Tanzania yapanda viwango vya Udhibiti Rushwa Afrika, yawa ya 14 kutoka 19

Tanzania yapanda viwango vya Udhibiti Rushwa Afrika, yawa ya 14 kutoka 19

Jihudi za Kukabiliana na Rushwa za Serikali ya awamu ya 6 Zinazidi kuzaa matunda baada ya Tanzania kuzidi kufanya vizuri.

Kwa mujibu wa jaridi la Transparency International linaloangazia masuala ya Rushwa,Tanzania imeendelea kufanya vizuri katika kudhibiti Rushwa kutoka kuwa ya 19 mwaka 2021 Hadi kuwa ya 14 mwaka 2022.
===

Leo ni maadhimisho ya Siku ya Mapambano dhidi ya Rushwa Afrika ambayo yanafanyika mkoani Arusha yakiongozwa na Mheshimiwa Rais Samia.

Tanzania imeendelea kufanya vizuri kupambana na rushwa ambapo imepanda kwa nafasi tano Afrika kutoka 19 mwaka 2021 hadi 14 mwaka 2022.


My Take
Hongera Serikali Kwa uwazi na kujitahidi Kukabiliana na Wala Rushwa ingawa kazi Bado ni kubwa.
Kama kuna nchi ambazo kasi ya rushwa inapanda zaidi kuliko Tanzania lazima Tanzania itaonesha kuwa inafanya vizuri. Ni nani hasa anayejivunia rekodi hiyo ya Tanzania na ni kwa data zipi?
 
napata changamoto kuelewa n kuelea! lakini tutafanyaje ikiwa tumekubaliana kuwa mchawi mpe mtoto alee na tumekubali sasa kuufanyia kazi usemi huu katika kutimiza haki na matakwa ya hawa watanganyika kwa kufuta t kwenye uraia wao na sasa wamekubali tena bila vitisho kuitwa wadanganyika! Ifike wakati nikubaliane na kauli zote ngumu zilizotolewa na watu wote walio na busara na hekima kwa kadri ya mazingira yao
TANU yajenga nchi nawengine wakaja na Chukua Chako Mapema wakijaa ubinafsi wakijilimbikizia mali midomo yao ikitamka asali lakini vitendo vyao ni zaidi ya sumu huku wakienda kazi na wimbo wao ccm mbele kwa mbele! bila hofu na siku si nyingi wataanza kuuana kwa kudhurumiana.
 
Back
Top Bottom