Tanzania yajipanga kufanya sensa ya viwandani mwakani

Tanzania yajipanga kufanya sensa ya viwandani mwakani

Dalton elijah

JF-Expert Member
Joined
Jul 19, 2022
Posts
373
Reaction score
829
Serikali ya Tanzania imetangaza kufanya sensa ya uzalishaji viwandani kuanzia Machi hadi Juni 2025, ikiwa ni mara ya kwanza kwa sensa kama hiyo kufanyika kwa wakati mmoja Tanzania Bara na Zanzibar.

Sensa hiyo ambayo mara ya mwisho ilifanyika miaka 12 iliyopita, inalenga kukusanya takwimu katika maeneo manne muhimu: usambazaji wa maji safi, mifumo ya kukusanya taka, usimamizi wa taka na shughuli za matumizi ya marudio. Sekta nyingine zitakazoshughulikiwa ni pamoja na viwanda, madini na uchimbaji mawe, uzalishaji wa umeme na gesi, na huduma za udhibiti wa hali ya joto.


Waziri wa Viwanda na Biashara wa Tanzania Bw. Selemani Jafo amesema sensa hiyo itakusanya takwimu katika makundi makuu mawili, vinavyoajiri wafanyakazi 10, au zaidi na vile vyenye mfanyakazi mmoja hadi tisa.
 
Back
Top Bottom