Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,984
- 13,760
Mkutano huu unalengo la kujadili masuala mbalimbali ya TEHAMA na uwezo wake katika kukuza maendeleo, kuimarisha upatikanaji wa habari na maarifa, kuchochea ustadi na kuhamasisha matumizi ya TEHAMA kwa maendeleo ya kijamii na kiuchumi..Mkutano huu unafanyika jijini Geneva, Uswisi kuanzia tarehe 27 hadi 31 Mei 2024.
Ushiriki wa Tanzania kwenye mkutano huu ni moja ya jitihada katika kuimarisha mashirikiano yake Duniani katika kukabili changamoto mbalimbali katika TEHAMA na kuongeza tija katika utekelezaji wa miradi ya TEHAMA.