Tanzania yashuka katika viwango vipya vya soka duniani

Tanzania yashuka katika viwango vipya vya soka duniani

Suley2019

JF-Expert Member
Joined
Oct 7, 2019
Posts
2,203
Reaction score
5,610
1575003485225.png

Katika viwango vipya vya soka vilivyotolewa na FIFA leo vinaonesha kuwa Tanzania imeshuka nafasi moja katika hivyo na kufikia nafasi ya 134, kutoka 133. Aidha, Kenya imepanda nafasi mbili na kufikia 106, huku Uganda ikipanda nafasi mbili na kufikia 77. Kutokana na viwango hivyo vipya orodha ya timu bora Afrika Mashariki itakuwa:
1.Uganda
2.Kenya
3.Rwanda
4.Tanzania
5.Burundi
6.Sudan Kusini

Wakati kwa Afrika Timu kumi bora zimewekwa kama ifuatavyo:
1. Senegal
2.Tunisia
3. Nigeria
4. Algeria
5. Moroko
6. Ghana
7. Misri
8. Cameroon
9. Mali
10. Congo DR

Na zifuatazo ndio timu kumi bora duniani:
1.Ubelgiji
2.Ufaransa
3.Brazil
4. Uingereza
5.Uruguay
6. Crotia
7. Ureno
8.Hispania
9. Argentina
10.Colombia

Chanzo:Swahili Times
 
Sisi kila siku ni kushuka tu. Watu milioni 55+ wote tuna miguu ya kushoto kweli?
 
kwa upande wa dunia naona list haiko sawa

Argentina, colombia haziwezi mshinda mholanzi kwa form aliyonayo sasa

wametumia vigezo gani?

kwa taifa stars pia siafiki imeshukaje kwani timu inaendelea kufanya vizuri tu licha ya kupoteza game ya mwisho lakini zingine tulifanya vizuri
 
Back
Top Bottom