SoC02 Tanzania yangu, mazingira yangu

SoC02 Tanzania yangu, mazingira yangu

Stories of Change - 2022 Competition

JF FARMS

Member
Joined
Jul 23, 2021
Posts
13
Reaction score
17
Tanzania, Tanzania nchi nzuri na inayovutia kila upande ikiwa na watu wenye upendo, furaha na amani. Asubui ndege uimba kwa sauti mubashara, kaskazini wanyama na milima ya vutia, vilima na bahari vyenye ubaridi na upepo mwanana vya pendeza mbele za macho ya watu. Tanzania nchi yenye milima, bahari, maziwa, mbuga za wanyama pamoja na madini ya kila aina ila yenye watu waharibu mazingira ya vyanzo hivi vya utalii, vyanzo vya nishati na vyanzo vya uhai kwa viumbe hai.

Mwanadamu amekuwa chanzo cha uharibifu kila kukicha hapa duniani, sio mazingira, sio utamaduni wala sio miundo mbinu na afya. Mungu alimuumba Adamu na akamweka katika bustani ya Edeni ailime na kuitunza (Mwanzo 2:16). Je, Mimi na wewe atujapewa mazingira kuyalima na kuyatunza? Kwa kila mtanzania ajiulize hilo swali na atambue anawajibu gani kwenye jamii juu ya mazingira yanayomzunguka. Je, tumlaumu Raisi, waziri mkuu, wabunge au polisi kwa mazingira machafu au tujilaumu sisi wenyewe kwa kukosa hekima na busara ya kutunza mazingira yetu.

Majiji, miji, manispaa na mitaa yote inawatu ambao sio waelevu na wenye mapenzi ya dhati kwa taifa na mazingira. Unakuta mtu kapanda basi, daladala, pikipiki, gari binafsi au anatembea huku akila kitu na kutupa mabaki barabarani, unajihuliza huyu mtu anataka nani amwokotee hili baki alilotupa mtaroni au barabarani. Kwenye vyanzo vingi vya maji watu wanatupa matakataka, je maji unayokunywa, unayotumia nyumbani yanatoka mbinguni au!. Kwa kila mtanzania atafakari umuhimu gani alionao juu ya mazingira yanayotunzuka tusiwe wajinga wakushindwa na wanyapori wanaotunza mazingira yao vizuri.

Nitazungumzia njia tatu kubwa ambazo kama serikali, makampuni binafsi, mashirika binafsi na watanzania wanaweza kutumia kwa kipimo cha kati kuleta ufahamu juu ya utunzaji wa mazingira. Kila mtanzania atambue afya ndio maendeleo ya kila mtu bila afya njema binadamu hawezi kufanya kazi yoyote. Je, mazingira yako yakiwa machafu kwa watoto, kwa shughuli zako na kwa afya yako utaweza kusonga mbele kimaendeleo?. Zifuatazo ni njia ambazo zinaweza kutumika kwa kila mtanzania kutunza mazingira;

Sheria kali na Uwajibikaji wa Viongozi
Kwa kila shughuli au kitu chochote kifanyike kwa Mwanadamu vizuri kunahitaji sharia kuchukua mkondo. Ukisoma kwenye Biblia, Musa alipewa sheria kumi na Mungu kwa wanaisraeli ambazo zinatumika hadi leo katika maisha yetu. Nchi hii inahitaji sheria kali juu ya mazingira, mtu akikamatwa anatupa uchafu apewe faini au akatumike katika miundo mbinu ya serikali ama hospitali au yatengwe mashamba ya serikali wakalime huko. Mfano, tarehe 1/06/2019 sheria ya mifuko ya plastiki ilianza kutumika na kutekelezwa mara moja na uchafu wa mifuko ya plastiki ikatokomea kwa kiasi kikubwa pia mwaka huu (2022) mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Mheshimiwa. Amosi Makala alianzisha kampeni ya usafi wa jiji la Dar es Salaam na akafanikiwa kusafisha mji na kuwamasisha watu kuwa kutunza mazingira. Kila mkoa unatakiwa kuwa na viongozi wa kuigwa kama, Mheshimiwa. Makala.
dar1.JPG

Picha inaonyesha: Wakazi wa Dar es Salaam wakifanya usafi

Utumiaji wa Mapipa ( Dustbins)
Kila mmoja anatakiwa kutambua kuwa kuishi kwenye mazingira masafi yanalahisisha shughuli zote ziwe za uchumi, familia.. n.k. Ni vyema kuanzia ngazi ya familia kuwa na mapipa ya kukusanya taka zote ambazo zitapelekwa kwenye majalala ya miji na majiji. Kwa kila anayemiliki gari liwe la biashara au binafsi anatakiwa kuwa mstari wa mbele kwenye kulinda usafi na afya za abilia wake, kwahiyo kila gari linatakiwa kuwa na mapipa ya usafi ambayo yatatumika kuweka uchafu wa abilia. Kwa kila stendi ya daladala kunatakiwa kuwepo na mapipa makubwa yakukusanyia uchafu wa magari. Jambo hili sio jepesi kwa Tanzania na watanzania ila tukiweka nia kila mmoja kuanzia majumbani tutaweza kweli kuifadhi mazingira yetu.
dustbin.jpg
Mfano wa pipa ( Dustbin) ambalo linaweza kuwekwa kwa magari.

Elimu elekezi na somo la Mazingira
Hili sio swala la Raisi wa nchi,waziri mkuu au wenye vyeo ila ni wajibu wa kila mtanzania kutoa elimu na kupata elimu juu ya mazingira. Tumekuwa na sera nyingi juu ya mazingira mfano “ Panda mti, kati mti” hizi zote zimefanya kazi kubwa katika ulindaji wa mazingira ila bado ili changamoto linazidi kukua. Kwa kila mtu anayejitambua hawezi kuishi kwenye jalala, inatakiwa kila mtanzania awe Mwalimu kwa mwenzake juu ya umuhimu wa mazingira safi na salama. Pia somo la mazingira liongozwe mashuleni ili kuanzia ngazi ya msingi hadi vyuoni ili kuzidi kutoa elimu juu ya mazingira.

Hitimisho, Biblia inasema; Je! Watu wawili waweza kutembea pamoja, wasipokuwa wamepatana? ( Amos 3:3). Kweli wawili hawezi kutembea pamoja kama hawajapata. Kwa kila badiliko hapa nchini tunahitaji kutembea pamoja na kutunza mazingira kwa pamoja. Mazingira yakiwa masafi magonjwa yanapungua, uchumi unaongezeka maana watu watafanya kazi kwa ufasaha kwenye mazingira rafiki.

MUNGU IBARIKI TANZANIA, MUNGU IBARIKI AFRIKA
 
Upvote 6
Nchi yangu, Tanzania nakupenda sana ila tunza mazingira yako na watu wako.
 
Back
Top Bottom