Tanzania yatia kiberiti vifaranga 6,400 kutoka Kenya

Sasa wafuasi wa raila walibaki na kura zao nyumbani aliibiwa kura zipi?alafu milango ya koti ipo wazi kama mnahisi hapakuwa na justice hamna atakaye wazuia kuenda huko
 
Du hii kali sasa vifaranga vina makosa gani... WaAfrika kama tumelogwa saa nyingine bora wangegawa kwa wananchi wa Arusha hata kwa siri..
 
Huenda hao vifaranga walikuwa ni GMO wenye vinasaba vyenye madhara kwa afya za watu.
Hata hivyo, tukio la kuvichoma moto liliibua hisia za huzuni miongoni mwa watanzania wengi hasa ukizingatia mwenye navyo alikuwa binti mdogo wa miaka 23 ambaye alipata hasara ya Tsh. 12M.

Ila na nyie wa K mmeshakuwa.Nchi yenye hadhi kama Kenya kendekeza tabia za kivita vita kama S.Sudani ni upumbavu.Kumbe mlitaka mtwangane mkijua mtakimbilia TZ? tulishapokea wakimbizi kutoka Congo, Burundi, Rwanda, SA, Mozambique, Uganda bado na nyie mnataka kuja? Kweli Tanzania ni nchi ya maziwa na asali.
 
Haha jamaa yako kapaniki ,
Umeongea vizuri MK254 jifunzeni kuitunza amani ya nchini kwenu, mtakapoiharibu kuirudisha itawagharimu sana...

Hao vifaranga kweli kuna jambo apo katikati..sisi wabongo pia limetushangaza Ilo jambo...sijui kama waliwapima wakagundua wanatatizo au laah na pia sijaelewa kulikua na ulazima gani kuagiza vifaranga kutoka 254 wakati uku Tz wapo kibao...
 
Mitanzania bana. Mna roho mbaya. Nyeusi kwelikweli . Kuna dhambi kubwa zaidi ya hii? Vifaranga pia vina uraia?
 
Why wachome kumtia mtu hasara,wanaijua biashara ama wanaiskia,na mwingine kakopa huo mtaji sehemu! Acheni kutia wenzenu hasara!

shida waliotekeleza hilo jambo wameajiriwa wanaona mambo ni mepesi hawa wakistaafu hawachelew kufa kwa bp na kisukar kila kitu hawawez
 
MK254
nigekuwa mod lazima ningekulambisha ban.

swali la kujiuliza; ni vifaranga vilichomwa kwa sababu vilitoka Kenya au kwa sababu ukiukwaji wa sheria, kanuni na taratibu za nchi yetu Tanzania??

halafu wewe unaleta uchochezi eti wamechoma simply because they are coming from Kenya. kwa taarifa yako taasisi husika ambazo zimenuia kuwa na a serious total quality control (tqc) zimechoma mavitu yasiyo na idadi mfano vipodozi, maziwa ya watoto, vyakula vya mifugo nk.

huo uchochezi unaoeneza ili kuharibu mahusiano yaliyopo ni kupoteza muda na no one will pay attention on this crap.

halafu uache unafiki. unajifanya kwa wakenya wenzako unapenda peace na togetherness. unamshauri sana Sammuel999 awe na sense of brotherhood. kumbe kwa majirani wewe ni mchochezi nambari wani. huwezi ishi kwa amani ndani kwako ikiwa hupatani na majirani.
 
Kwanini visirudishwe vilipotoka kuliko kuvichoma moto jamani

kwa gharama ya nini!!!!
halafu kwani kuchoma bidhaa zisizokidhi matakwa ya sheria kanuni na taratibu ni wa kwanza huyu.

tumieni vizuri uwezo wenu wa kufikiri.
 

Issue ya kuvichoma kisa ukiukwaji wa sheria hapo mpo sahihi, lakini hasira ya kuvichoma vikiwa hai bila huruma inadhihirisha chuki fulani, bora hata mngevilisha sumu vife kwanza.
Mumekua na vituko vya kiajabu kwa siku za hivi majuzi, mara ng'ombe wote wa Wamaasai mkataifisha kisa wametokea Kenya. Ilhali wale jamii wa hapo mpakani ni kabila moja na ndugu hata kabla mzungu hajaja kuwachorea mpaka, kuna ng'ombe wengi hutokea Tanzania na kuja Kenya pia. Badala ya kutafuta jinsi ya kurekebisha, mkajitoa ufahamu na kutaifisha wote tena kwa hasira kali.

Hamna sehemu nimeeneza uchochezi, labda utakua hujui maana ya hilo neno, nimetoa tahadhari kwa Wakenya wote walinde amani tuliyo nayo, maana matukio ya hizo hasira zenu ni wazi kwamba tukijiingiza kwenye machafuko na kuanza kukimbilia kwenu, basi tutakipata.

Ujumbe huo nimelenga Wakenya wote bila kujali chama au itikadi, sasa sijui Sammuel999 umemtag wa nini kana kwamba yeye ndiye anaharibu amani. Mimi nawalenga Wakenya wote, awe Jubilee au NASA au chochote kingine wanachojiita, lazima tuzingatie amani. Hizi sio zama ambazo nchi majirani walikua wanapokea wakimbizi kiulaini, mambo yameharibika, kwanza sisi Wakenya huwa tumesubiriwa sana siku tuwe wakimbizi, ndio tutakoma.
 

tumia njia nzuri kuhamasisha upendo kati ya wakenya. kutumia njia kama hii ya kujenga uadui na majirani ni kubomoa. maana huwezi kuishi kwa amani ikiwa umezungukwa na maadui. amani nyumbani amani na jirani ndiyo uungwana.
 

namna ya kuviharibu vitu kama hivyo Mimi si mtaalam. sijui lolote huwa naona bidhaa ikiharibiwa. hata juzi nimeona kwenye SABC wanaharibu Jack Daniel za kughushi. kifupi sijui.

kuhusu mifugo ya maasai hilo ndo tunaiita victim of the situation. madhara ya ukoloni hayatatuacha salama. kwa hilo umeongea kwa uchungu sana lifungulie Uzi wake. usichanganye habari.

pia nimemwita Sammuel999 si kama yeye ndiye anayevuruga amani ya Kenya, bali nimemwita ili ashuhudie uchochezi kwa jirani unavyofanya. tofauti na unavyomsihi awapende wakenya wote bila kubagua
 
Mm kama mtz,nalaani vikali ufanyaji wa biashara isiyofuata sheria, BUT,kitendo cha kutketeza viumbe namna ile,is totally inhuman.
 

Kuna tofauti kati ya viumbe hai na bidhaa kama mvinyo, nafikiri kama umeenda shule utakua na uwezo wa kufahamu hilo tofauti. Hata mbwa akimuua mtoto wa binadamu, huwa anadungwa sindano yenye sumu ili afe bila mateso, lakini kutia kiberiti kiumbe chochote sio kabisa, lazima kuna kasoro sehemu.
 

ok boss, so the issue is the methodology of distorting.

le me find out how they were supposed to destroy the living organisms.

aksante.
 

habari ni mgando sasa. auto correct messing with me. lets hug and move on. I stick with justice delivering peace but not wizi wa kura, maombi then lets move on. thats recipe for chaos!!
 
Kitu ambacho mnatakiwa kukijua ni kwamba Yule mfanyabiashara hakuwa na kibali chochote kile cha biashara ile, hata vya kuwanunulia wale vifaranga tu, Kwahiyo hata uhakika wa kwamba wale vifaranga walinunuliwa Kenya haupo kwa mazingira hayo ungekuwa wewe ungewarudisha wapi? Maana hata Kenya wangeweza kukataa kuwa hawajanunuliwa kwao.


Remember hata box zilizobeba hao vifaranga hazikuwa hata na nembo ya mzaalishaji wake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…