Tanzania yajitoa rasmi katika mpango wa uendeshaji Serikali kwa Uwazi (OGP)

Tanzania yajitoa rasmi katika mpango wa uendeshaji Serikali kwa Uwazi (OGP)

Return Of Undertaker

JF-Expert Member
Joined
Jun 12, 2012
Posts
4,572
Reaction score
26,896
Tanzania imejitoa rasmi katika Mpango wa Uendeshaji wa Shughuli za Serikali kwa Uwazi (Open Government Partnership-OGP) hatua ambayo inazua wasiwasi kuhusu utekelezaji wa sera ya uwazi na uwajibikaji iliyoasisiwa na Rais mstaafu Jakaya Kikwete.

Hatua hiyo ya kujitoa kwa Tanzania imetangazwa na Kamati ya Uongozi ya mpango huo iliyokutana katika kikao cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa mjini New York, Marekani.

Hii ina maana kwamba kuanzia sasa mipango yote ya serikali itakuwa ikiendeshwa kwa usiri mkubwa (itafanyika gizani). Hakutakuwa na uwazi tena.

Moja ya athari za uamuzi huo ni nyaraka zinazohusu mambo nyeti ya nchi Mfano:- (matumizi ya pesa za Serikali, ugawaji wa ardhi) zitafichwa, na iwapo mwananchi atakutwa nazo atakuwa ametenda jinai na anaweza kushtakiwa (disclose of classified information), chini ya sheria ya usalama wa taifa ya mwaka 1971.

Bado haijaeleweka kwanini Tanzania imeamua kujitoa katika mpango huo na kuamua kuendesha mambo yake gizani, lakini, Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kiksnda, Dr.Aziz Mlima amesema “Ni kweli tumejiondoa. Lengo ni kuutathmini mpango huo kama unaendana na masilahi ya Taifa. Kama tutaona una maslahi kwa taifa tutajiunga tena”

Tanzania ilijiunga na mpango huo mwaka 2011 na kuwa nchi ya pili barani Afrika ikitanguliwa na Afrika Kusini. Kwa sasa nchi zaidi ya 40 za Afrika zimesaini mpango huo wa kuendesha mambo kwa uwazi. Pia zaidi ya 75% ya nchi zote duniani zinatekeleza mpango huo.

Mpango huo unasaidia kuondokana na kasumba ya kuendesha mambo kwa usiri kati ya serikali na wananchi.

Kusaini mpango huu kulimpa sifa Rais Kikwete kimataifa kwa kuunga mkono kuendesha mambo kwa uwazi. Bado haieleweki kwanini Rais JPM ameamua kujitoa katika mpango huo, na kuamua kurudi gizani.

Baadhi ya wachambuzi wa masuala ya kisiasa wanaeleza kuwa Tanzania kujitoa inaweza kuwa kwa sababu ya ushawishi wa Rwanda kwa kuwa Rwanda ni moja ya nchi ambazo hazijasaini mpango huo.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora, Angela Kairuki alipoulizwa kuhusiana na hatua hiyo amekataa kueleza lolote lakini akasema kuwa Serikali itatoa ufafanuzi itakapoona kuna umuhimu wa kufanya hivyo. “Nisikilize, sisi kama serikali tutalieleza hilo tutakapoona inafaa,” alisema Waziri Kairuki.

Nini maoni yako?
 
Maoni yetu ni kwamba Tanzania ni sovereignty state inayo haki hio na sio mkoloni au kibaraka
Sawa. Lakini kwa akili zako za kuzaliwa tu, unaona ni sawa kwa serikali kujiendesha kwa siri? Ondoa hiyo OGP, fikiria kama ni sawa kwa wewe kama mlipa kodi kutofahamu jinsi kodi yako inavyotumika.

Kwa upande mwingine umetoa an ironic statement. Kwa sababu sidhani kama Tanzania ni sovereign country if we take literal meaning of the word sovereignty. Ebu nenda pale BOT na Wizara ya Fedha uone wataalamu wanaotunga sera za kiuchumi. Vivyo hivyo wizara na idara nyingi za serikali zinatumia technical advisers/foreign experts hadi sasa. Bajeti ya serikali bado inategemea handouts za Waingereza, Wamarekani n.k.

Is that what you mean by a sovereign country?
 
Maoni yetu ni kwamba Tanzania ni sovereignty state inayo haki hio na sio mkoloni au kibaraka

Maoni yenu na nani? Serikali inatakiwa kuendeshwa kwa uwazi na uwajibikaji. Wananchi wanatakiwa kujua serikali yao inaendeshwa vipi kwasababu wao ndio walipa kodi.
Huu ni ukoloni wa mtu mweusi kujiendeshea serikali kama kundi la watumwa.
 
Swali ni wangapi watatusaidia kuwekeza kwenye projests zisizo na uwazi?
kwani extension ya mikataba ya madini ilikuwa wazi kwa wananchi?hizo kashfa za enzi za jk zilikuwa wazi?km zimewekwa wazi baaada ya hasara huo mpango hauna faida
 
Maoni yenu na nani? Serikali inatakiwa kuendeshwa kwa uwazi na uwajibikaji. Wananchi wanatakiwa kujua serikali yao inaendeshwa vipi kwasababu wao ndio walipa kodi.
Huu ni ukoloni wa mtu mweusi kujiendeshea serikali kama kundi la watumwa.
Mkuu unabishana na mtu ambae nusu ya ubongo wake umeliwa na wadudu..
Yupo kama hayupo kwenye ufahamu.
 
Hapa siri tu, kimbelembele chenu kitawaishia hapa hata tukienda Credit Suisie hakuna kujua sasa!
 
Hao wazungu unaowatetemekea kuna siku Marekani ilikuletea report yake namna inavyoendesha serikali yake?

Hivi hii mikataba ya hovyo ambayo Magufuli anapambana nayo saivi ilisainiwa tukiwa timeshasaini huo mkataba wa uwazi?
 
Back
Top Bottom