Tanzania yaitaka Jumuiya ya Kimataifa kuheshimu uhuru wa Tume

Mawele

Platinum Member
Joined
Jul 25, 2023
Posts
1,161
Reaction score
4,251
Screenshot 2026-03-04 at 15-42-22 Instagram.png

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imetoa majibu makali mbele ya Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa (UNHRC), ikiyashutumu mataifa ya Magharibi na asasi za kimataifa kwa kutoa kauli za upendeleo na "kuchagua matukio" kuhusu hali ya usalama nchini kufuatia uchaguzi wa Oktoba 2025.

Katika haki yake ya kujibu iliyotolewa Machi 2, 2026, Tanzania kupitia kwa Mwakilishi wake wa Kudumu katika Ofisi za Umoja wa Mataifa (UN) mjini Geneva, Dk. Abdallah Saleh Possi, amesema Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imetumia haki yake ya kujibu kauli zilizotolewa na wawakilishi wa Ubelgiji, Uingereza, Uswisi, Sweden, Ireland, Ubelgiji, Norway, Jumuiya ya Ulaya (EU), pamoja na mashirika ya Human Rights Watch na Amnesty International.

Tanzania imepinga vikali madai ya mauaji ya kinyume cha sheria yaliyotolewa na Uingereza, ikidai kuwa washirika hao wa kimataifa wamefumbia macho uharibifu mkubwa uliofanywa na vikundi vilivyohamasisha vurugu. Serikali imeeleza kuwa tarehe 29 Oktoba 2025, nchi ilishuhudia vitendo vya kigaidi vilivyolenga vituo vya polisi, ofisi za serikali, na miundombinu ya umma.

"Haya hayakuwa matukio yaliyojitokeza tu, bali yalikuwa yameandaliwa na kupangwa mapema ili kudhoofisha, kuharibu na kuvuruga utaratibu wa kikatiba. Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inapinga vikali madai yaliyomo katika kauli hizo zilizo wazi au wanazomaanisha; na kwa sababu ya maksudi wamefumbia macho mchakato na chanzo cha mambo yaliyopelekea matukio yaliyotokea", imeeleza taarifa hiyo.

Tanzania imesisitiza kuwa kama nchi huru, ina jukumu la kikatiba la kulinda utulivu wa umma na kwamba hatua zilizochukuliwa na vyombo vya usalama zilikuwa ndani ya wigo wa sheria ili kuzuia nchi isiingie kwenye ghasia.

Serikali imewataka washirika wa kimataifa kuheshimu uhuru wa nchi na kutozichukulia hatua za kulinda amani kama ukiukwaji wa haki za binadamu.

Kuhusu shinikizo la kufanya uchunguzi huru, serikali imekumbusha kuwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan alishateua Tume Huru ya Uchunguzi kisheria. Tume hiyo imepangiwa kuwasilisha matokeo ya uchunguzi wake tarehe 3 Aprili, 2026.

Serikali imesema matokeo hayo yatatumika
 
Uharibifu wa vitu, miundombinu na masanduku ya kura hatuwezi kuwa sawa na mauaji ya makusudi ya wananchi!
Serikali inapaswa kufahamu kuwa mara nyingi wanaharibu fedha ili kujaribu kuokoa maisha yao ama kusitiri vyema miili ya marehemu wao!

Hivi wanapofanya hivyo hawajui kuwa wanaharibu vitu ama kufuja mali Ili kujali utu wa binadamu?
Au na wao wahesabiwe gharama?
 
Unaweza ukawafanya wanainchi wako wajinga ingawa siyo wajinga kama unavyofikili ila ni manguvu yako tu kwa vyombo vya dola ambavyo havivuki mipaka ila huwezi kuwafanya viongozi wenzako wa inchi zilizoendelea wajinga
Hii ngoma inaenda kuwalamba watawala ambao sisi tunawaona wao kama hawana uwezo
 
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imetoa majibu makali mbele ya Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa (UNHRC), ikiyashutumu mataifa ya Magharibi na asasi za kimataifa kwa kutoa kauli za upendeleo na "kuchagua matukio" kuhusu hali ya usalama nchini kufuatia uchaguzi wa Oktoba 2025.

Katika haki yake ya kujibu iliyotolewa Machi 2, 2026, Tanzania kupitia kwa Mwakilishi wake wa Kudumu katika Ofisi za Umoja wa Mataifa (UN) mjini Geneva, Dk. Abdallah Saleh Possi, amesema Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imetumia haki yake ya kujibu kauli zilizotolewa na wawakilishi wa Ubelgiji, Uingereza, Uswisi, Sweden, Ireland, Ubelgiji, Norway, Jumuiya ya Ulaya (EU), pamoja na mashirika ya Human Rights Watch na Amnesty International.

Tanzania imepinga vikali madai ya mauaji ya kinyume cha sheria yaliyotolewa na Uingereza, ikidai kuwa washirika hao wa kimataifa wamefumbia macho uharibifu mkubwa uliofanywa na vikundi vilivyohamasisha vurugu. Serikali imeeleza kuwa tarehe 29 Oktoba 2025, nchi ilishuhudia vitendo vya kigaidi vilivyolenga vituo vya polisi, ofisi za serikali, na miundombinu ya umma.

"Haya hayakuwa matukio yaliyojitokeza tu, bali yalikuwa yameandaliwa na kupangwa mapema ili kudhoofisha, kuharibu na kuvuruga utaratibu wa kikatiba. Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inapinga vikali madai yaliyomo katika kauli hizo zilizo wazi au wanazomaanisha; na kwa sababu ya maksudi wamefumbia macho mchakato na chanzo cha mambo yaliyopelekea matukio yaliyotokea", imeeleza taarifa hiyo.

Tanzania imesisitiza kuwa kama nchi huru, ina jukumu la kikatiba la kulinda utulivu wa umma na kwamba hatua zilizochukuliwa na vyombo vya usalama zilikuwa ndani ya wigo wa sheria ili kuzuia nchi isiingie kwenye ghasia.

Serikali imewataka washirika wa kimataifa kuheshimu uhuru wa nchi na kutozichukulia hatua za kulinda amani kama ukiukwaji wa haki za binadamu.

Kuhusu shinikizo la kufanya uchunguzi huru, serikali imekumbusha kuwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan alishateua Tume Huru ya Uchunguzi kisheria. Tume hiyo imepangiwa kuwasilisha matokeo ya uchunguzi wake tarehe 3 Aprili, 2026.

Serikali imesema matokeo hayo yatatumika
Sons and daughters of bitches. Faki them all.
 
Yaani tume inakutana hadi na vibaka kama akina Sabaya na Yericko Nyerere hiyo ni tume au genge la vibaka?

Muundaji tume ndio muuaji namba moja halafu anaunda tume humo humo yumo mtu aliyekua kwenye chain ya kupokea maelekezo kuua watu.

Yaani wewe uibe halafu useme utaleta mashahidi wewe uliyekamatwa ili wathibitishe hukuiba?

Utter nonsense!
 
Abdallah Posi anataka watu wamseme vibaya tu wadakwe.
Poleni sana Watanganyika. Damu yenu inaonekana haina thamani yoyote
Huyu mjinga tukisema yeye awekwe juani bila kupaka sunscreen atajisikia vipi , maana hapo maumivu yake si zaidi ya watu waliopoteza maisha na ndugu waliishia kuona clip walizorecord wasamaria wema halafu maiti zikaenda kufukiwa katika kaburi la halaiki wasipate kuwazika ndugu zao kwa heshima.

Pengine akifanyiwa hivyo atapata walau kusikia maumivu.
 
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imetoa majibu makali mbele ya Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa (UNHRC), ikiyashutumu mataifa ya Magharibi na asasi za kimataifa kwa kutoa kauli za upendeleo na "kuchagua matukio" kuhusu hali ya usalama nchini kufuatia uchaguzi wa Oktoba 2025.

Katika haki yake ya kujibu iliyotolewa Machi 2, 2026, Tanzania kupitia kwa Mwakilishi wake wa Kudumu katika Ofisi za Umoja wa Mataifa (UN) mjini Geneva, Dk. Abdallah Saleh Possi, amesema Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imetumia haki yake ya kujibu kauli zilizotolewa na wawakilishi wa Ubelgiji, Uingereza, Uswisi, Sweden, Ireland, Ubelgiji, Norway, Jumuiya ya Ulaya (EU), pamoja na mashirika ya Human Rights Watch na Amnesty International.

Tanzania imepinga vikali madai ya mauaji ya kinyume cha sheria yaliyotolewa na Uingereza, ikidai kuwa washirika hao wa kimataifa wamefumbia macho uharibifu mkubwa uliofanywa na vikundi vilivyohamasisha vurugu. Serikali imeeleza kuwa tarehe 29 Oktoba 2025, nchi ilishuhudia vitendo vya kigaidi vilivyolenga vituo vya polisi, ofisi za serikali, na miundombinu ya umma.

"Haya hayakuwa matukio yaliyojitokeza tu, bali yalikuwa yameandaliwa na kupangwa mapema ili kudhoofisha, kuharibu na kuvuruga utaratibu wa kikatiba. Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inapinga vikali madai yaliyomo katika kauli hizo zilizo wazi au wanazomaanisha; na kwa sababu ya maksudi wamefumbia macho mchakato na chanzo cha mambo yaliyopelekea matukio yaliyotokea", imeeleza taarifa hiyo.

Tanzania imesisitiza kuwa kama nchi huru, ina jukumu la kikatiba la kulinda utulivu wa umma na kwamba hatua zilizochukuliwa na vyombo vya usalama zilikuwa ndani ya wigo wa sheria ili kuzuia nchi isiingie kwenye ghasia.

Serikali imewataka washirika wa kimataifa kuheshimu uhuru wa nchi na kutozichukulia hatua za kulinda amani kama ukiukwaji wa haki za binadamu.

Kuhusu shinikizo la kufanya uchunguzi huru, serikali imekumbusha kuwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan alishateua Tume Huru ya Uchunguzi kisheria. Tume hiyo imepangiwa kuwasilisha matokeo ya uchunguzi wake tarehe 3 Aprili, 2026.

Serikali imesema matokeo hayo yatatumika
Serikali italindaje utulivu wa umma kwa kuua watu na kuwazika kwenye makaburi ya pamoja na wengine kuwatupa bila ndugu zao kuwazika. Kama kweli serikali ingekuwa na nia nzuri ya kuwaua wahalifu ili kulinda usalama wa nchi, iweje ifiche miili ya waliouliwa. Huwezi ukajitetea kwamba niliua ili kudhibiti vurugu wakati uliowaua ulikuwa unawafukia kwa usiri ili ndugu zao wasiwaone. Huo ni ukikwaji mkubwa wa haki za binadamu.
 
Back
Top Bottom