Tanzania yashika nafasi ya kwanza kwa usambazaji wa Umeme Vijijini Barani Afrika

Tanzania yashika nafasi ya kwanza kwa usambazaji wa Umeme Vijijini Barani Afrika

TANESCO

Official Account
Joined
Jul 12, 2014
Posts
4,600
Reaction score
2,134
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa amesema Tanzania imeshika nafasi ya kwanza barani Afrika kwa kufanikiwa kusambaza umeme nchini kote kwa asilimia 80.

Mhe. Majaliwa aliyasema hayo wakati akielezea mafanikio ya Serikali ya Awamu ya Tano kwenye mkutano wa viongozi wa dini kutoka kamati za amani za Mikoa mbalimbali Tanzania bara na Zanzibar, uliofanyika kwenye Kituo cha Mikutano cha Mwalimu Julius Nyerere (JNICC) jijini Dar es Salaam.

“Leo hii Tanzania ni ya kwanza barani Afrika kwa kusambaza umeme kote nchini hadi vijijini na kufikisha asilimia 80. Kuna nchi ngapi barani Afrika, lakini Tanzania imefanikiwa kuwa ya kwanza. Tumeweza kufikia vijiji 9,112 Tanzania na hadi Aprili 2020 na tumetumia shilingi trilioni 2.27,” amesema.

Akizungumza na viongozi waliohudhuria mkutano huo uliandaliwa ili kuunga mkono juhudi za Rais Dkt. John Pombe Magufuli na Serikali yake katika ustawi wa amani, uzalendo na kumtanguliza Mungu, Waziri Mkuu amesema ushirikiano mkubwa wanauonesha kwa Serikali, umewezesha kufanya mambo mengi ikiwemo kuimarisha huduma za upatikanaji wa nishati kwa ajili ya ustawi wa Watanzania
 
Mnasemea vijiji gani? Kijijini kwetu mbona hamna Umeme? Hata nguzo tu hamna yaani hata ile dalili tu ya kuwekewa umeme hamna.

Mradi wa REA tu wenyewe umeshindikana kumalizika mmeacha nguzo zimesimama mkaondoka sijui mnatuonaje sisi wananchi.
 
Na nyie angalieni uhakika wa taarifa hiyo vizuri kwa kuhakiki taarifa za usambazaji umeme vijijini katika nchi zote 54 za bara la Africa.
 
Naomba mpeleke umeme kwenye kitongoji cha nyamanche na nyamichale katika kijiji cha nyakunguru wilayani Tarime

Wekeni transforma kwenye centre inaitwa nyakato, msambazie watu karibu na hiyo centre.

Kuna machine za kusaga na kukoboa zinasubiri umeme

Kuna ubaguzi katika kugawa umeme

Kuna vitongoji vinarukwa sijui ni kwa maelekezo ya nani
 
Mnasemea vijiji gani? Kijijini kwetu mbona hamna Umeme? Hata nguzo tu hamna yaani hata ile dalili tu ya kuwekewa umeme hamna.

Mradi wa REA tu wenyewe umeshindikana kumalizika mmeacha nguzo zimesimama mkaondoka sijui mnatuonaje sisi wananchi.
Kama hakuna kiongozi mkubwa anatoka kwenye kijiji chenu au kitongoji chenu ,mtasubiri sana. Na taarifa zitaonyesha kuna umeme.
 
Mnafuata kauli ya jukwaani (kisiasa) ya Waziri Mkuu na kuifanya hoja utadhani nyie wenyewe hamjui uhalisia, hovyo kabisa, jana tumejadili hili ni kweli mmejitahidi lakini sio kuwa wa kwanza.
 
Vijiji vingi tu havina umeme.

e.g Mafyeko, kambikatoto no energy supply there.

Mnapika data kuadaa umma. Ndiyo maana mnampasia Majaliwa (mwanasiasa) kuzungumza ili kutimiliza furaha ya kisiasa.
 
Hii ni kweli kabisa, wengine wanaweza kuja kujifunza kwetu. Mtupongeze wananchi tunachangia 3% kwenda REA kila tunaponunua umeme.
 
Nanyi mmekuwa wanasiasa? Ovyo! Imeshajadiliwa humu.
 
Naomba mpeleke umeme kwenye kitongoji cha nyamanche na nyamichale katika kijiji cha nyakunguru wilayani tarime
Wekeni transforma kwenye centre inaitwa nyakato ,msambazie watu karibu na hiyo centre.
kuna machine za kusaga na kukoboa zinasubiri umeme
Kuna ubaguzi katika kugawa umeme
kuna vitongoji vinarukwa sijui ni kwa maelekezo ya nani
Ombi lako limepokelewa rafadhali onyesha namba ya simu
 
Mnasemea vijiji gani? Kijijini kwetu mbona hamna Umeme? Hata nguzo tu hamna yaani hata ile dalili tu ya kuwekewa umeme hamna.

Mradi wa REA tu wenyewe umeshindikana kumalizika mmeacha nguzo zimesimama mkaondoka sijui mnatuonaje sisi wananchi.
Kijiji chenu kipo kwenye hizo 20% zilizobaki ni simple arthimetic progression development fund.
 
Back
Top Bottom