Issue ya kuvichoma kisa ukiukwaji wa sheria hapo mpo sahihi, lakini hasira ya kuvichoma vikiwa hai bila huruma inadhihirisha chuki fulani, bora hata mngevilisha sumu vife kwanza.
Mumekua na vituko vya kiajabu kwa siku za hivi majuzi, mara ng'ombe wote wa Wamaasai mkataifisha kisa wametokea Kenya. Ilhali wale jamii wa hapo mpakani ni kabila moja na ndugu hata kabla mzungu hajaja kuwachorea mpaka, kuna ng'ombe wengi hutokea Tanzania na kuja Kenya pia. Badala ya kutafuta jinsi ya kurekebisha, mkajitoa ufahamu na kutaifisha wote tena kwa hasira kali.
Hamna sehemu nimeeneza uchochezi, labda utakua hujui maana ya hilo neno, nimetoa tahadhari kwa Wakenya wote walinde amani tuliyo nayo, maana matukio ya hizo hasira zenu ni wazi kwamba tukijiingiza kwenye machafuko na kuanza kukimbilia kwenu, basi tutakipata.
Ujumbe huo nimelenga Wakenya wote bila kujali chama au itikadi, sasa sijui
Sammuel999 umemtag wa nini kana kwamba yeye ndiye anaharibu amani. Mimi nawalenga Wakenya wote, awe Jubilee au NASA au chochote kingine wanachojiita, lazima tuzingatie amani. Hizi sio zama ambazo nchi majirani walikua wanapokea wakimbizi kiulaini, mambo yameharibika, kwanza sisi Wakenya huwa tumesubiriwa sana siku tuwe wakimbizi, ndio tutakoma.