Tanzania yapangwa Kundi L na Nigeria, AFCON 2027

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
5,383
Reaction score
18,776
Shirikisho la Soka Barani Afrika (CAF) limefanya droo rasmi ya upangaji wa makundi ya Kufuzu michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2027, ambapo Timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars, imepangwa katika Kundi L pamoja na timu za taifa za Nigeria, Madagascar na Guinea-Bissau.

1779196000857.png
Katika droo hiyo iliyofanyika Mei 19, 2026, timu mbalimbali zimepangwa katika makundi 12, kuanzia Kundi A hadi Kundi L, huku kila kundi likiwa na timu nne zitakazoshindana kwenye mashindano hayo makubwa ya soka barani Afrika.

1779196101472.png
Mashindano hayo yataandaliwa kwa pamoja na nchi za Kenya, Tanzania na Uganda, na yanatarajiwa kufanyika kuanzia Juni 19 hadi Julai 17, 2027.

Je, unaonaje nafasi ya Taifa Stars dhidi ya Nigeria na wababe hawa wa Kundi L? Watatoboa kweli?

Screenshot 2026-05-19 155029.png

Soma pia
 
Coefficient ya timu za Taifa ipoje? Uganda, Msumbiji na Zambia wapo juu yetu? Japo tulifuzu mtoano Afcon iliopita?
 
Hadi sasa serikali inaruka ruka tu, ilipaswa huu mwaka mzima wachezaji waanxe kuandaliwa kama timu B, baadaye wanaunganishwa na timu A kupata mjumuiko wa timu itayowakilisha nchi...

Tumekazana kuandaa viwanja tu wakati muamko utakuwa mkubwa endapo kama taifa tutafanya vizuri
 
Shirikisho la Soka Barani Afrika (CAF) limefanya droo rasmi ya upangaji wa makundi ya michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2027, ambapo Timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars, imepangwa katika Kundi L pamoja na timu za taifa za Nigeria, Madagascar na Guinea-Bissau.

Katika droo hiyo iliyofanyika Mei 19, 2026, timu mbalimbali zimepangwa katika makundi 12, kuanzia Kundi A hadi Kundi L, huku kila kundi likiwa na timu nne zitakazoshindana kwenye mashindano hayo makubwa ya soka barani Afrika.

Mashindano hayo yataandaliwa kwa pamoja na nchi za Kenya, Tanzania na Uganda, na yanatarajiwa kufanyika kuanzia Juni 19 hadi Julai 17, 2027.

Je, unaonaje nafasi ya Taifa Stars dhidi ya Nigeria na wababe hawa wa Kundi L? Watatoboa kweli?

Soma pia
kuna uwezekano wa mpaka 95% kombe hilo likabaki TZ
 
Hadi sasa serikali inaruka ruka tu, ilipaswa huu mwaka mzima wachezaji waanxe kuandaliwa kama timu B, baadaye wanaunganishwa na timu A kupata mjumuiko wa timu itayowakilisha nchi...

Tumekazana kuandaa viwanja tu wakati muamko utakuwa mkubwa endapo kama taifa tutafanya vizuri
Kichwa cha mwendawazimu kinafanyaje vizuri
 
Hadi sasa serikali inaruka ruka tu, ilipaswa huu mwaka mzima wachezaji waanxe kuandaliwa kama timu B, baadaye wanaunganishwa na timu A kupata mjumuiko wa timu itayowakilisha nchi...

Tumekazana kuandaa viwanja tu wakati muamko utakuwa mkubwa endapo kama taifa tutafanya vizuri
Si mmeletewa riofernand na drogba..
Na wamepandishwa Bentley na BASHITE
 
Mwenyeji hata akifungwa mechi zote,yeye alishafuzu tyr ,yani lazima ashiriki mashindano
Hapo atawahujumu wake ambao hawana nafasi hiyo kwenye kundi maana hawatakiwa siriaz sana
 
Back
Top Bottom