Tanzania Yasaidia Kuleta Muafaka Kenya

Tanzania Yasaidia Kuleta Muafaka Kenya

Mimi natoa shukrani sana kwa Annan hasa hasa maana JK na BM sijui kama wangalikuwa na la kusema mbele ya Wakenya .Waliona watanzania wakikimbilia shimoni Mombasa kukwepa mauji wakati CCM inapora madaraka .So BM hana la kuwaambia Wakenya hapa dume ni Annan.JK tangia gogoro limeanza hadi linaisha kaenda kwenye kuweka sahihi pekee .

Wote wanafaa kupongezwa, lakini ngoja nikukumbushe Mzee Roja Mila, alikuwa reserve mechi zake zilizompa sifa kuliko zote, watu wanacheza weeee akiingia yeye tu dakika za mwisho ananyuka bao sifa zote ni zake, lakini "ananyuka bao" ndio muhimu. Na hivyo ndio alivyofanya JK, watu wamecheza weeeeeee, kuingia yeye kanyuka bao.

Team nzima iliyofanya kazi Kenya inastahili sifa zote, pamoja na Kibaki na Raila wanapongezwa sana kufikia makubaliano na JK anapata golden shoes ya kuwa mfungaji bora.
 
Weka link ya gazeti la Kenya linalo sema ni JK ndiye kawezesha jambo hili kuisha tafadhali .

The agreement was the result of a five-hour meeting chaired by President Kikwete involving Mr Annan, President Kibaki and Raila Odinga. details

Jiulize aliyekuwa anasimamia mediation alikuwa Annan, iwe vipi hapa akawa JK ndiye mwenyekit...

Alafu pia Jiulize wakati mazungumzo yanaendelea ODM na PNU walikuja mara ngapi Dar es Salaam, kuwa makini kidogo, do not underate Tanzania on politics
 
Yaani JK kuitwa kwenye photo op baada ya watu kuchakalika kwa wiki kadhaa ndiyo "kafanya kweli"?

Juzi Waziri wa PNU alivyowatukana Annan na Mkapa mkutanoni JK alikuwa wapi?

Pleease, watu wamemuita JK kama rais wa nchi jirani na mwenyekiti wa AU aje kwenye photo ops,period .
 
Kuna pionti kubwa sana katika maandiko yako.
Odinga amekuwa akiyageuka makubaliano kila mara. Leo wakijadli hivi anakubali, ikija kwenye utekelezaji anakana kabisa kuhusika na makubaliano ya mwanzo. Annan ana kazi kubwa!
Tuvute subira kwanza kabla ya kuwapongeza kwa hatua hii.


Si kweli kwamba Odinga ndiye alikuwa akisumbua makubaliano.
Aliyekuwa akisumbua ni upande wa PNU kwani ikumbukwe kuwa PNU ilikuwa ikiwakilishwa na watu wawili ambao wanatoka vyama tofauti Martha Karua na Mtula Kilonzo wa ODM Kenya ya Kalonzo Msyoka, hawa watu wwili walikuwa na maslahi tofauti, na wakati wa kwenda ku brief viongozi wao upande wa PNU ulikuwa na wakati mgumu kwani Kibaki hayuko peke yake ni timu ya watu watatu, Mh. Mwai Kibaki, John Njoroge Michuki na Kalonzo, huyu mtu anaitwa Michuki ambaye kwa sasa ni waziri anayeshughulikia barabara huyu ndiye engine ya PNU na unapofanya Post Mortem wanakuwa na mawazo tofauti kwani wote wana sauti sawa ndani ya PNU na inasemwa PNU ni Michuki ndiye anayemwambia Kibaki afanye nini na aseme nini. ilihali timu ya Raila yenye Musalia Mudavadi, James Orengo, Dr Sally Kosgei na Mbunge wa Mvita Najib Balala hawa wote wana msimamo mmoja na wanamsikiliza Raila tu.
 
Yaani JK kuitwa kwenye photo op baada ya watu kuchakalika kwa wiki kadhaa ndiyo "kafanya kweli"?

Juzi Waziri wa PNU alivyowatukana Annan na Mkapa mkutanoni JK alikuwa wapi?

Pleease, watu wamemuita JK kama rais wa nchi jirani na mwenyekiti wa AU aje kwenye photo ops,period .

The agreement was the result of a five-hour meeting chaired by President Kikwete...

Link ipo hapo juu Mkuu.
 
Yaani JK kuitwa kwenye photo op baada ya watu kuchakalika kwa wiki kadhaa ndiyo "kafanya kweli"?

Juzi Waziri wa PNU alivyowatukana Annan na Mkapa mkutanoni JK alikuwa wapi?

Pleease, watu wamemuita JK kama rais wa nchi jirani na mwenyekiti wa AU aje kwenye photo ops,period .

My friend at least for this!!! you have missed a point!!! Ukiwauliza Wakenya, na hii utaona wataendelea kuamini Tanzania ndiyo iliyoleta amani,,, kumbuka msimamo wa Tanzania kutolalia upande wowote ndiyo ilifanya ipewe position hiyo... Remember PNU na ODM walituma ujumbe Bongo!!!

Lingine kama unaona Tanzania haikufanya kitu muulize Kaguta Museveni kama anajisikia je sasa hivi.

Mwisho kumbuka bila Tanzania hakuna kitu kinaitwa EAC.
 
somebody shoot me! Hongera JK kwa kufanya kweli Kenya, natumaini the same procedure itafuatwa Zanzibar pia au sio (kama kweli ni wewe umefanya hili).

sasa kama JK ameweza kufanya muafaka Kenya kwa muda mfupi kiasi hicho, anashindwa nini kufanya hivyo hivyo ili kupata muafaka visiwani? Hongera sana kwa kazi nzuri JK. Waliopoteza maisha yao, mwenyezi mungu awalaze mahali pema hopefully hakutakuwa na vurugu nyingine za kusababisha maafa zaidi.
 
Kilichobaki sasa ni wakenya kutupatia dada zao tuwafanye wake wa pili na watatu kama zawadi
 
Je swala la katiba mpya lini na vipi?

This agreement is not an end itself!

Swali safi sana,
hapo nd'o naseme Mzee Kibaka bado hajatia kete
zake mezani.We need to tread carefully mpaka katiba
mpya itiwe sahihi,ile tume ya Kura ivunjwe na swala
la kuajiri baraza la majaji pia liwekwe wazi.
The problem is that tunamjua Kibaki na
haaminiki.Haya WanaODM kaeni macho msije mkapigwa dole
tena!
 
sasa kama JK ameweza kufanya muafaka Kenya kwa muda mfupi kiasi hicho, anashindwa nini kufanya hivyo hivyo ili kupata muafaka visiwani? Hongera sana kwa kazi nzuri JK. Waliopoteza maisha yao, mwenyezi mungu awalaze mahali pema hopefully hakutakuwa na vurugu nyingine za kusababisha maafa zaidi.

Sitaki kuamini kwamba JK kafanya haya kwa muda mfupi vile hapana ila najua kaenda kushuhudia kuweka sahihi makubaliano .
 
Kilichobaki sasa ni wakenya kutupatia dada zao tuwafanye wake wa pili na watatu kama zawadi

Wewe kweli Brazameni!!!!
Watu hata bado hawajazikana wewe tayari unawaalika
dada zao kuwafanya wake.A'fu ndo iweje?
 
Kibaki na timu yake walikabwa koo walipoambiwa bila soni: "Power sharing must be real, not an illusion."

Kuendelea kujigalagaza kwa siku hizi mbili za mwisho na kutukana, kote kulikuwa ni kukosa njia ya kupumulia. Annan alikwishayaona haya, na kujua ni tapatapa za mwisho katika kufikia makubaliano!

Wakubwa, Marekani, Ulaya walishahitimisha Kibaki hakuwa na njia ya kutorokea. Bila sauti za hawa wakubwa, na hasa kwa nchi kama Kenya tusijigambe bure kuwa ni sisi ndio tumeleta upatanishi.

Ni furaha kuona viongozi wetu Kikwete na Mkapa kuwemo, na kutoa mchango wa aina katika makubaliano hayo, lakini si busara kuanza kujigamba kuwa ni sisi ndio sababu ya makubaliano yale.
 
The agreement was the result of a five-hour meeting chaired by President Kikwete...

Link ipo hapo juu Mkuu.

Kwa hiyo kazi yote ya wiki kadhaa haikuwa na maana, kaja Superman Kikwete katika kikao cha masaa matano kaweza kufanya Annan na Mkapa walichoshindwa kufanya tangu January 10 siyo?

Woow, kwa nini asitumie magic touch yake Zanzibar basi?
 
sasa kama JK ameweza kufanya muafaka Kenya kwa muda mfupi kiasi hicho, anashindwa nini kufanya hivyo hivyo ili kupata muafaka visiwani? Hongera sana kwa kazi nzuri JK. Waliopoteza maisha yao, mwenyezi mungu awalaze mahali pema hopefully hakutakuwa na vurugu nyingine za kusababisha maafa zaidi.

Labda ni muhimu kufahamu political mediation and conflict resolution is not an event rather is a process which needs resources and time. Kama kuna wa kusifiwa ni wale walioweka vitu hivyo viwili nilivyotaja. Actors wengine ambao mchango wao tunaweza kuuthamini kidogo ni AU kupitia mwenyekiti wake kwa kwenda Kenya na kuhitimisha mazungumzo. Sifa kuu lazima iende kwa EU kwa kutishia kukata misaada na US government kwa kuiongezea uzito kamati ya Annan kwa kutishia kuwaadhibu wale waliokuwa wakikwaza mazungumzo.

Siamini kama kuna Magic solution au significant contribution ambazo JK ametia. Kwani katika mgogoro huo, US wana maslahi ya moja kwa moja na amani ya Kenya, awe Odinga au Kibaki rais wao wanachotaka ni amani na stability in Kenya kwani bila Kenya maslahi ya US Sudan ya kusini na Pembe ya Afrika yako hatarini. Kwa hiyo yeyote aliyekuwa hataki suluhu alikuwa anahatarisha maslahi ya Bw. Mkubwa.

Kama JK ana magic solution ya kusuluhisha mgogoro kwa siku moja, mbona wa kwake kule visiwani una miaka miwili? aende Zimbabwe akasuluhishe.
 
..Lakini huyu ndugu kibaki hakushinda uchaguzi, sasa inakuwaje tena apewe nafasi katika mgawanyo wa madaraka??? Nini maana ya uchaguzi??? Huu mgawanyo wa madaraka utawapa jeuri viongozi ving'ang'anizi afrika kuendelea kung'ang'ania madaraka kinyume na matakwa ya wapiga kura.

Ni kweli watu wamepoteza maisha. Ni kweli watu wamepoteza mali zao, wapendwa wao nk. Lakini hii haitoi justification ya power sharing. Huyu kibaki alipaswa kufunguliwa mashtaka katika mahakama za kimataifa. Ndiyo. Ushahidi upo kwamba huyu jamaa hakushinda uchaguzi. Sasa inakuwaje leo hii anashirikishwa katika kushea madaraka. Haya ni matusi kwa watu wa kenya. Ni lesson gani nchi nyingine za africa zijifunze kutoka kenya???

Halafu la kushangaza zaidi eti Mkapa naye ni mmoja kati ya ma TX katika hiyo tume. Huku nyumbani tuhuma zinamsakama kila kukicha. Mnategemea nini hapo wakuu???

Inaonekana huu utamaduni wa magharibi hatuuwezi. Umetushinda. Tubuni utaratibu mwingine wa utawala. Shame on us Africans.

Cha kujifunza hapa ni-Ukiona umeshindwa uchaguzi ni kumukaba tu koo wmenyekiti wa uchaguzi ili akutangaze wewe ni mshindi.

Harafu wakilalamika wewe fuata ma Olya somalia unawavisha magwanda wanatandika watuu weee wanaua watu weee kisha unachukua watu wako unajifanya kuwapa makazi misikitini/makanisani kisha unawatia moto Na unaanza wewe kulalama jinsi wapinzani wako walivyo magaidi hapo hapo unajifanya wewe mtu wa watu kwa kuomba wapatanishi wa kimataifa.

Kisha Una create Makamu wa Makamo wa RAis Harafu unacreate makamo wa waziri mkuu Hapo tayari utasifiwa sana kwa juhudi ulizofanya za kufanikisha upatanishi.
 
Li-Museven litakuwa limeumbuka hapa!

Kitila sio kweli, alichofanya Museveni ni kumpongeza Kibaki kwa kushinda urais na kumtambua kama mshindi. Kama kuna mtu aliyeumbuka ni Odinga ambaye alishasema from day one kuwa awezi kushirikiana na wezi...na yeye ndiye rais halali wa Kenya. Sasa katika hili ni nani aliyeumbuka.

Bila shaka Nchi za kiafrika hasa Tanzania zimeumbuka. Kwa sasa tumeonyesha hatuna misimamo, tunashindwa kutangaza kuwa tunamtambua mtu kama rais lakini tunampa mapokezi kama mkuu wa Nchi, na mawaziri wake na makamu wa rais alikadhalika tunampa mapokezi yanayolingana na nyadhifa zao. Huu ni unafiki wa kisiasa.
 
Sitaki kuamini kwamba JK kafanya haya kwa muda mfupi vile hapana ila najua kaenda kushuhudia kuweka sahihi makubaliano .

Haina shida, kama mkuu wa kaya yetu kachangia kuleta suluhu tunampongeza! Unaweza kukuta Anna, Condoleeza, Mkapa na wengine walkuwa wanacheza majokeri wakati Madume alikuwa kayalamba JK! Good job papaa, uje utuokoe na huku Pemba.
 
Back
Top Bottom