Tanzania yapongezwa Mapambano Dhidi Ya Virusi Vya Corona

Tanzania yapongezwa Mapambano Dhidi Ya Virusi Vya Corona

mkiluvya

JF-Expert Member
Joined
May 23, 2019
Posts
815
Reaction score
733
1590729996502.png

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Prof. Pamalagamba John Kabudi (Mb) amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Ufaransa nchini, Mhe. Frederic Clavier ambapo pamoja na mambo mengine, Balozi Clavier ameipongeza Tanzania kwa hatua ilizochukua kupambana na janga a virusi vya corona nchini.

Balozi Clavier pia amemhakikishia Mhe. Waziri kuwa Ufaransa inaiunga mkono Tanzania kwa asilimia 100 kwa hatua ilizochukua kupambana na janga la virusi vya corona na kusema Ufaransa itaipatia Tanzania Euro milioni 30 ikiwa ni mkopo wenye masharti nafuu na riba ndogo kwa ajili ya kupambana na janga la virusi vya Corona pamoja na kusaidia kuinua uchumi.

Katika mazungumzo yao, Mhe. Waziri Kabudi amemuelezea Balozi wa Ufaransa jitihada zinazochukuliwa na Serikali ya Tanzania katika kupambana na Janga la Corona nchini na kumhakikishia utayari wa Tanzania katika kupambana na janga hilo na kuongeza kuwa Serikali ya Tanzania ilichukua hatua hizo kulingana na hali halisi ya maisha ya watanzania.

Prof. Kabudi amesema hatua zilizochukuliwa na Tanzania zililenga kuwafanya watanzania kuendelea na maisha yao bila ya kuathiriwa kiuchumi huku wakijilinda na kuchukua tahadhari ambazo zilikuwa zikitolewa na wataalamu wa afya nchini na duniani.

Balozi Clavier amemuambia Mhe. Waziri Kabudi kuwa Ufaransa pia imetoa msaada wa Dola 500,000 ambazo watapewa wakulima wadogowadogo 6,000 nchini kwa ajili ya kuboresha na kuimarisha kilimo chao na maghala ya kuhifadhia mazao yao. Ameongeza kuwa Rais wa Ufaransa ameziandikia nchi za G20 na Paris Club kuzishawishi kuahirisha ulipaji wa madeni na riba zake na pia kufuta kabisa madeni hayo ili kuimarisha uchumi ambao umeathiriwa na janga la corona katika nchi zinazoendelea.

Katika hatua nyingine Waziri Kabudi amekutana na kuagana na Balozi wa Uturuki nchini Mhe. Ali Davutaglu ambaye amemaliza muda wake wa utumishi na amemtakia maisha mema na kumwambia kuwa ni matarajio yake kuwa atakuwa Balozi wa hiari wa Tanzania nchini uturuki na kwingineko duniani.

Naye balozi Davotaglu ameishukuru Serikali ya Tanzania kwa ushirikiano ambao imekuwa ikimpatia alipokuwa akitekeleza majukumu yake nchini na kuahidi kuwa ushirikiano uliopo utaendelezwa hasa ikizingatiwa kuwa.
 
Kwani raia wa UK na USA wamerudi kwao kwa ajili ya Pasaka kama Wachaga?

Hajamwambia lini Ufaransa inawaondoa raia wako Tz Kwa ajili ya maandalizi ya x mass?
 
Tumejitosa kwenye mvua ya corona bila mwamvuli halafu tunasema hatulowi
 
Kabudi naona anabomu hela, hamna cha corono wala covid-19 hapo.
 
Hili ni jambo la kidoplomasia tu! Au kaulizwa jambo kimtego ili kujua maoni yake (kumbuka alerts za balozi za US na UK) na akaamua kuwa mwanadiplomasia. Hata mtu akila nyumbani kwako na ukamuuliza chakula kilikuwaje na akawa hakukipenda, busara inamtaka aseme kilikuwa kizuri.

Haiwezekani anasema kujifukiza ni njia ya kupambana na corona. Au kutopima na kutotoa takwimu.
 
Raia wa Marekani wamepuuza Propaganda za kitoto za Raia wao kukimbia kutoka sehemu yenye Maambukizi 400 kwenda kujitosa sehemu ambayo kuna Mamilion wameathirika na wanakufa kama Kuku wa Mdondo

Tunajivunia Rais Msomi Dr Magufuli
 
Back
Top Bottom