISHUKURU BENKI YA EXIM YA KOREA KWA MCHANGO WAKE KATIKA MAENDELEO NCHINI

Serikali ya Tanzania imeishukuru Benki ya Exim ya Korea (KEXIM) kwa mchango wake mkubwa katika kuunga mkono agenda ya maendeleo ya taifa kupitia uwekezaji katika miradi ya miundombinu, maendeleo ya ujuzi, maboresho ya huduma za afya na mageuzi ya uchumi.

Shukrani hizo zimetolewa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Dkt. Mahmoud Thabit Kombo wakati wa mazungumzo na Rais wa Benki ya Exim ya Korea, Bw. Hwang Ki-Yeon ambapo pande hizo mbili zilijadili namna ya kuimarisha zaidi ushirikiano wa maendeleo kati ya Tanzania na Korea.

Wakati wa mazungumzo yao, Mhe. Waziri Kombo alisema kuwa ushirikiano wa Benki ya EXIM ya Korea na Tanzania umekuwa na mchango mkubwa katika kufanikisha utekelezaji wa miradi ya kimkakati inayochochea ukuaji wa uchumi na kuboresha maisha ya wananchi.

Kwa upande wake, Rais wa Benki ya EXIM ya Korea, Bw. Hwang Ki-Yeon alieleza dhamira ya benki hiyo kuendelea kushirikiana na Tanzania katika kutekeleza miradi yenye tija na kuunga mkono vipaumbele vya maendeleo vinavyolenga kukuza uchumi shindani na jumuishi.

Mazungumzo baina ya Mhe. Waziri Kombo na Bw. Hwang Ki-Yeon yamefanyika pembezoni mwa Mkutano wa Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Korea na Afrika unaoendelea jijini Seoul ambapo Mhe. Waziri Kombo anaongoza ujumbe wa Tanzania kushiriki Mkutano huo.
 

Attachments

  • IMG-20260601-WA0238.jpg
    IMG-20260601-WA0238.jpg
    122.7 KB · Views: 14
  • IMG-20260601-WA0234.jpg
    IMG-20260601-WA0234.jpg
    114.6 KB · Views: 18
  • IMG-20260601-WA0232.jpg
    IMG-20260601-WA0232.jpg
    78.4 KB · Views: 12
  • IMG-20260601-WA0228.jpg
    IMG-20260601-WA0228.jpg
    121.1 KB · Views: 13
  • IMG-20260601-WA0237.jpg
    IMG-20260601-WA0237.jpg
    139 KB · Views: 15
  • IMG-20260601-WA0236.jpg
    IMG-20260601-WA0236.jpg
    96.7 KB · Views: 16
  • IMG-20260601-WA0235.jpg
    IMG-20260601-WA0235.jpg
    99.6 KB · Views: 13
  • IMG-20260601-WA0231.jpg
    IMG-20260601-WA0231.jpg
    74.6 KB · Views: 11
  • IMG-20260601-WA0230.jpg
    IMG-20260601-WA0230.jpg
    109.3 KB · Views: 17
  • IMG-20260601-WA0233.jpg
    IMG-20260601-WA0233.jpg
    111.9 KB · Views: 13
  • IMG-20260601-WA0229.jpg
    IMG-20260601-WA0229.jpg
    117.1 KB · Views: 11
Back
Top Bottom