Tanzania yashuka viwango vya FIFA, yashika nafasi ya 125

Tanzania yashuka viwango vya FIFA, yashika nafasi ya 125

kirerenya

JF-Expert Member
Joined
Aug 27, 2013
Posts
1,696
Reaction score
2,253
stars.jpg

Viwango vya soka duniani kwa mwezi August vimetolewa leo Septemba 14 na shirikisho la soka la Kimataifa FIFA ambapo Tanzania imeshuka kwa nafasi tano licha ya kushinda mchezo wake wa kirafiki wa kalenda ya FIFA dhidi ya Botswana.

Taifa Stars sasa inashika nafasi ya 125 ikiachwa mbali na nchi za Kenya na Uganda ambazo zipo ndani ya nchi 100 bora. Uganda ambayo imecheza michezo miwlli ya kuwania kufuzu kombe la dunia 2018 dhidi ya Misiri na kushinda mchezo mmoja ikipoteza mmoja imepanda kwa nafasi mbili na sasa ianshika nafasi ya 71.

Nchi ya Kenya ambayo nayo inatoka ukanda wa Afrika Mashariki imeshuka nafasi 6 na sasa ipo nafasi ya 88 wakati Rwanda imepanda kwa nafasi moja hadi 118. Misri ndio inaongoza Afrika ikiwa katika nafasi ya 30 baada ya kushuka nafasi 5. Katika orodha hiyo Ujerumani imerejea kwenye namba 1 baada ya kuipiku Brazil ambayo imeshuka hadi nafasi ya 2.

Kumi bora
1. Germany 2. Brazil 3. Portugal 4. Argentina 5. Belgium 6.Poland 7. Switzerland 8. France 9. Chilem 10. Colombia.

Chanzo: EATV
 
Afu huu ndio mchezo ambao watanzania tunaamini tunauweza zaidi BTW maboresho yanahitajika zaidi
 
Labda wanangu wakianza kucheza soka ulaya tutaongoza afrika
 
Kikwete ni rais aliyeipenda socca sana tu mpaka kuolewa Real Madrid kucheza na taifa stars wakiwa wanakwenda SA kwenye world cup
 
Tatizo kulazimisha mchezo ambao hatuwezi

tubaki na shilawadu yetu
 
Wale wacheza Makirikiri tuliowafunga hawakutusogeza?
 
Nahc kwa siasa tanzania tunaweza ongoza kwa kushika namba moja ivo mpira tuwaachie wanaoujua na kuuthamini, team mbovu miundo mbinu mibovu ivo ngoja tuone uongoz ulioingia saiv tff ni kitu gani watakirekebsha....
 
Kikwete ni rais aliyeipenda socca sana tu mpaka kuolewa Real Madrid kucheza na taifa stars wakiwa wanakwenda SA kwenye world cup
we mdigo/mbondei wa Madrid haichezi world cup. Ilikuwa Brazil.

Hata hivyo wakati wa JK timu ya wachezaji waliochezea Madrid zamani ilikuja kucheza na wastaafu wa taifa stars.

NB matumizi ya herufi kubwa na ndogo nimekaushia,usijeniwekea 4/10.
[HASHTAG]#TeamKifimboCheza[/HASHTAG]
 
jamani nani anafahamu vigezo vinavyotumika kupanga hivyo viwango vy soka from FIFA?
Wanaangalia mambo manne

1)matokeo ya mechi. Umeshinda 3,umefungwa au umedroo
2)aina ya mechi kama ni kirafiki au kufuzu au ya fainali ya masindano baada ya kufuzu

3)unayecheza naye anatoka bara gani. Ulaya,america etc kila mmoja kuna point tofauti. Ulaya ni kubwa kuliko.

4) Rank ya uliyecheza naye wakati mnacheza.

Point zinazopatikana hapa zinaunganishwa na ulizokuwa nazo kabla Kwa kanuni fulani .
Kwa maelezo zaidi gugo.
 
we mdigo/mbondei wa Madrid haichezi world cup. Ilikuwa Brazil.

Hata hivyo wakati wa JK timu ya wachezaji waliochezea Madrid zamani ilikuja kucheza na wastaafu wa taifa stars.

NB matumizi ya herufi kubwa na ndogo nimekaushia,usijeniwekea 4/10.
[HASHTAG]#TeamKifimboCheza[/HASHTAG]
Asante Mzingo mwenzangu
 
Back
Top Bottom