Tanzania yatajwa miongoni mwa nchi kumi bora Afrika kwa uwekezaji. Tarajieni mafuriko ya wawekezaji

Wawekezaji sio wehu hatuna mfumo imara kitawala hivyo haitatokea anaweza akaja aina yamwendazake ikawa shida
 
EeeenHeeee!

Wewe jamaa, hii kazi ya kueneza 'propaganda' hapa JF ni kazi iliyo juu ya uwezo wako sana.

Hayo uliyotaja hapo juu siyo zawadi anayotoa mtu yeyote kwa Taifa lolote. Hiyo ni haki ya jamii ya taifa hilo ambayo hata ikiporwa, kama ilivyokuwa imeporwa chini ya Magufuli, watu wataidai na wataipata tu hakuna wa kuizuia.
Kwa hiyo Samia awepo asiwepo, hayo ni mambo ambayo yatapatikana tu.

Kuhusu kushabikia hicho kipeperushi ambacho pengine hata hujakisoma na kukielewa vizuri, uwekezaji wenye maana zaidi ni ule unaoshirikisha wananchi.
Haitoshi kushangilia uwekezaji, kumbe aina kubwa ya uwekezaji huo ni kupora mali za wananchi na kuzihamisha na kuzipeleka kwingineko. Kwa hiyo, mazingira mazuri ya uwekezaji ni lazima yaendane na juhudi za kuhakikisha kwamba uwekezaji huo ni lazima uwe na manufaa kwetu, na siyo kushangilia tu mradi watu wanakuja hapa kuzoa na kutuacha maskini.

Mwambie huyo 'best' wako, aimarishe maeneo yote yanayohusiana na uwekezaji ili pawe na uwezo wa kuhimili mitifuko inayohusika na watu hao, wengi wao wakiwa ni watu wadanganyifu na wasiojali tunabaki na nini wakati wao wanaponeemeka na mali zetu.

Mwambie 'Best' wako awe na mipango juu ya uwekezaji huo utakaohakikisha bila kubahatisha kuwa tunapata ujuzi tunapowakaribisha hao watu, ujuzi ambao utatuwezesha sisi wenyewe kusimama na kuendesha miradi ya aina wanayoleta hapa hao wawekezaji. Swala la kuajiliwa pekee halina maana sana kama kuajiliwa na kupata ujuzi wa kazi hiyo ili muhusika aweze kwenda akajisimamie mwenyewe kama atahitaji kufanya hivyo

Mwambie huyo 'Best' wako, kila mara anapoleta hao wawekezaji akumbuke kuwa wawekezaji wakuu tunaohapa sisi wenyewe, ambao tumeamua kuwatelekeza kuwa "Machinga". Hawa tunaowaona kila siku wakihangaikia maisha, hii ndio nguvu yetu itakayoliinua taifa hili, na siyo hao tunaotafuta kutoka huko nje. Kwa hiyo ni kazi yake kuunganisha uwekezaji huo na hawa Machinga wetu na wengine watakaolijenga taifa hili kwa uhakika kabisa.

Huyo 'Best' wako akifanya kazi katika misingi hiyo, nami nitaanza kukusifu wewe kwa kumsaidia kuona mwanga wa Tanzania upo wapi.
 
Usipoteze muda wako kuandika hivi better keep quite
Unamaanisha nini hapa.
Kama lugha huiwezi, kwa nini ulazimishe kuitumia? Hii inaonyesha "kipimo"chako ni hafifu (hata sijui kama kweli utanielewa).

Unazidi kujifunua na kujiaibisha.
 
"Tanzania: Tanzania has been on a rapid path of development over the past few years. This growth can be attributed to consistent public investment from the government in key secondary and tertiary sectors, ranging from the energy sector to advancements in the telecommunications and finance sectors". Sina uhakika mleta uzi una uwezo mzuri wa kutafsiri lugha ya watu.
 
S

Sio kweli sijalipwa na Mungu ni shahidi,

Nahisi ni uzalendo wangu tu ndio unanisukuma,

Kuwa na amani tuendelee kuisemea vizuri nchi yetu pendwa
Mlikuwa mnasema hayati Magufuli ni best president lakini leo mnasema alikimbiza wawekezaji, hamuaminiki nyie
 
Hivi TTCL inafanya kitu gani ? Yule dogo pale amekalia propaganda tu atolewe anapoteza muda tu pale Mama vipi tena ?? Aweke watu wenye uwezo .....Kazaura was the best wapo wengine pia...wanaweza kuifumua kuisuka upya ikafanya vzr....wapo...
 
Kwakuwa mmesikia nafasi za Ma DED bado na Ummy kasema mademu wanawagombania mmeanza kuzisaka eee
Rais Samia ameongeza wanafunzi 29,000 kwenye mikopo ya elimu ya juu HESLB kwa miezi sita tu,

miaka mitano mfululizo iliyopita tulifanikiwa wanafunzi wapya 32,000

Unaisemaje kasi ya Rais Samia?
 
Hivi TTCL inafanya kitu gani ? Yule dogo pale amekalia propaganda tu atolewe anapoteza muda tu pale Mama vipi tena ?? Aweke watu wenye uwezo .....Kazaura was the best wapo wengine pia...wanaweza kuifumua kuisuka upya ikafanya vzr....wapo...
Nani huyo mkuu?
 
👇🏿👇🏿👇🏿👇🏿

Kutoka Mwaka 2015/16 hadi 2020/21 pesa iliyoongezwa bodi ya mikopo ilikuwa Tshs 101BL na wanafunzi wapya walikuwa elfu 32 ,

Awamu ya sita kwa miezi sita pesa iliyoongezwa kwenye bodi hiyohiyo ni Tsh 120b na wanafunzi wapya ni elfu 29

Budget ya HESLB kwa mwaka 2015/16 ilikuwa 348.7B kwa wanafunzi 98,300

Budget ya HESLB mwaka 2020/21 ilifikia 450B kwa wanafunzi 130,883

_________________________

Awamu ya sita kwa miezi sita imeongeza budget kutoka 450B za awali hadi 570B za sasa na idadi ya wanufaika imeongezeka na kufikia 160,000.

#Hoja hapa ni muda wa matokeo

#HAKUNA KAMA SAMIA
 
Kundi la majizi yanakuja kwa upya mbabe mlinda raslimali hayupo,mtaandika sana ila Magufuli muhuri wake haufutiki,aliwanyoosha haswa
 
Safi sana go goo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…