Tanzania yatajwa kuwa miongoni mwa nchi 7 zinazotarajiwa kuwekewa vikwazo vya kuingia Marekani


Source: Trump administration plans to add Nigeria and six other nations to travel ban list: reports
 
Halafu mod Mhariri hizi taarifa tulizifungulia uzi kule jukwaa la Wakenya ambako huwa tunajadili mambo ya EAC na Watanzania wanaokuja huko, naona mumehamisha na kuunganisha huku kwenye siasa za Watanzania, ambako kila taarifa huku hujadiliwa kwa milengo ya siasa za Tanzania, kitu ambacho hakituhusu sisi Wakenya.
Inafaa mfahamu JF imekua international, kuna baadhi ya taarifa mziruhusu zijadiliwe kwingine kwenye level ya kimataifa maana wachangiaji wanatokea mataifa tofauti, sio kusindika kila kitu kiwe kwenye siasa za nchi yenu.
 
Mpango wangu wa kwenda itabidi nighairi

Mambo yasiwe mengi, mengi yasiwe mambo
 
Namba kubwa ya vijana wa Tanzania inajiingiza ISIS, Al-Shabab ect. Yote haya yanasababishwa na kukosa ajira.

Kuwekeza katika nguvu kazi ya vijana ni muhimu.
Si kweli ajira sio kigezo cha uuaji bali ni roho za uuaji zi ndani mwao.ISIS umuona blackman ni kafili kwenye dini anajipendekeza
 
Hakuna social media yeyeto isiyo international ukishaingia kwenye ulimwengu Wa vidole hakuna siri utakayowezaificha
 
Something is wrong hadi nchi yetu ipigwe ban ujue sio kitu cha kawaida
 
Waache watufungie,nani anataka kwenda huko
Hizo ni hasira tu baada ya sera za ushoga kukataliwa,watarudi kivingine wakikwama na ubeberu wao
Vikelele vya namna hii haviwatoi vidonda wala nini
 
Wakiambiwa democrasia imeminywa viongozi wetu wanaweka pamba masikioni haya ndo madhara yake
Jamani hivi kweli MAREKANI kuna demokrasia na inafuata hakai za binadamu? Mbona kila kukicha watu wanauawa katika kumbi za starehe na mashuleni? Pia swala la mapenzi ya jinsi moja si haki kwa utamaduni wa Kiafrika! Tatizo kubwa ni kuibuka kwa Makundi ya Kigaidi yanayozidi kuongezeka katika nchi za Afrika Mashariki, usafirishaji wa binadamu kwa ajili ya biashara ya ngono. Pia bado kuna wanaohusika na biashara haramu ya madawa ya kulevya! Inawezekana wapo wanaojulikana katika uharifu huu.
 
Sababu ya kuwekewa ni kuwa na idadi kubwa ya watu kukaa bila vibali. Halafu sio wanafungia visa zote. Kama Tanzania inaweza kuwa student visa na visiting visa lakini Business visa waruhusu.
have had relatively higher rates of their citizens overstaying visas in the U.S., according to DHS data
Source:Wsj
 
Tamko la Marekani kuhusu chaguzi za Mitaa

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Selemani Jafo amefafanua kuwa uchaguzi wa serikali za mitaa uliofanyika Jumapili iliyopita November 14, 2019 uliendeshwa kwa haki akijibu tamko la nchi za Marekani na Uingereza ambazo zimeukosoa.

Jafo, ambaye ofisi yake ilisimamia uchaguzi huo, aliiambia Mwananchi jana kuwa mchakato wote ulifuata kanuni na sheria za nchi.

Balozi za Marekani na Uingereza nchini, jana zilitoa tamko zikikosoa uchaguzi huo wa serikali za mitaa zikidai haukuwa huru, haukuendeshwa kwa haki na kutengwa kwa wapinzani.

Katika uchaguzi huo, CCM ilishinda vijiji 12,260 sawa na asilimia 99.9, mitaa yote nchini 4,263 sawa na asilimia 100 na vitongoji 63,970 sawa na asilimia 99.4.

Akizungumzia tamko la mataifa ya Marekani na Uingereza, Jafo alisema kwa mujibu wa maadili ya kazi yake hana mamlaka ya kujibu suala hilo isipokuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Profesa Palamagamba Kabudi ingawa alitoa maelezo ya kutetea mchakato huo.

“Sina sababu ya kujibu kwa sababu maadili hayaniruhusu isipokuwa wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa kwa mujibu wa taratibu za kazi. Ila ninachojua uchaguzi ulikuwa wa haki na ulifanyika kwa mujibu kwa kanuni na sheria za nchi.

“Huo ni mtazamo wao (nchi za Marekani na Uingereza), sisi tuliendesha uchaguzi vizuri kwa kufuata kanuni za uchaguzi wa serikali za mitaa za mwaka 2019,” alieleza Jafo.

Jafo alisema uchaguzi huo ulikuwa wa kidemokrasia hakukuwa na mashaka yoyote ndio maana baadhi ya vyama vya upinzani vilitangaza kujitoa katika mchakato huo kwa sababu mbalimbali ingawa baadhi ya wagombea wao wa nafasi mbalimbali waligoma kujitoa,” alisema.

Katika uchaguzi huo, vyama vya upinzani vya Chadema, UPDP, CUF, NCCR-Mageuzi, NLD, Chauma na ACT-Wazalendo vilijitoa kwa kile walichodai kutoridhishwa na mwenendo wa mchakato huo na kulalamikia wagombea wao kutotendewa haki.

Hata hivyo, vyama vya DP, Ada Tadea, NRA, TLP, AAFP vilishiriki uchaguzi huo vikidai sababu zilizotolea na viongozi wa vyama vilivyojitoa hazikuwa na mashiko.

“Ni kweli wapinzani walijitoa lakini baadhi ya wagombea wao hawakukubaliana na hali hii, waligoma kujitoa katika mchakato huu. Mfano mzuri katika wilaya ya Nkasi (Rukwa), Chadema imepata vijiji viwili,” alisema Jafo.

Jafo kuwa Waziri wa Kwanza wa Tanzania kuwekewa vikwazo na Jumuiya ya kimataifa kutokana na muendelezo wa kubinya demokrasia uliohitimishwa November 14, 2019 wakati wa Chaguzi za Serikali za Mitaa na Vijiji
 
Watanzania ni madenialists kishenzzy. Mashoga na ushoga upo Tanzania miaka nenda miaka rudi, hili linajulikana tangu enzi za Nyerere. Kinachotuuma ni kuambiwa kutowabagua. AJABU sana.
 
bagamoyo,
It doesn’t make sense kama uchaguzi haukuwa huru na haki halafu wa ban wananchi wa kawaida kwenda USA!! Hitasaidiaje!!

Tanzania itakuwa ban kwasababu ya Kuwa na idadi kubwa ya VISA OVERSTAYERS!
 
Tusije tukadhani kuwa ni Marekani inataka kutuwekea vikwazo wakati kumbe ni sisi wenyewe tunaumana ndani kwa ndani, na wajanja wameamua kumtumia tu Marekaani ili aonekana kuwa ni yeye! Kumubuka Marekani yeye alisha-abolish permanence; NO PERMANENT FRIEND, NO PERMANENT ENEMY. Hiii kitu mimi nina wasiawsi, yaweza kuwa ni sisi wenyewe. Unajua hapa Tanzania kuna watu wana mipango sana, na hasa kwenye kipindi hiki cha JPM, kisa ameziba mirija yao ya wizi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…