Tanzania imetangaza azma ya kuwania nafasi ya uanachama usio wa kudumu katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kwa kipindi cha 2029–2030.
Akizungumza wakati akimwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, katika Mjadala wa Mkutano wa 81 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani Makamu wa Rais Deogratius Ndejembi amesema Tanzania ikichaguliwa itapeleka katika Baraza hilo sauti imara ya Afrika.
Amesema Tanzania itaweka kipaumbele katika diplomasia ya kuzuia migogoro kabla haijawa vita na utatuzi wa migogoro kwa njia za amani.
Ndejembi amesema Tanzania pia itasukuma mbele kuimarishwa kwa nafasi ya wanawake katika ulinzi na ujenzi wa amani pamoja na kuongeza ushiriki wa vijana katika ajenda za amani na usalama.
Amesema Tanzania itahimiza mageuzi ya operesheni za Umoja wa Mataifa za kulinda amani, ikiwa ni sehemu ya juhudi za kuimarisha amani na usalama duniani.
Tanzania imesema azma yake ya kuwania nafasi hiyo imepata uungwaji mkono wa Umoja
wa Afrika,