Tanzania yashiriki maonesho ya utalii nchini Finland

Habari za Zanzibar

JF-Expert Member
Joined
Dec 18, 2024
Posts
651
Reaction score
433
Ubalozi wa Tanzania nchini Sweden umeratibu na kushiriki katika Maonesho ya Kimataifa ya Utalii ya Matka yanayofanyika jijini Helsinki, Finland, kuanzia tarehe 14-18 Januari, 2026, huku ukitangaza vivutio vya utalii vya Tanzania pamoja na filamu ya Tanzania: The Royal Tour.

IMG-20260117-WA0065.jpg
Maonesho hayo ni miongoni mwa maonesho makubwa barani Ulaya yakijumuisha kampuni 950 za utalii, usafiri wa ndege, vyombo vya habari, na ushauri elekezi wa utalii kutoka duniani kote ambapo katika siku ya kwanza yalipokea washiriki 56,000 wakiwemo watalii watarajiwa.

Kampuni binafsi za Lifestyle Safaris & Holidays na Lifetime Safaris za Tanzania nazo zinashiriki katika maonesho hayo zikiwa na timu ya Ubalozi wa Tanzania. Nchi zingine za Afrika zinazoshiriki ni Uganda, Kenya, Ushelisheli, Namibia, Afrika Kusini, Senegal, Moroko, Tunisia na Misri.

Balozi wa Tanzania nchini Sweden, Mhe. Mobhare Matinyi, anayeiwakilishia pia Tanzania katika nchi za Nodiki, Baltiki na Ukraina, alitumia jukwaa kuelezea namna Tanzania ilivyopata heshima kubwa ya kushinda Tuzo za Utalii za Dunia tarehe 6 Desemba 2025, nchini Bahrain, ikiwa ni mwaka wa tatu mfululizo.

Balozi Matinyi alielezea pia namna Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, alivyoshiriki na kuigiza katika filamu ya kuitangaza Tanzania ya dakika 57 iitwayo Tanzania: The Royal Tour akiwa na mwandishi wa Marekani mshindi wa Tuzo ya Emmy, Peter Greenberg, mwaka 2022.

Balozi Matinyi aliiambia hadhira kwamba Tanzania ina vivutio vitatu kati ya Maajabu Saba ya Asili ya Afrika na pia maeneo saba yanayotambuliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) kama Urithi wa Dunia, akiutaja mathalani Mlima Kilimanjaro, uhamaji mkubwa wa wanyamapori hifadhini Serengeti na bonde la Ngorongoro. Mbali ya hifadhi za taifa 22, Balozi Matinyi pia alitaja utajiri wa utamaduni wa makabila 126 ya Tanzania, hifadhi za historia ya kale kama michoro ya mapangoni ya Kondoa, Mji Mkongwe wa Zanzibar na miji ya Bagamoyo na Kilwa.

Balozi Matinyi pia alitumia maonesho hayo kufanya mazungumzo na wadau mbalimbali wakiwemo Afisa Mtendaji Mkuu wa Atlantic Link, Bi. Karin Gert Nielsen na Mwakilishi wa Danish Travel Show, zote za Denmark, Bw. Johnny Frandsen; Meneja wa kampuni ya Flygresor ya Sweden, Bw. Peter Hallgren; na kwa kampuni za Finland Mwanzilishi na Mkurugenzi Mwendeshaji wa GapEdu, Bw. Jyrki Nilson; Mkurugenzi Mwendeshaji wa Amanihoiva Limited, Bw. Juha Valtanen na Mwakilishi wa Matka Travel Fair, Inkeri Vainik. Mazungumzo hayo yalilenga namna ya kushirikiana katika kuutangaza zaidi utalii wa Tanzania barani Ulaya.

Imetolewa na:
Ubalozi wa Tanzani nchini Sweden,
17 Januari, 2025.

TANZANIA YASHIRIKI MAONESHO YA UTALII NCHINI FINLAND

wakaonyeshe nn? tumeshakuwa maarufu dunia nzma inatufahamu baada ya octaba 29 kwa ushndi wa kishndo 98%
 
Attachments

  • IMG-20260117-WA0063.jpg
    IMG-20260117-WA0063.jpg
    158.7 KB · Views: 31
  • IMG-20260117-WA0065.jpg
    IMG-20260117-WA0065.jpg
    91.2 KB · Views: 35
  • IMG-20260117-WA0064.jpg
    IMG-20260117-WA0064.jpg
    124 KB · Views: 37
  • VID-20260117-WA0069(1).mp4
    12.8 MB
Kwa hio kazi ya balozi ni kutangaza utalii tu hakuna kazi nyingine vijana hawana ajira huku baada awasetie michongo wakwee pipa wakapige kazi mambali huko yeye kakomaa na utalii na mazafuckingroyaltour
 
TANZANIA YASHIRIKI MAONESHO YA UTALII NCHINI FINLAND

Ubalozi wa Tanzania nchini Sweden umeratibu na kushiriki katika Maonesho ya Kimataifa ya Utalii ya Matka yanayofanyika jijini Helsinki, Finland, kuanzia tarehe 14-18 Januari, 2026, huku ukitangaza vivutio vya utalii vya Tanzania pamoja na filamu ya Tanzania: The Royal Tour.

Maonesho hayo ni miongoni mwa maonesho makubwa barani Ulaya yakijumuisha kampuni 950 za utalii, usafiri wa ndege, vyombo vya habari, na ushauri elekezi wa utalii kutoka duniani kote ambapo katika siku ya kwanza yalipokea washiriki 56,000 wakiwemo watalii watarajiwa.

Kampuni binafsi za Lifestyle Safaris & Holidays na Lifetime Safaris za Tanzania nazo zinashiriki katika maonesho hayo zikiwa na timu ya Ubalozi wa Tanzania. Nchi zingine za Afrika zinazoshiriki ni Uganda, Kenya, Ushelisheli, Namibia, Afrika Kusini, Senegal, Moroko, Tunisia na Misri.

Balozi wa Tanzania nchini Sweden, Mhe. Mobhare Matinyi, anayeiwakilishia pia Tanzania katika nchi za Nodiki, Baltiki na Ukraina, alitumia jukwaa kuelezea namna Tanzania ilivyopata heshima kubwa ya kushinda Tuzo za Utalii za Dunia tarehe 6 Desemba 2025, nchini Bahrain, ikiwa ni mwaka wa tatu mfululizo.

Balozi Matinyi alielezea pia namna Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, alivyoshiriki na kuigiza katika filamu ya kuitangaza Tanzania ya dakika 57 iitwayo Tanzania: The Royal Tour akiwa na mwandishi wa Marekani mshindi wa Tuzo ya Emmy, Peter Greenberg, mwaka 2022.

Balozi Matinyi aliiambia hadhira kwamba Tanzania ina vivutio vitatu kati ya Maajabu Saba ya Asili ya Afrika na pia maeneo saba yanayotambuliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) kama Urithi wa Dunia, akiutaja mathalani Mlima Kilimanjaro, uhamaji mkubwa wa wanyamapori hifadhini Serengeti na bonde la Ngorongoro. Mbali ya hifadhi za taifa 22, Balozi Matinyi pia alitaja utajiri wa utamaduni wa makabila 126 ya Tanzania, hifadhi za historia ya kale kama michoro ya mapangoni ya Kondoa, Mji Mkongwe wa Zanzibar na miji ya Bagamoyo na Kilwa.

Balozi Matinyi pia alitumia maonesho hayo kufanya mazungumzo na wadau mbalimbali wakiwemo Afisa Mtendaji Mkuu wa Atlantic Link, Bi. Karin Gert Nielsen na Mwakilishi wa Danish Travel Show, zote za Denmark, Bw. Johnny Frandsen; Meneja wa kampuni ya Flygresor ya Sweden, Bw. Peter Hallgren; na kwa kampuni za Finland Mwanzilishi na Mkurugenzi Mwendeshaji wa GapEdu, Bw. Jyrki Nilson; Mkurugenzi Mwendeshaji wa Amanihoiva Limited, Bw. Juha Valtanen na Mwakilishi wa Matka Travel Fair, Inkeri Vainik. Mazungumzo hayo yalilenga namna ya kushirikiana katika kuutangaza zaidi utalii wa Tanzania barani Ulaya.

Imetolewa na:
Ubalozi wa Tanzani nchini Sweden,
17 Januari, 2025.
Endeleeni kujipiga doko makalioni na kujinusa , pumbavu Kabisa ninyi ,mtalii gani mwendawazimu asiye na akili aje shithole country linaloongozwa na vibaka mataahira yanayoua watu ,kukandamiza haki za binadamu na kujipachika madrakani bila ridhaa ya wananchi
 
Maonesho hayo ni miongoni mwa maonesho makubwa barani Ulaya yakijumuisha kampuni 950 za utalii, usafiri wa ndege, vyombo vya habari, na ushauri elekezi wa utalii kutoka duniani kote ambapo katika siku ya kwanza yalipokea washiriki 56,000 wakiwemo watalii watarajiwa.

Kampuni binafsi za Lifestyle Safaris & Holidays na Lifetime Safaris za Tanzania nazo zinashiriki katika maonesho hayo
Hii ni habari njema, na kwa vile maonesho pia yamehusisha vyombo vya habari, natamani kujua kama kuna chombo chochote cha habari cha Tanzania kimeshiriki.

Pia natamani kujua zaidi ya kampuni binafsi za Lifestyle Safaris & Holidays na Lifetime Safaris za Tanzania zinazoshiriki, je kuna any public company za Tanzania, TTB, Tanapa, NCAA ?

Na mwisho natamani kujua ushiriki wa jirani zetu Wakenya compared to ushiriki wetu ukoje?.

P
 
Back
Top Bottom