Tanzania yapata msaada wa Tsh. Trilioni 1.15 kutoka Ulaya

Tanzania yapata msaada wa Tsh. Trilioni 1.15 kutoka Ulaya

beth

JF-Expert Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
3,880
Reaction score
6,368
Kamisheni ya Umoja wa Ulaya (EC) imetoa Msaada wa Euro Miliono 425 (Tsh. Trilioni 1.15) kwa ajili ya kugharamia miradi mbalimbali ya Maendeleo

Fedha zilizotolewa zinatarajiwa kutumika katika miradi mbalimbali ya maendeleo kwa kipindi miaka mitatu ijayo na Serikali imeainisha kutumia Tsh. Bilioni 480 (Euro Milioni 180) kwenye miradi mitatu ikiwemo kuimarisha mifumo ya kidijitali

Aidha, Rais wa EC, Ursula von der Leyen amesema Tanzania ni miongoni mwa Nchi za Afrika zitakazonufaika na mpango mpya wa EU (Global Gateway Investment Package) unaokusudia kukabiliana na changamoto ikiwemo Ajira na kuimarisha Huduma za Afya na Elimu

9E0C97FB-61BF-460B-A6FD-4950F8F79B59.jpeg
 
Kamisheni ya Umoja wa Ulaya (EC) imetoa Msaada wa Euro Miliono 425 (Trilioni 1.15) kwa ajili ya kugharamia miradi mbalimbali ya Maendeleo

Fedha zilizotolewa zinatarajiwa kutumika katika miradi mbalimbali ya maendeleo kwa kipindi miaka mitatu ijayo na Serikali imeainisha kutumia Tsh. Bilioni 480 (Euro Milioni 180) kwenye miradi mitatu ikiwemo kuimarisha mifumo ya kidijitali

Aidha, Rais wa EC, Ursula von der Leyen amesema Tanzania ni miongoni mwa Nchi za Afrika zitakazonufaika na mpango mpya wa EU (Global Gateway Investment Package) unaokusudia kukabiliana na changamoto ikiwemo Ajira na kuimarisha Huduma za Afya na Elimu

View attachment 2123602
Ni msaada au mkopo?
 
AHADI YA MAMA

BAADA YA SERIKALI KAPATA MSAADA WA EURO MILIONI 425 SAWA NA TSH TRILIONI 1.15 KUTOKA KAMISHENI YA UMOJA WA ULAYA (E.C)

Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan ameahidi kuendelea kushirikiana na Kamisheni ya Umoja wa Ulaya (E.C) kuainisha maeneo mengine ya kipaumbele kupitia mashauriano ya pande zote mbili baadaye ili msaada huo ulete ustawi wa maendeleo kwa Watanzania.

#NyukiWaMama
#KaziIendelee
FB_IMG_1645263415648.jpg
 
  • Thanks
Reactions: MCN
Mataifa yote yaliyoendelea duniani, Siri yake kubwa Ni kuwa na Uongozi wa haki, unaojali haki ya watu wake. Tutakuwa tunakopa kila siku lakini bila kujua Siri hiyo hatutakaa tutokee tutabaki kutembeza bakuli na kujichekesha kwa Wazungu huku wao wakiendelea kufaidi rasilimali zetu.

Hongera Mama una nyota ya kukubalika kwenye mikopo.
 
kila mtanzania na apewe one million euro akawekeze anakokujua na bado zitabiki nyingine za maendeleo...bado siamini kama kweli million 425 zitakuja na kufanya malengo yaliyokusudiwa...ukichukua hizo million 425 na kugawa population yetu ya 60 million, hii ni sawa na kila mtu kupata mil 7...ni fedha ndefu hii kwa kweli.. tushindwe tu...
 
  • Thanks
Reactions: MCN
Fisadi hata apewe EURO bilioni moja hawezi kufua dafu katika maendeleo🐒🐒🐒
 
Ataendelea Kushirikiana (YEYE) au inabidi tuendelee Kushirikiana (SISI) na (WAO) na tufahamu tunashirikiana kwenye (NINI)

Haya mambo yanahohitaji collectiveness kufanywa Individually ndio yameleteleza Kila mtu akija anakuja na ya (KWAKE) na kuacha yaliyopita....
 
Mataifa yote yaliyoendelea duniani, Siri yake kubwa Ni kuwa na Uongozi wa haki, unaojali haki ya watu wake. Tutakuwa tunakopa kila siku lakini bila kujua Siri hiyo hatutakaa tutokee tutabaki kutembeza bakuli na kujichekesha kwa Wazungu huku wao wakiendelea kufaidi rasilimali zetu.

Hongera Mama una nyota ya kukubalika kwenye mikopo.
Unapokea msaada ukiwa umenuna, haikusaidii kwa namna yoyote ile. Tajiri hanuniwi na pia kumbuka kusema sisi ni matajiri wakati maisha yetu ya mtaani hayafanani na watu wanaotaka kujikomboa ni kazi bure.
 
Back
Top Bottom