Tanzania Yasisitiza Kuimarisha Ushirikiano wa Kimkakati na India

Tanzania Yasisitiza Kuimarisha Ushirikiano wa Kimkakati na India

Habari za Zanzibar

JF-Expert Member
Joined
Dec 18, 2024
Posts
651
Reaction score
433
IMG-20260816-WA0025.jpg


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mheshimiwa Balozi Dkt. Mahmoud Thabit Kombo (Mb), amesema Tanzania imedhamiria kuimarisha ushirikiano wa kimkakati na India, hususan katika sekta za biashara na uwekezaji, ili kuchochea maendeleo endelevu na kuboresha maisha ya wananchi wa nchi hizo mbili.

Waziri Kombo ameyasema hayo katika maadhimisho ya miaka 80 ya Uhuru wa India, ambapo ameipongeza India kwa mafanikio makubwa iliyofikia kwa zaidi ya miongo minane ya kujenga taifa lenye nguvu, demokrasia imara, ubunifu na ustawi.

Amesema mafanikio ya India katika sayansi, teknolojia, elimu, afya, kilimo, viwanda na utawala wa kidemokrasia yanaendelea kuwa mfano wa kuigwa na mataifa mbalimbali duniani, ikiwemo Tanzania, huku akisisitiza kuwa uhuru ni safari endelevu inayohitaji kujitolea, uvumilivu, ubunifu na dhamira ya dhati ya kuitumikia jamii.

IMG-20260816-WA0007.jpg

Mhe. Kombo amempongeza Balozi wa India nchini, Mhe. Bishwadip Dey, kwa jitihada zake za kuimarisha uhusiano wa kihistoria na kirafiki kati ya Tanzania na India, ikiwemo kuwezesha ziara ya Rais wa Zanzibar, Dkt. Hussein Ali Mwinyi, nchini India Julai 2026, pamoja na mafunzo kwa Maafisa 30 wa Huduma za Kigeni, yanayochochea ushirikiano katika diplomasia, elimu na maendeleo.

India ni miongoni mwa wawekezaji watano wakuu nchini Tanzania, ikiwa imewekeza takribani dola bilioni 4.7 za Marekani kupitia miradi 814, hasa katika sekta za uzalishaji, dawa na kilimo.

Aidha, Tanzania hupokea zaidi ya fursa 1,000 za mafunzo kila mwaka katika sekta muhimu zikiwemo TEHAMA, ulinzi na usalama, kilimo, elimu na afya.

Naye Balozi wa India nchini Tanzania, Mhe. Bishwadip Dey, ameelezea dhamira ya India ya kuimarisha ushirikiano na Tanzania katika biashara, uwekezaji, na teknolojia ili kuongeza fursa za maendeleo ya kidijitali kwa wananchi wa nchi zote mbili.

IMG-20260816-WA0030.jpg
IMG-20260816-WA0026.jpg
IMG-20260816-WA0023.jpg
IMG-20260816-WA0029.jpg
IMG-20260816-WA0009.jpg
 

Attachments

  • IMG-20260816-WA0022.jpg
    IMG-20260816-WA0022.jpg
    104.7 KB · Views: 10
  • IMG-20260816-WA0021.jpg
    IMG-20260816-WA0021.jpg
    104.7 KB · Views: 12
  • IMG-20260816-WA0031.jpg
    IMG-20260816-WA0031.jpg
    159.1 KB · Views: 12
  • IMG-20260816-WA0033.jpg
    IMG-20260816-WA0033.jpg
    176.4 KB · Views: 11
  • IMG-20260816-WA0020.jpg
    IMG-20260816-WA0020.jpg
    102.8 KB · Views: 11
  • IMG-20260816-WA0017.jpg
    IMG-20260816-WA0017.jpg
    90.3 KB · Views: 11
  • IMG-20260816-WA0008.jpg
    IMG-20260816-WA0008.jpg
    69.4 KB · Views: 13
Back
Top Bottom