McLaren
JF-Expert Member
- Feb 19, 2025
- 1,170
- 3,743
Taasisi ya EF Education First imetoa orodha ya viwango vya ufasaha wa lugha ya Kiingereza ( EF English Proficiency Index) kwa mwaka 2025, ambapo Tanzania imeorodheshwa katika nafasi ya 11 barani Afrika.
Orodha hiyo inaonyesha Afrika Kusini ikiongoza, ikifuatiwa na Zimbabwe katika nafasi ya pili, huku Kenya ikishika nafasi ya tatu.
Katika kiwango cha dunia, Tanzania imechukua nafasi ya 77 kati ya nchi zilizotathminiwa, katika orodha inayoongozwa na Uholanzi, ikifuatiwa na Croatia na Austria.
Kwa upande wa Afrika Mashariki, Tanzania imeshika nafasi ya tatu, ikitanguliwa na Kenya na Uganda ambazo zote zimeorodheshwa miongoni mwa nchi 10 bora barani Afrika. Rwanda imechukua nafasi ya 20 barani Afrika kulingana na tathmini hiyo.
Source: EF English Proficiency Index
Tanzania Profile on EF Proficiency Index