Tanzania yaungana na Marekani kusherehekea miaka 249 ya uhuru wa Marekani

Tanzania yaungana na Marekani kusherehekea miaka 249 ya uhuru wa Marekani

Ojuolegbha

JF-Expert Member
Joined
Sep 6, 2020
Posts
1,773
Reaction score
1,174
Tanzania imeungana na Marekani kuadhimisha miaka 249 ya Uhuru wa Marekani katika hafla iliyofanyika katika Makazi ya Balozi wa Marekani jijini Dar es Salaam, sambamba na kutimiza miaka 64 ya uhusiano wa kidiplomasia kati ya mataifa hayo.

Akizungumza katika hafla hiyo, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Mahmoud Thabit Kombo, alisema Tanzania inatambua mchango wa Marekani katika sekta za afya, elimu, teknolojia, miundombinu na mafunzo ya kijeshi, ambapo zaidi ya dola bilioni 8 za Kimarekani zimewekezwa kupitia mashirika kama USAID, MCC na Peace Corps.

Mhe. Kombo pia alitambulisha Sera Mpya ya Mambo ya Nje (2021, toleo la 2024), iliyozinduliwa rasmi Mei 2025 na Rais Samia Suluhu Hassan, ambayo inalenga kukuza diplomasia ya kiuchumi, biashara, teknolojia na maendeleo.

Kwa upande wake, Kaimu Balozi wa Marekani nchini Tanzania, Mhe. Andrew Lentz, alitangaza kuwa ifikapo Septemba 2, 2025, USAID itafungwa rasmi ili kuwezesha ushirikiano wa kibiashara wenye matokeo ya moja kwa moja kati ya nchi hizo.

Hafla hiyo ilihudhuriwa na mabalozi wakiwemo wastaafu, viongozi wa serikali, viongozi wa vyama vya siasa, wakuu wa mashirika ya kimataifa na wadau mbalimbali.

publer-1751548156243.jpg
publer-1751548159616.jpg
publer-1751548172758.jpg
 

Attachments

  • publer-1751548161400.jpg
    publer-1751548161400.jpg
    67.8 KB · Views: 31
Back
Top Bottom