MK254
JF-Expert Member
- May 11, 2013
- 32,408
- 50,809
- Thread starter
-
- #21
Uko sahihi kuwa hakuna mwenye uhakika kuhusu uwepo au kukamatwa kwa hao majasusi kutoka Kenya. Tulichokisema ni kama kweli tukio limetokea, lazima polisi watakana kuwakamata na hata serikali yenu yaweza kukanusha kwenye media kuwa hawajakamatwa! Ila kama kuna masirahi binafsi, basi tz itatangaza kuwashikilia!
Kingine ni kuhusu Plausible deniability! Labda nikujulishe tu kuwa sio kila spy basi anafanya kazi ambayo akikamatwa atakanwa! Walio wengi hawafanyi kazi kwenye mazingira hayo! Mfano kwa CIA, kitengo pekee ambacho majasusi wake wana plausible deniability ni SAD (special activity division) na hawa ni wachache kweli kweli. Wengine wakikamatwa serikali zao huwa zinahaha kweli kweli.
By the way, suala la lagame kama nilivokwambia kuwa mimi na wewe tunaweza tusiwe na majibu maana lazima kuna makubaliano flani. Nimekupa mfano wa ushirikiano wa MOSSAD na CIA jinsi mossad walivyo wengi kule marekani na wanajulikana. Utaishia kusema tu kuwa wanasaidiana lakini kwa nyanja zipi huwezi kujua!
Ndo sawa na hili la kagame.
Ukisoma kwa makini ninachokiandika hutahangaika kueleza sana maana ni wazi hukukumbana na hii sentensi yangu "Japo kuna wale mambo hufanywa kimya kimya ya kubadilishana wafungwa."
Bila shaka sio wote hukanwa na serikali pande zote, hii michezo imekua ikichezwa tangu enzi zileee, hivyo hamna jipya.
Halafu umesababisha nicheke, sasa kipi hicho mnakifanya na mashushushu wa Kagame kiasi cha kulinganisha uhusiano wenu na ligi ya Mossad na CIA. Ukweli ni kwamba Kagame ametuhumiwa kuikojolea nchi yenu na uongozi wenu mara nyingi, mara eti ndiye alimumaliza Mtikila, mara amejaza machangudoa yakusanye taarifa kutoka kwa viongozi wenu wazinifu, mara amejaza watu wake kwenye JWTZ, mara katishia kumhit rais wenu...yaani tuhuma kibao halafu unajitetea kwa kusema mnashirikiana naye kama wafanyavyo CIA na Mossad...hehehehe