Tanzania yaorodheshwa kati ya mataifa 12 yenye league bora ya mpira wa miguu

Tanzania yaorodheshwa kati ya mataifa 12 yenye league bora ya mpira wa miguu

eden kimario

JF-Expert Member
Joined
Jun 13, 2015
Posts
10,356
Reaction score
16,379
Hatua hiyo inajiri baada ya taifa la Tanzania kuorodheshwa miongoni mwa mataifa 12 barani Afrika yenye ligi bora .
Hiyo inamaanisha kwamba klabu ya Yanga ambayo ilimaliza katika nafsi ya pili itajiunga na mabingwa wa ligi ya Tanzania Simba katika kushiriki ligi ya mabingwa.

Timu nyengine zitakazowakilisha Tanzania katika michuano hiyo ya Caf ni Azam Fc na KMC zitakazoshiriki katika kombe la Shirikisho.

Zitto Kabwe Ruyagwa
[emoji818]
@zittokabwe
Tunaposema @SimbaSCTanzania ni Timu ya Taifa tuna maana hii. Sasa Tanzania kuwa na Timu 4 makombe ya Bara la Afrika Kwa sababu ya mafanikio ya Simba kwenye ligi ya mabingwa Afrika. Sherehe za Uhuru Mwaka 2019 Simba ipewe Nishani ya Uhuru ya Uzalendo uliotukuka. Eid Mubarak

KMC itashiriki katika kombe la Shirikisho kwa mujibu wa kanuni hiyo ambayo inasema kuwa timu iliomaliza katika nafasi ya tatu ndio mabingwa wa kombe la FA , hivyobasi mshindi wa 4 atapata nafasi ya kucheza kombe la shirikisho kwa sababu bingwa wa FA ataiwakilisha nchi katika mashindano hayo.

Azam FC ni mabingwa wa kombe la FA

Rais wa TFF Wallace Karia amezitaka klabu zilizopata nafasi kusajili kwa umakini ili kujiandaa kwa mashindano ya CAF kwa lengo la kutopoteza nafasi ya kuingiza timu nne katika mashindano ya CAF.
Tayari CAF imefungua dirisha kwa mashirikisho kusajili timu zao.

Mohammed Dewji MO
[emoji818]
@moodewji
Tunajivunia kuwa sehemu ya kufanikisha nchi yetu kuingiza timu 4 kwenye michuano ya kimataifa, na tutaendelea kupambana kuhakikisha tunapata mafanikio makubwa kimataifa kwa maslahi ya klabu na nchi yetu. Hongera kwa Wanasimba wote kwa kazi kubwa tuliyofanya, tunastahili pongezi!

CAF imesema kuwa mwisho wa usajili wa timu hizo kushiriki ni mwezi Juni 30,2019

Baadhi ya mataifa ambayo yameorodheshwa kuwa na ligi bora Afrika ni pamoja na Algeria, Angola, DR Congo, Misri , Guinea, Morocco, Nigeria, Afrika Kusini,Sudan Tunisia na Zambia

League bora huangaliwa kwa jinsi vilabu kutoka nchi hizo, zilizofanya vizuri katika michuano ya club bingwa Africa kwa mwaka husika wa mashindano
mediekagere_officialaccount___ByF2fd-gC89___.jpg
 
Ni Heshima Kubwa kwa Simba bila shaka........Fundisho kubwa kwa mpira wetu. Ile zomea zomea kwa timu zetu zinapocheza na wageni na kushangilia timu za wageni sio jambo la zuri kwa mustakabari wa nchi.
 
Halafu kuna mijitu inapinga uwekezaji wa Mo simba
 
Halafu kuna mijitu inapinga uwekezaji wa Mo simba
Yule ni kama shabiki tu au mwanachama wa kawaida hana cheo chochote kwa sasa, ametoa maoni kama ambavyo shabiki mwingine anaweza kutoa.

Maaumuzi yote ya simba sc yanafanywa na bodi ya wakurugenzi wakiongozwa na mwenyekiti wao.

Yeye anakaa na kitu ambacho anaweza kunyang'anywa muda wowote kwa sababu yeye sio mmiliki wa simba kwa sasa au unaweza kusema sio mdhamini wa simba kwa sasa kwa sababu alishavuliwa na mkutano mkuu wa wanachama kipindi kile mambo ya uwekezaji yanapamba moto
 
Mbona alisema yeye simba ni kama mke wake

Pongezi TFF.
Pongezi Simba Sports Club.
Pongezi Taifa Star.
Kwasukwasu siku zote hawanaga Shukrani.
 
Yule ni kama shabiki tu au mwanachama wa kawaida hana cheo chochote kwa sasa, ametoa maoni kama ambavyo shabiki mwingine anaweza kutoa.

Maaumuzi yote ya simba sc yanafanywa na bodi ya wakurugenzi wakiongozwa na mwenyekiti wao.

Yeye anakaa na kitu ambacho anaweza kunyang'anywa muda wowote kwa sababu yeye sio mmiliki wa simba kwa sasa au unaweza kusema sio mdhamini wa simba kwa sasa kwa sababu alishavuliwa na mkutano mkuu wa wanachama kipindi kile mambo ya uwekezaji yanapamba moto
Pamoja kiongozi nimekuelewa
 
Simba sports club ndio team inayo nipa furaha
 
Back
Top Bottom